Wakati dhambi zetu sisi wanaomwamini Bwana zinasamehewa, je, tunapokea utakaso? Ikiwa hatutajitahidi kupata utakaso, na kujali tu kutumika kwa ajili ya Bwana na kufanya kazi ya Bwana kwa uaminifu, je, tutanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni? Filamu hii ya Kuamka Kutoka kwa Ndoto, itakupa majibu yote!
Mwenyezi Mungu anasema, " Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja."
Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni