Ⅰ
Niliishi katika ulimwengu usio na tumaini, bila kujua ukweli.
Nilisoma neno la Mwenyezi na sasa najua maana ya maisha.
Ni ajabu kuu iliyoje, Kristo analeta mwanga ulimwenguni.
Kutoka kwa hukumu Yake nimepata njia ya uzima wa milele.
Nalithamini neno la Mungu, nauthamini ukweli wa Mungu.
Kumpenda Mungu ni tarajio langu, milele hilo ndilo nitakalofanya.
Kumpenda Mungu ni tamanio langu, nataka kweli. Haleluya!
Ⅱ
Tunakusanyika kanisani; neno linatudumisha.
Najua jinsi ya kuishi maisha yenye thamani na yenye maana sana.
Mungu alinipa ukweli kama uzima, ili niufurahishe moyo Wake,
kutembea katika njia sahihi; shukrani kwa Mungu kwa kuniongoza hadi hapa.
Nilitoka mavumbini, sikuwa chochote kabisa, masikini na hafifu.
Lakini Mungu ameniinua juu.
Kumpenda Mungu ni tarajio langu, milele hilo ndilo nitakalofanya.
Kumpenda Mungu ni tamanio langu, nataka kweli. Haleluya!
Ⅲ
Ni ukweli ambao umenitakasa; neno la Mungu ni kuzaliwa kwangu upya.
Moyo wangu unashukuru; Mungu wa kweli anapendeza vipi.
Neno linafichua ukweli na njia za uovu za mwanadamu.
Mwanadamu ni mwenye majivuno, anajiishia mwenyewe tu.
Neno la Mungu limenitakasa. Sasa naweza kuishi kama mwanadamu
kwa kuelewa ukweli; Mungu anastahili upendo zaidi.
Limekita mizizi moyoni mwangu, neno la Mungu ni njia ya uzima.
Neno Lake limenibadilisha, likinipa maisha mapya.
Nataka kumfuata Mungu, niwe shahidi Wake, nimpende Yeye kwa kweli; hili ndilo tamanio langu.
Nalithamini neno la Mungu, nauthamini ukweli wa Mungu.
Ukweli ni wa thamani vipi! Nimeoshwa katika chemichemi ya uzima ya Mungu.
Kumpenda Mungu ni tarajio langu, milele hilo ndilo nitakalofanya.
Kumpenda Mungu ni tamanio langu, nataka kweli. Haleluya!
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Yaliyopendekezwa : Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni