Kama mtoto, Yangwang aliwafuata wazazi wake katika imani yao kwa Bwana, na kama mtu mzima alihudumia Bwana kanisani. Mnamo 2013, kanisa lake lilijiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni ambalo hutetea uunganishwaji wa kanisa kote ulimwenguni na wingi wa dini. Akisadiki kwamba kusisitiza kwa wachungaji na baraza la wazee wake katika kujiunga na Baraza kulikuwa kuondoka kwa njia ya Bwana na hakuwiani na moyo wa Bwana, hatimaye aliliacha dhehebu lake na kuanza kulitafuta kanisa lililo na kazi ya Roho Mtakatifu.
Lakini, baada ya kuyatembelea makanisa mbalimbali, aligundua kwamba madhehebu yote yalikuwa na ukiwa, na kwamba hakukuwa na nuru katika mahubiri ya wachungaji na mabaraza yao ya wazee. Hakuweza kupata utoaji wa uzima, na roho yake ilikuwa ikinyauka na kugeuka kuwa giza. Kwa maumivu yake, mara nyingi angemuita Bwana, akimwomba Bwana arudiharaka. … Siku moja, alienda mtandaoni kutafutataarifa kuhusu kurudi kwa Bwana, pale alipoiona video ambayo maneno ya Mwenyezi Mungu yalisomwa. Maneno ya Mwenyezi Mungu yaliishtua nafsi yake. Alihisi yalikuwa na mamlaka na nguvu na yalionekana kama sauti ya Mungu. Ili kuamua kama Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, alianza kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kupitia kwa kulisoma neno la Mwenyezi Mungu na kusikia ushirika wa watoaji ushuhuda, aliutatua mkanganyo wake. Aligundua kwamba neno lote la Mwenyezi Mungu ni la ukweli, kwamba kwa hakika ni sauti ya Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu ambaye kurudi kwake alikuwa akisubiri kwa miaka mingi akiutamani. Kwa kuwa, amelisoma neno la Mungu kila siku, hivyo basi kuilisha nafsi yake yenye kiu, na kupokea kwa kweli maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi.
Yaliyopendekezwa :Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni