2/17/2019

Nyimbo za Kanisa | Kufuatilia Ukweli ili Kujiokoa Mwenyewe

Ninathibitisha kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima.
Sitapumzika mpaka nimjue Mungu!
Kama siwezi kuvumilia mateso ninayopaswa kubeba, sitastahili kuitwa binadamu kamwe.
Kama siwezi kulipiza upendo wa Mungu nitahisi aibu mno kumwona Yeye.
I
Neno kuonekana katika mwili ni Mungu Mwenyewe.
Yeye ndiye Mungu mwenye mwili wa vitendo katika siku za mwisho.
Kabla ya muda kuanza, Alitabiri kuzaliwa kwangu katika siku za mwisho.
Kupitia kunishinda na kunikomboa, Mungu amenipa uhai Wake.
Mungu amehukumu asili ya binadamu yenye dhambi.
Ameweka wazi uso mbaya na mwovu wa wanadamu wa Shetani.
Nimeaibika nisiwe na mahali pa kujificha, nina aibu kabisa.
Najua kwamba mimi si kitu ila uchafu mdogo.
Sina chochote kilichobaki cha kujivunia.
Ninasujudu chini, moyo wangu umeshindwa.
II
Haki na utakatifu wa Mungu hufunua uasi wangu,
na ninadharau ubaya na uovu wangu hata zaidi.
Uhai halisi wa Mungu ni ukweli.
Moyo wangu una kiu ya ukweli, nitajitahidi kuwa na maendeleo.
Kumjua Mungu kunanitia moyo kufuatilia maisha.
Kuishi kwa maneno Yake kweli ni baraka kubwa.
Nimejielewa kupitia kwa kazi ya Mungu.
Nimeona upotovu wangu wa kina, kwamba mimi sistahili kumtumikia.
Nina hamu ya kutii, kujitoa, na kumpenda Mungu kwa kimya.
Ninahisi kuridhika kwamba ninaweza kumshuhudia.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni