9/14/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Tisa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Tisa

Kila siku Natembea juu ya ulimwengu, Nikiangalia kwa makini vitu vyote vilivyoumbwa kwa mkono Wangu. Juu ya mbingu ni mahali Pangu pa pumziko, na chini yake ni nchi ambayo Natembea. Natawala kila kitu miongoni mwa vyote vilivyoko, Naamuru kila kitu miongoni mwa vitu vyote, Nikisababisha vyote vilivyoko kufuata hali halisi ya maisha na kutii amri ya asili. Kwa sababu Nawadharau wale wasiotii, na Nawachukia sana wale wanaonipinga na wasiojiunga na wengine, Nitafanya kila kitu kuwa chini ya utaratibu Wangu, bila kupinga, Nitafanya kila kitu ndani ya ulimwengu kiwe na mpango. Nani bado anathubutu kunipinga apendavyo? Ni nani anayethubutu kutotii utaratibu wa mkono Wangu? Mwanadamu anawezaje kupenda hata kidogo kuasi dhidi Yangu? Nitawaleta watu mbele ya "babu” zao, Nitawafanya babu zao wawaongoze kurudia jamii zao, na hawataruhusiwa kuasi dhidi ya babu zao na kurudi upande Wangu. Huo ni mpango Wangu. Leo, Roho Wangu anatembea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa dunia, akigawa tarakimu kwa aina zote za watu, akiweka alama tofauti kwa kila aina ya mtu, ili babu zao waweze kuwaongoza kwa ufanisi kurudia jamii zao na Sihitaji kuendelea "kuwa na wasiwasi" kuwahusu, ambalo linasumbua sana; hivyo, Nagawa kazi pia, na kusambaza juhudi. Hii ni sehemu ya mpango Wangu, na haiwezi kuvurugwa na mtu yeyote. Nitawachagua wawakilishi wanaofaa kutoka katika kila kilichoko ili kusimamia vitu vyote, na kusababisha unyenyekevu wa mpango wa wote walio mbele Yangu. Mimi mara nyingi huzurura juu ya mbingu, na mara nyingi Hutembea chini yake. Nikiitazama dunia kuu ambayo watu huja na kwenda ndani, Nikiwaangalia kwa makini wanadamu, walivyojaa juu ya dunia, na Nikiona ndege na wanyama wanaoishi juu ya sayari, Sina budi kuwa na hisia kubwa moyoni Mwangu. Kwa sababu, wakati wa uumbaji, Niliumba vitu vyote, na ukamilifu wa kila kitu kinatekeleza wajibu wake katika nafasi yake chini ya utaratibu Wangu, Mimi hucheka kutoka juu, na wakati ambapo vitu vyote chini ya mbingu husikia sauti ya kicheko Changu, hivyo mara moja hutiwa moyo, kwani wakati huu shughuli Yangu kubwa hukamilika. Naongeza hekima ya mbinguni ndani ya mwanadamu, kumfanya aniwakilishe miongoni mwa vitu vyote, kwani Nilimuumba mwanadamu ili awe mwakilishi Wangu, sio kunipinga Mimi bali kunisifu katika kina cha moyo wake. Na ni nani awezaye kutimiza maneno haya rahisi? Kwa nini daima mwanadamu hujihifadhia moyo wake? Je, moyo wake si Wangu? Sio kwamba Nataka vitu kutoka kwa mwanadamu bila ya masharti, lakini kwamba yeye daima amekuwa Wangu. Ningewezaje bila mpango kuwapatia wengine vitu ambavyo ni Vyangu? Ningewezaje kutoa "nguo" ambazo Nimezitengeneza kwa mtu mwingine kuvaa? Katika macho ya watu, ni kana kwamba Nimepoteza akili Yangu, Nikiugua ugonjwa wa akili, na Sielewi chochote kuhusu njia za binadamu, ni kama kwamba Mimi ni mpumbavu. Na kwa hiyo, watu daima huniona kuwa mnyofu, lakini hawanipendi kwa dhati. Kwa sababu yote ambayo mwanadamu anafanya ni kwa ajili ya kunidanganya kwa makusudi, Nawakomesha wanadamu wote kwa hasira. Miongoni mwa vitu vyote Nilivyoumba, wanadamu pekee ndio hujaribu kila mara kubuni njia za kunicheza shere, na ni kwa sababu ya hili ndio Nasema kwamba mwanadamu ni "mtawala" wa vitu vyote.
Leo, Nawatupa watu wote katika "tanuru kubwa" ili wasafishwe. Nasimama juu kuangalia kwa makini watu wakichomeka motoni na, kwa kulazimishwa na miale ya moto, watu wanatoa ukweli. Hii ni mojawapo ya njia ambazo kwazo Mimi Hufanya kazi. Kama haingekuwa hivyo, watu wangekiri kuwa "wanyenyekevu," na hakuna mtu ambaye angependa kuwa wa kwanza kufungua mdomo wake kuzungumza juu ya uzoefu wake mwenyewe, lakini wote wangeangaliana tu. Hili hasa ndilo dhihirisho la hekima Yangu, kwa kuwa Niliamua mapema mambo ya leo kabla ya enzi. Hivyo, watu wanaingia ndani ya tanuru bila kujua, kama kwamba wameongozwa huko kwa kamba, kama kwamba wamekuwa wasiosikia. Hakuna mtu anayeweza kuepuka shambulio la ndimi za moto, wao "wanashambuliana," "wanakurupuka huku na huko wakifurahia," bado wakihangaika juu ya hatima yao wenyewe katika tanuru, wakiogopa sana kwamba watateketea hadi kufa. Ninapochochea moto, unakuwa mkubwa mara moja, ukitapakaa mbinguni, na miale yake hukwama kwa majoho Yangu mara kwa mara, kama kwamba inajaribu kuyavuta katika tanuru. Watu wananiangalia kwa macho yaliyokodoa. Mara moja, Naufuata moto ndani ya tanuru, na wakati huu, miale ya moto inaongezeka, na watu wanalia. Nazurura kati ya ndimi za moto. Miale ya moto inazidi, lakini haina nia ya kunidhuru, na Ninatoa majoho yaliyo juu ya mwili Wangu kwa miale ya moto mara nyingine—lakini inakaa mbali na Mimi. Wakati huo tu ndio watu wanaona wazi uso Wangu halisi kwa nuru ya miale ya moto. Kwa sababu wako kati ya joto kali la tanuru, wanakimbia kuelekea pande zote kwa sababu ya uso Wangu, na tanuru inaanza "kuchemka" mara moja. Wote walio katika miale ya moto wanamwona Mwana wa Adamu, ambaye amesafishwa katika ndimi za moto. Ingawa mavazi yaliyo juu ya mwili Wake ni ya kawaida, ni ya uzuri mkubwa kabisa; ingawa viatu vilivyo katika miguu Yake si vya ajabu, vinachochea wivu mkubwa; mng’aro mkali unaangaza kutoka kwa uso Wake, macho Yake yanang’aa, na inaonekana kuwa ni kwa sababu ya nuru iliyo machoni Mwake ndio watu wanaona uso wake halisi kwa dhahiri. Watu wanaingiwa na hofu, na wanaona vazi jeupe juu ya mwili Wake, na nywele Zake, nyeupe kama sufu, zinaning’inia chini kuelekea kwa mabega Yake. Kwa kutambulika, mshipi wa dhahabu juu ya kifua chake unaangaza kwa nuru ya kupofusha, huku viatu vilivyo katika miguu Yake ni vya kuvutia zaidi. Na kwa kuwa viatu vinavyovaliwa na Mwana wa Adamu vinabaki katikati ya moto, watu wanaamini kuwa ni vya ajabu. Ni wakati wa milipuko ya maumivu tu ndio watu huona kinywa cha Mwana wa Adamu. Ingawa wako kati ya usafishaji wa moto, hawaelewi maneno yoyote kutoka kwa kinywa cha Mwana wa Adamu, na hivyo, wakati huu, hawasikii lolote zaidi kuhusu sauti ya kupendeza ya Mwana wa Adamu, lakini wanaona upanga mkali ukiwa ndani ya kinywa Chake, na Hasemi zaidi, lakini upanga Wake unamuumiza mwanadamu. Wakiwa wamezingirwa na miale ya moto, watu wanavumilia maumivu. Kwa sababu ya udadisi wao, wanaendelea kutazama umbo la ajabu la Mwana wa Adamu, na ni wakati huu tu ndio wanagundua kuwa nyota saba katika mkono Wake zimepotea. Kwa sababu Mwana wa Adamu yuko ndani ya tanuru, na sio hapa duniani, zile nyota saba katika mkono wake zinaondolewa, kwa maana ni sitiara tu. Wakati huu, hazitajwi tena, lakini zinagawanywa kwa sehemu mbalimbali za Mwana wa Adamu. Katika kumbukumbu za watu, kuwepo kwa nyota saba kunaleta kero. Leo, mimi Sifanyi mambo kuwa magumu kwa mwanadamu, Naondoa zile nyota saba kutoka kwa Mwana wa Adamu, na Naunganisha sehemu zote za Mwana wa Adamu kuwa kitu kizima. Ni wakati huu tu ambapo mwanadamu anaona umbo Langu lote. Watu hawatatenganisha Roho Wangu na mwili Wangu, kwa kuwa Nimepaa kutoka duniani hadi juu zaidi. Watu wameuona uso Wangu halisi, hawanitenganishi tena, na Sivumilii tena masingizio ya mwanadamu. Kwa sababu Natembea katika tanuru kubwa pamoja na mwanadamu, yeye bado ananitegemea, anahisi kuweko Kwangu katika ufahamu wake. Hivyo, yote ambayo ni dhahabu safi hukusanyika polepole pamoja nami katikati ya kuchomeka kwa moto, ambao ni wakati ule ule ambapo kila moja inaainishwa kulingana na asili. Ninabainisha kila aina ya "chuma," Nikisababisha zote kurudi kwa jamii yake, na sasa tu ndio vitu vyote vinaanza kurudishiwa nguvu ...
Ni kwa sababu mwanadamu ana madoa mengi sana ndio Namtupa ndani ya tanuru ateketezwe. Hata hivyo hakomeshwi na miale ya moto, bali anasafishwa, ili Nipendezwe naye—kwani Ninachotaka ni kitu kilichoundwa kwa dhahabu safi, bila takataka, si vitu vichafu, vyenye najisi. Watu hawaelewi hali Yangu ya moyo, kwa hiyo kabla ya kupanda juu ya "meza ya upasuaji" wanazongwa na wasiwasi, kama kwamba, baada ya kuwachangua, Nitawaua papo hapo wanapolala juu ya meza ya upasuaji. Naelewa hali za watu za moyo, na hivyo Naonekana kuwa mshirika wa wanadamu. Nina huruma nyingi kwa "msiba" wa mwanadamu, na Sijui ni kwa nini mwanadamu "ameugua." Kama angekuwa na afya, na bila ulemavu, kungekuwa na haja gani ya kulipa gharama, na kukaa juu ya meza ya upasuaji? Lakini ukweli hauwezi kufutwa—nani alimwambia mwanadamu asizingatie "usafi wa chakula"? Nani alimwambia asizingatie kuwa na afya? Leo, Nina njia gani nyingine? Ili kuonyesha huruma Yangu kwa mwanadamu, Naingia katika "chumba cha upasuaji" pamoja naye—na ni nani aliniambia Nimpende mwanadamu? Hivyo, Mimi binafsi Nachukua "kisu cha daktari mpasuaji" na kuanza "kufanya upasuaji" kwa mwanadamu ili kuzuia athari zozote zionekanazo baada ya kuugua. Kwa sababu ya uaminifu Wangu kwa mwanadamu, watu walilia machozi katikati ya maumivu kuonyesha shukrani yao Kwangu. Watu wanaamini kuwa Nathamini haki, kwamba Nitasaidia wakati "marafiki" Zangu wako katika shida, na watu wanashukuru zaidi kwa ajili ya wema Wangu, na wanasema watanitumia "zawadi" ugonjwa huo utakapoponywa—lakini Sitilii maanani maneno yao, na badala yake Nalenga kumpasua mwanadamu. Kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu wa mwili, chini ya athari ya kisu yeye huyafumba macho yake na kulala juu ya meza ya upasuaji akiwa ameshtuka—lakini Sijali, Naendelea tu kufanya kazi iliyo mikononi Mwangu. Wakati upasuaji umemalizika, watu wameepuka kutoka kwa "taya za chui mkubwa mwenye milia." Nawastawisha kwa virutubisho vingi, na ingawa hawajui, virutubisho vilivyo ndani yao huongezeka polepole. Kisha Nawatazama Nikitabasamu, na wanaona tu uso Wangu halisi kwa dhahiri baada ya kupata tena afya yao, na kwa hiyo wananipenda zaidi, wananichukulia kama baba yao—na je, huu sio uhusiano kati ya mbingu na dunia?
Mei 4, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi:Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni