11/10/2018

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (4) - Je, Ufalme wa Mbinguni uko Mbinguni au Ulimwenguni?


Watu wengi walio na imani kwa Bwana wanasadiki kwamba ufalme wa mbinguni uko mbinguni. Je, hivyo ndivyo ilivyo kwa kweli? Sala ya Bwana inasema: "Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni" (Mathayo 6:9-10). Kitabu cha Ufunuo kinasema, "Falme za dunia zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake" (Ufunuo 11:15). "Mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni, … maskani ya Mungu yako pamoja na wanadamu" (Ufunuo 21:2-3). Hivyo, ufalme wa mbinguni uko mbinguni au ulimwenguni?

Katika mwanzo wa Februari 1991, mtu fulani katika kanisa alionekana kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, na akaanza kunena, akiwashuhudia jina la Mungu na ujio wa Mungu. Maneno haya yalitumwa kwa makanisa, na baada ya kuyasoma, kila mtu alipatwa na msisimko sana, wote walifurahi mno, na kuamini kwamba hii hakika ilikuwa kupata nuru na maneno ya Roho Mtakatifu. Kuanzia hapo kuendelea, Kristo alianza kuongea. Wakati mwingine Kristo alinena kifungu kimoja kwa siku, wakati mwingine kimoja kila baada ya siku mbili, na matamshi yakawa zaidi na zaidi na mara kwa mara zaidi. Kila mtu aliyapitisha kwa mwenzake na kuhisi msisimko zaidi, mikutano ilijaa furaha, na kila mtu alikuwa amezama katika furaha. Kristo alipoonyesha maneno zaidi na zaidi, watu wote walisikiza kwa makini na kufurahia maneno ya Mungu, na mioyo yao ilinatwa kabisa na maneno ya Mungu. Na hivyo, wakati wa mabaraza, walianza rasmi kufurahia maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu. Wakati huo, watu walikuwa bado hawajatambua kwamba Mungu alikuwa mwili tayari na huku kulikuwa ni kuonekana kwa Kristo. Wao walichukulia tu maonyesho ya Kristo kama nuru ya Roho Mtakatifu iliyopokewa na mtu wa kawaida, kwa sababu katika maonyesho ya Kristo, Yeye hakuwa Amethibitisha rasmi kupata mwili kwa Mungu. Hakuna yeyote aliyeelewa kupata mwili kulikuwa ni nini hasa, na walijua tu kuwa maneno haya yalikuwa nuru ya Roho Mtakatifu.

Sikiliza zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni