9/12/2018

Latest Swahili Christian Video "Njia ya mwenendo wa Binadamu" | Hukumu ya Mungu



Tangu umri mdogo, wazazi wa Cheng Jianguang na walimu walimfundisha sheria kama vile "Uwiano ni hazina, uvumilivu ni wema," "Kunyamazia makosa ya rafiki wazuri hudumisha urafiki mzuri na wa muda mrefu," "Ingawa utaona makosa, ni vyema useme machache" zilikuwa ni nguzo za kudumisha uhusiano mzuri na watu wengine. Alichukua mafunzo haya kwa moyo, na kujifinza kamwe kutowakosea wengine katika matendo na mazungumzo yake, na daima kutunza uhusiano wake na wengine, hivi kumpatia sifa ya "mtu mzuri" kwa wale wliokuwa karibu naye. Baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika zile siku za mwisho, Cheng Jiangunag anajifunza kutoka kwa neno la Mungu kwamba ni kwa kutafuta ukweli na kuwa mtu mwaminifu pekee ndiyo anaweza kupata idhini ya Mungu na kupewa wokovu na Mungu, kwa hivyo anaapa kiapo kuwa mtu mwaminifu. Lakini, katika majukumu yake, yeye anazuiwa na tabia yake potovu, na anashindwa kujizuia kutenda kulingana na falsafa za kishetani za maisha: Wakati anapotambua kiongozi wa kanisa ambaye hatendi kulingana na ukweli katika kazi zake, ambayo inaathiri kazi ya kanisa, Cheng Jianguang anaamua kulinda uhusiano wake na kiongozi yule, na anashindwa kuwasilisha suala hilo upesi; wakati dada mmoja anapokuja kwake kutafuta jibu ambalo litamlazimu yeye kusimama imara na kulinda maslahi ya kanisa, Cheng Jianguang badala yake anachagua kusema uongo, kudanganya, na kukimbia kutoka kwa majukumu yake kwa sababu anaogopa kuwakosea wengine, kusababisha dada zake kukamatwa na serekali ya kikomunisti ya Kichina.... Alipokuwa akifunuliwa tena na tena na mambo ya kimsingi na kuhukumiwa na kufunuliwa katika neno la Mungu, Cheng Jianguang anakuja kuelewa kwamba mantiki na sheria ambazo yeye hutenda ni sumu za kishetani na kwamba jinsi anavyoishi ni tabia ya kishetani. Anakuja kuona kuwa kiini cha kuwa mtu wa ndio ni kile cha mtu mdanganyifu, mtu ambaye Mungu huchukia kabisa na kudharau, na huyo mtu wa ndio asipotubu na kubadikika, yeye bila shaka hataepuka kukataliwa na kuondolewa na Mungu. Anakuja pia kuelewa kwamba ni kwa kuwa mtu mwaminifu pekee ndipo anaweza kuwa mtu mzuri kila mara. Hivyo, yeye anajitahidi kutafuta ukweli na kuwa mtu mwaminifu, na chini ya uongozi wa neno la Mungu, hatimaye anafanikiwa kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu mwaminifu na kutembea katika njia ya wokovu na Mungu.

Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni