4/20/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Utambulisho

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Mwenyezi Mungu anasema, "Nyie watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwakomboa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika vishawishi vya wanadamu? Na tena, ni mara ngapi mmejikuta katika ugomvi usio na kikomo kati yenu kwa kukosa kuziachilia nafsi zenu? Ni mara ngapi miili yenu imekuwa katika nyumba Yangu ila roho zenu zikiwa kusikojulikana? Licha ya hayo, ni mara ngapi Nimewanyooshea mkono Wangu wa ukombozi; ni mara ngapi Nimewaonea huruma; ni mara ngapi Nimekosa uvumilivu wa kuziona hali zenu za kuhuzunisha za mateso? Ni mara ngapi … hamfahamu?"

Yaliyopendekezwa: Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”.  Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni