“Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni” – Jinsi ya Kufuatilia Ili Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (1) | Swahili Gospel Movie Clip 1/5
Waumini wengi wa Bwana wanahisi kwamba almradi tukiyafuata maneno ya Bwana, tukitenda unyenyekevu na uvumilivu, na kufuata mfano wa Paulo kwa kujitolea, kutumia rasilmali na kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, tutayaridhisha mapenzi ya Mungu. Na tutaletwa katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Hata hivyo, je, tumewahi kufikiria iwapo jitihada kama hizi kweli zitastahili sifa za Bwana na ruhusa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni? Kama sivyo, tunapaswa kufuatilia kupata sifa ya Bwana na kuletwa katika ufalme wa mbinguni vipi?
Mwenyezi Mungu anasema, “ Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu.
Ingawa imani hii ni sahihi, ni ya kuegemea upande mmoja sana; kile ambacho Mungu anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu; ni huduma zaidi na kujitoa ndani ya roho. Ndugu wengi hawajawahi kufikiria juu ya kumfanyia Mungu kazi hata baada ya miaka mingi sana ya uzoefu, maana kazi kama mwanadamu anavyoielewa haipatani na ile ambayo Mungu anaitaka. Kwa hiyo, mwanadamu havutiwi kwa namna yoyote ile na kazi ya Mungu, na hii ndiyo sababu kuingia kwa mwanadamu ni kwa kuegemea upande mmoja kabisa. Nyinyi nyote mnapaswa kuingia kwa kumfanyia Mungu kazi, ili muweze kupata uzoefu wa vipengele vyake vyote. Hiki ndicho mnapaswa kuingia ndani. Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu alio nao kwa Mungu na maarifa aliyo nayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu, na yote ambayo mwanadamu anapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupata uzoefu wa Mungu sio tu kuweza kula na kunywa neno Lake; na muhimu zaidi, mnapaswa kuweza kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia na kumkimu mwanadamu. Hii ni kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza. Kuna watu wengi ambao wanatilia mkazo tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu, lakini hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuza kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu. Kwa miaka mingi sana, wale wanaomtumikia Mungu na kumhudumia mwanadamu wanaona kufanya kazi na kuhubiri kuwa ndio kuingia, na hakuna anayechukulia uzoefu wake binafsi wa kiroho kuwa kuingia muhimu. Badala yake, wanatumia nuru ya kazi ya Roho Mtakatifu kuwafundisha wengine. Wanapohubiri, wanakuwa na mzigo mkubwa sana na wanapokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kupitia hili wanatoa sauti ya Roho Mtakatifu. Wakati huo, wale wanaofanya kazi wanahisi kuridhika kana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wao binafsi wa kiroho; wanahisi kwamba maneno yote wanayoyazungumza wakati huo ni ya yao wenyewe, na pia kana kwamba uzoefu wao si wazi kama walivyoeleza. Kuongezea, wao hawana fununu ya nini cha kusema kabla ya kunena, lakini Roho Mtakatifu anapofanya kazi ndani yao, wao huwa na mtiririko wa maneno usioisha na usiosita. Baada ya kuwa umehubiri kwa namna hiyo, unahisi kwamba kimo chako halisi sio kidogo kama ulivyoamini. Baada ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yako kwa namna ile ile mara kadhaa, basi unaamini kwamba tayari una kimo na unaamini kimakosa kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuingia kwako na asili yako mwenyewe. Unapopitia uzoefu huu kwa mfululizo, unakuwa mzembe kuhusu kuingia kwako. Halafu unakuwa mvivu bila kujua, na kutozingatia kabisa kuingia kwako mwenyewe. Kwa hiyo, unapowahudumia wengine, unapaswa kutofautisha waziwazi kati ya kimo chako na kazi ya Roho Mtakatifu. Hii itasaidia zaidi kuingia kwako na kunufaisha zaidi uzoefu wako. Mwanadamu akidhani kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wake binafsi ndio mwanzo wa upotovu. Hivyo, kazi yoyote mnayoifanya, mnapaswa kuzingatia kuingia kwenu kama somo muhimu.”
kutoka katika Kazi na Kuingia (2)
Tazama Video: Filamu za Injili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni