2/28/2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 4

Neno la Mwenyezi Mungu  | Sura ya 4

Daima tutakuwa tukiangalia na kusubiri, kuwa na utulivu katika roho na kutafuta kwa moyo safi. Chochote kitakachotufikia, tusishiriki kwa upofu. Twahitajika tu kuwa kimya mbele ya Mungu na daima kushiriki naye, na kisha nia Yake itafichuliwa kwetu. Roho zetu sharti daima ziwe tayari kutofautisha na sharti ziwe na bidii na zisiokubali kushindwa. Ni lazima tuteka kutoka kwa maji ya uhai mbele ya Mungu, maji ambayo huondoa kiu kutoka kwa roho zetu zilizokauka. Ni lazima tuwe tayari wakati wowote, kujitakasa kutokana na haki ya kibinafsi, kiburi chetu, kujiridhisha kibinafsi, na ridhaa yetu, kila moja kuzaliwa kutoka kwa tabia yetu ya kishetani. Ni sharti tufungue mioyo yetu ili kukubali neno la Mungu, sharti tutumainie maneno Yake tunapojishughulisha na maisha yetu. Ni lazima tupitie na tuwe na uhakika juu ya neno Lake na kutimiza ufahamu wa neno Lake. Ni lazima turuhusu neno Lake kuwa maisha yetu. Huu ni wito wetu! Sisi hushinda tu tunapoishi kwa maneno ya Mungu.
Sasa dhana zetu ni kali sana, sisi husema kwa wepesi na kuchukua hatua kwa pupa na hatuwezi kufuata roho. Leo haitakuwa kama zamani; kazi ya Roho Mtakatifu husonga kwa kasi kubwa. Sharti tupitie neno la Mungu kwa undani; kila wazo na fikira, kila mwendo na jibu ni lazima tutofautishe mioyoni mwetu. Hakuna tunachofanya mbele ya mtu au nyuma yao yanaweza kutoroka hukumu mbele ya kiti cha Kristo. Roho Mtakatifu anatuongoza katika maeneo ya uzoefu zaidi, na kwa njia hii ya uzoefu tunakaribia kuwa na uhakika juu ya mwenye Uweza.
Mungu wa ulimwengu Amefungua macho yetu ya kiroho na siri katika roho huendelea kufichuliwa kwetu. Tafuta kwa moyo safi! Kuwa tayari kulipa gharama, songa mbele kwa moyo wako wote, kuwa tayari kujinyima, usiwe na tamaa tena, fuata Roho Mtakatifu na furahia neno la Mungu na kwa ujumla mtu mpya ataonekana. Majaliwa ya Shetani yatafika hatima mbele ya macho yako na mapenzi ya Mungu yatatendeka. Mataifa yote ya dunia yatakuwa Ufalme wa Kristo na Kristo Atatawala kama Mfalme duniani milele!
 kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni