1/30/2019

Nyimbo za Injili | Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,nyimbo

Nyimbo za Injili | Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

I
Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia,
unaanza kutenda wajibu wako.
Katika mpango na utaratibu wa Mungu,
unachukua nafasi yako,
na unaanza safari ya maisha.
Vyovyote vilivyo msingi wako
ama safari iliyo mbele yako,
hakuna anayeweza kuepuka utaratibu
na mpango ambao Mbingu imeweka,
na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake,
kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote
ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.
II
Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo
Mungu amekuwa imara katika kazi Yake,
Akisimamia ulimwengu huu na kuelekeza
mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote.
Kama vitu vyote,
mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea
uboreshaji wa utamu,
mvua na umande kutoka kwa Mungu.
Kama vitu vyote,
mwanadamu bila kujua anaishi chini
ya utaratibu wa mkono wa Mungu.
III
Moyo na roho ya mwanadamu
viko mkononi mwa Mungu,
na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa
machoni mwa Mungu.
Bila kujali kama unaamini katika hili ua la,
chochote na vitu vyote,
viishivyo au vilivyokufa,
vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea
kulingana na fikira za Mungu.
Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Tazama Zaidi: Neno la Mungu, Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni