Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Arubaini na Sita
Sijui jinsi watu wanavyoendelea katika kuyafanya maneno Yangu kuwa msingi wa kuweko kwao. Nimehisi wasiwasi kila mara kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu, lakini watu hawaonekani kuwa na fahamu yoyote kuhusu hili—na kutokana na hilo, hawajawahi kuyatilia maanani mambo Yangu, na hawajawahi kukuza kuabudu kokote kwa ajili ya mtazamo Wangu kuhusiana na mwanadamu.
Ni kana kwamba walitupa hisia zamani ili kuuridhisha moyo Wangu. Nikikumbwa na hali kama hizo, Nakimya mara nyingine. Kwa nini maneno Yangu hayastahili kufikiriwa na watu, kuhusu kuingia zaidi? Je, ni kwa sababu "Sina uhalisi" nami Najaribu kuwa na mamlaka juu ya watu? Kwa nini watu kila mara “hunitendea kwa njia ya pekee"? Je, Mimi ni mgonjwa aliye katika wadi yake pekee maalum? Kwa nini, mambo yakiwa yamefika kiwango ambacho yamefika leo, bado watu huwa na maoni tofauti kunihusu? Je, kuna kosa katika mtazamo Wangu kwa watu? Leo, Nimeanza kazi mpya juu ya ulimwengu. Nimewapa watu walio duniani mwanzo mpya, na Nimewaambia wote watoke nyumbani Mwangu. Na kwa kuwa kila mara watu hupenda kujideka, Nawashauri wajijue, na wasiisumbue kazi Yangu kila mara. Katika "nyumba ya wageni" ambayo Nimeifungua, hakuna kinachotia msukumo chuki Yangu kuliko mwanadamu, kwa sababu kila mara watu huniletea taabu na kunisikitisha. Mwenendo wao huniletea aibu na Sijawahi kuweza kujiamini. Hivyo, Nazungumza nao kwa utulivu, Nikiwataka waondoke nyumbani Kwangu haraka iwezekanavyo na waache kula chakula Changu bila kukilipia. Kama wanataka kubaki, basi lazima wapitie mateso na kuvumilia kuadibu Kwangu. Katika mawazo yao, Sifahamu na Siyajui mambo yao kabisa, na hivyo kila mara wamesimama wima mbele Yangu, bila ishara yoyote ya kuanguka, wakijifanya tu kuwa wanadamu ili kukamilisha idadi. Ninapowahitaji kufanya mambo fulani, wao hushangaa: Hawakuwa wamewahi kufikiri kwamba Mungu, ambaye Amekuwa mwenye ukarimu na mwenye huruma kwa miaka mingi sana, Angeweza kusema maneno kama hayo, maneno ambayo ni ya kikatili na yasiyothibitika, na kwa hiyo wao huduwaa. Nyakati kama hizo, Naona kwamba chuki iliyo ndani ya mioyo ya watu Kwangu imekua mara nyingine, kwa sababu wameanza tena kazi ya kulalamika. Wao kila mara huilaumu dunia na kulaani Mbinguni. Lakini katika maneno yao, Sioni chochote kinachowalaani wao wenyewe kwa sababu wanajipenda sana. Hivyo Nafanya muhtasari wa maana ya maisha ya mwanadamu: Kwa kuwa watu wanajipenda kupita kiasi, maisha yao yote ni ya uchungu na matupu, na wao huwa na uharibifu wa kujitakia kotekote kwa sababu ya chuki yao Kwangu.
Ingawa kuna "upendo" usiosimuliwa katika maneno ya mwanadamu kwa ajili Yangu, Ninapoyapeleka maneno haya katika "maabara" kwa ajili ya upimaji na kuyachunguza chini ya hadubini, yote yaliyo ndani yake hufichuliwa kwa uwazi kabisa. Wakati huu, Naja miongoni mwa wanadamu ili niwaruhusu waone "rekodi zao za matibabu," ili kuwafanya waridhike kwa kweli. Watu wanapoziona, nyuso zao hujaa huzuni, wao huhisi majuto ndani ya mioyo yao—na wao hata wao huwa na wasiwasi sana kiasi cha kuwa na hamu ya kuzitelekeza njia zao za uovu na kurudi kwa njia sahihi ili kunifanya Nifurahi. Ninapoona uamuzi wao, Nafurahishwa kabisa, Najawa na furaha: "Duniani, ni nani pasipo mwanadamu ambaye angeweza kushiriki nami furaha na huzuni? Je, si ni mwanadamu pekee?" Lakini Ninapoondoka, watu huchana rekodi zao za matibabu na kuzitupa sakafuni kabla ya kuondoka kwa mikogo. Katika hizi siku tangu wakati huo, Nimeona machache katika matendo ya watu ambayo yanaupendeza moyo Wangu. Hata hivyo uamuzi wao mbele Yangu umeongezeka mno, na, Ninapotazama uamuzi wao, Nahisi kuchukizwa, kwani ndani yao hakuna kitu kinachoweza kuwa mfano wa kufurahia Kwangu, wametiwa doa kupita kiasi. Wanapoona Ninapuuza uaumzi wao, watu huwa baridi. Baadaye, wanatuma tu "maombi" kwa nadra kwa sababu moyo wa mwanadamu haujawahi kusifiwa mbele Yangu na umewahi tu kukataliwa nami—hakuna tena msaada wowote wa kiroho katika maisha ya watu, na kwa hiyo ari yao hupotea, na Sihisi tena kwamba hali ya hewa ni "yenye joto kali." Watu huteseka sana kotekote katika maisha yao, kiasi kwamba, kwa majilio ya hali ya leo, wanateswa sana nami kiasi kwamba wanakaribia kufa; kwa hiyo, nuru kutoka kwa nyuso zao inafifia, na wanapoteza "kusisimuka" kwao kwani wote "wamekomaa." Siwezi kuvumilia kuona hali ya watu ya kusikitisha wanaposafishwa wakati wa kuadibu—lakini ni nani anaweza kurekebisha hali za mwanadamu zenye taabu? Ni nani anayeweza kumwokoa mwanadamu kutokana na maisha ya mwanadamu yenye taabu? Kwa nini watu hawajawahi kamwe kujinasua kutoka kwa lindi kuu la bahari ya mateso? Je, Mimi huwanasa watu mtegoni kwa makusudi? Watu hawajawahi kamwe kuelewa hali Yangu ya moyo, kwa hiyo Naomboleza kwa ulimwengu kwamba miongoni mwa vitu vyote mbinguni na duniani, hakuna kitu ambacho kimewahi kuutambua moyo Wangu, hakuna kitu ambacho kinanipenda kweli. Hata leo, bado Sijui kwa nini watu hawawezi kunipenda. Wanaweza kunipa mioyo yao, wanaweza kutoa hatima yao kama dhabihu kwa ajili Yangu, lakini ni kwa nini hawawezi kunipa upendo wao? Je, hawana Ninachotaka? Watu wanaweza kupenda kila kitu isipokuwa kunipenda Mimi—kwa hiyo mbona wasinipende? Ni kwa nini upendo wao daima umefichwa? Kwa nini, kwa kuwa wamesimama mbele Yangu mpaka leo, Sijawahi kamwe kuuona upendo wao? Je, hiki ni kitu wanachokosa? Je, Nafanya mambo kuwa magumu kwa watu kwa makusudi? Je, bado wana haya ndani ya mioyo yao? Wanaogopa kumpenda mtu mbaya, na kutoweza kujirekebisha? Ndani ya watu kuna siri nyingi zisizoeleweka, na hivyo Mimi daima huwa "mwenye haya na mwoga" mbele ya mwanadamu.
Leo, wakati wa kusonga mbele kuelekea kwa lango la ufalme, watu wote wanaanza kuendelea mbele—lakini wanapofika mbele ya lango, Nafunga lango, Nawafungia watu nje, na kuwataka waonyeshe pasi zao za kuingia. Kitendo cha ajabu kama hiki hakifanani na kile ambacho watu walikuwa wanatarajia, na wote wanastaajabu. Mbona lango—ambalo kila mara limekuwa wazi kabisa—leo limefungwa ghafla kwa kubanwa? Watu wanakanyaga miguu yao kwa nguvu na kutembea hapa na pale. Wanafikiri kwamba wanaweza kuingia ndani kwa hila, lakini wanaponipa pasi zao za kuingia zisizo halisi, Nazitupa ndani ya shimo la moto papo hapo—na, wanapoona "juhudi zao za kujitahidi" zikiteketea moto, wanakata tamaa. Wanashika vichwa vyao, wakilia, wakitazama mandhari mazuri ndani ya ufalme lakini wasiweze kuingia. Lakini Siwaruhusu kuingia kwa sababu ya hali yao ya kusikitisha—ni nani awezaye kuuvuruga mpango Wangu apendavyo? Je, baraka za siku za baadaye hutolewa kwa kubadilishana na ari ya watu? Je, maana ya kuweko kwa mwanadamu inategemea kuingia katika ufalme Wangu apendavyo mtu? Je, Mimi ni duni sana? Kama sio maneno Yangu makali, je, si watu wasingekuwa wameingia katika ufalme zamani sana? Hivyo, watu hunichukia kila mara kwa ajili ya kero lote ambalo kuweko Kwangu huwasababishia. Kama Nisingekuwepo, wangeweza kufurahia baraka za ufalme wakati wa sasa—na kungekuwa na haja gani kuvumilia mateso haya? Na kwa hiyo Nawaambiwa watu ni heri wangeondoka, kwamba wanapaswa kujinufaisha na jinsi mambo yanavyoendelea vizuri wakati huu ili kujitafutia njia ya kutoka; wanahitaji kujinufaisha na wakati huu, huku wakiwa bado wachanga, kujifunza ujuzi fulani. Wasipofanya hivyo, katika siku za baadaye watakuwa wamechelewa sana. Katika nyumba Yangu, hakuna ambaye amewahi kupokea baraka. Mimi huwaambia watu waharakishe kuondoka, wasishikilie kuishi katika "umaskini"; katika siku za baadaye watakuwa wamechelewa sana kujuta. Msijilaumu sana: mbona ujisumbue? Hata hivyo Mimi pia huwaambia watu kwamba wanapokosa kupata baraka, mtu yeyote asilalamike kunihusu. Sina wakati wa kupotezea maneno Yangu kwa mwanadamu. Natumaini kwamba watu watakumbuka jambo hili, kwamba wasilisahau—maneno haya ni ukweli usio na raha kutoka Kwangu. Nilipoteza imani kwa mwanadamu kitambo sana, Nilipoteza tumaini kwa watu kitambo sana, kwani wanakosa lengo, hawajawahi kuweza kunipa moyo unaompenda Mungu, na wao kila mara hunipa misukumo yao badala yake. Nimesema mengi kwa mwanadamu, na kwa kuwa bado watu wanapuuza ushauri Wangu leo, Mimi huwaambia kuhusu maoni Yangu ili kuwazuia kuuelewa vibaya moyo Wangu katika siku za baadaye; kama wataishi au kufa katika nyakati zijazo ni shauri yao, Sina mamlaka juu ya jambo hili. Natumaini watapata njia yao wenyewe ya kuendelea kuishi, nami Sina mamlaka katika hili. Kwa sababu mwanadamu hanipendi kwa kweli, tunatengana tu; katika siku za baadaye, hakutakuwa tena na maneno yoyote kati yetu, hatutakuwa tena na jambo la kuzungumzia, hatutaingiliana, kila mmoja wetu atashika njia yake, watu wasije kunitafuta, Sitawahi tena kutaka msaada kutoka kwa mwanadamu. Hili ni jambo linalotuhusu sisi, na tumezungumza bila kuwapotosha watu ili kuzuia kuweko kwa masuala yoyote katika siku za baadaye. Je, hili haliyafanyi mambo kuwa rahisi zaidi? Kila mmoja wetu aende njia yake na tusiwe na uhusiano wowote kati yetu—hilo lina kosa gani? Natumaini watu watalifikiria hili.
Mei 28, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni