Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (6) - Tofauti Kati ya Njia ya Toba na Njia ya Uzima wa Milele
Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja. Bwana Yesu hufanya kazi ya ukombozi, Yeye anahubiri njia ya toba. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anafanya kazi ya hukumu ya kuwatakasa wanadamu, Yeye huleta njia ya uzima wa milele. Sasa, kama unataka kujua tofauti kati ya njia ya toba na njia ya uzima wa milele, tafadhali angalia hii video fupi.
Mwenyezi Mungu alisema: "Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu."
Yaliyopendekezwa : Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni