5/28/2019

“Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni” | Swahili Gospel Movie Clip 5/5


“Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni” – Ushuhuda wa Kupitia Hukumu Mbele ya Kiti cha Kristo na Kupokea Uzima | Swahili Gospel Movie Clip 5/5


Mwenyezi Mungu ameanzisha kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu kwa kuonyesha ukweli. Utangulizi wa hukumu kabla ya ufalme mkuu mweupe kuanza. Tunapitia hukumu ya Mungu na kuadibiwa na Mungu vipi? Je, ni aina gani ya utakaso na mabadiliko yanaweza kupatikana baada ya kupitia hukumu na adabu ya Mungu? Ni maarifa gani ya kweli ya Mungu yanaweza kuarifiwa?

Mwenyezi Mungu anasema, “Leo, mazungumzo juu ya kufanywa mkamilifu ni hali moja tu. Haijalishi kinachofanyika, lazima muwe na hatua hii ya ushuhuda kwa kufaa. Kama mngeulizwa mumhudumie Mungu katika hekalu, mngefanyaje hivyo? Kama hungekuwa kuhani, na hungekuwa na cheo cha wana wazaliwa wa kwanza au wana wa Mungu, bado ungeweza kuwa mwaminifu? Bado ungeweza kufanya yote unayoweza ili kuueneza ufalme? Bado ungeweza kufanya kazi ya agizo la Mungu kwa kufaa? Haijalishi vile maisha yako yamekua, kazi ya leo itakusababisha uridhishwe kabisa ndani yako, na uweke kando dhana zako zote. Kama una kinachohitajika kuyafuatilia maisha au la, kwa jumla, kazi ya Mungu itakufanya uridhike kabisa. Watu wengine husema: Naamini katika Mungu, lakini sielewi ni nini maana ya kuyafuatilia maisha. Na wengine husema: Mimi nimetatanishwa katika imani yangu kwa Mungu. Najua kwamba siwezi kufanywa mkamilifu, kwa hivyo niko tayari kuadibiwa. Hata watu kama hawa, ambao wako tayari kuadibiwa au kuangamizwa, lazima washurutishwe kukubali kwamba kazi ya leo inafanywa na Mungu. Watu wengine pia husema: Siombi kufanywa mkamilifu, lakini, leo, niko radhi kukubali mafundisho yote ya Mungu, na niko radhi kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, kuendeleza uhodari wangu, na kutii mipango yote ya Mungu..... Katika hili, wao pia wameshindwa na kuwa na ushuhuda, ambalo linathibitisha kwamba kuna maarifa fulani ndani ya watu hawa. Hatua hii ya kazi imetekelezwa haraka kabisa, na katika siku za usoni, itatekelezwa hata haraka zaidi ng'ambo. Leo, watu walio ng'ambo hawawezi kungoja, wote wanakimbilia China—na kwa hiyo ikiwa hamwezi kufanywa wakamilifu, mtakuwa mnawashikilia watu walio ng'ambo. Wakati huo, haijalishi vile mlivyo, wakati utakapofika kazi Yangu itahitimishwa na kutimizwa! Sijali kuhusu vile ambavyo mmeingia vizuri au mlivyo ninyi; kazi Yangu yote haiwezi kushikiliwa nanyi. Nafanya kazi ya wanadamu wote, na hakuna haja ya Mimi kutumia muda wowote zaidi kwenu! Ninyi ni wasio na motisha kabisa, wanaokosa kujitambua kabisa! Hamstahili kufanywa wakamilifu—mna uwezo mdogo sana! Katika siku za usoni, hata watu wakiendelea kuwa wazembe na hobelahobela sana, na kubaki wasioweza kuendeleza uhodari wao, hili halitazuia kazi ya ulimwengu mzima. Wakati ukifika wa kazi ya Mungu kumalizika, itamalizika, na wakati ukifika wa watu kuondoshwa, wataondoshwa. Bila shaka, wale wanaopaswa kufanywa wakamilifu, na wanastahili kufanywa wakamilifu, pia watafanywa wakamilifu—lakini ikiwa hamna tumaini kabisa, basi kazi ya Mungu haitawangoja ninyi! Hatimaye, ukishindwa, hili pia linaweza kufikiriwa kama kuwa na ushuhuda; kuna mipaka kwa kile ambacho Mungu anakutaka ufanye. Hata kama kimo ambacho mwanadamu anaweza kutimiza ni cha juu kiasi gani, urefu wa ushuhuda wake unatakiwa kuwa hivyo. Sio kama anavyofikiria mwanadamu kwamba ushuhuda kama huo utafikia mipaka ya juu zaidi na kwamba utakuwa mkubwa sana—hakuna vile hili linaweza kutimizwa ndani ya ninyi watu wa China. Nimeshirikiana nanyi kwa wakati huu wote, na ninyi wenyewe mmeona hili. Nimewaambia msipinge, msiwe waasi, msifanye mambo ya aibu bila Mimi kufahamu. Nimewaambia maneno haya bayana mara nyingi, lakini hata hilo halitoshi—mara tu Ninapogeuka wao hubadilika, na wengine hunipinga Mimi kisirisiri, bila majuto yoyote. Unadhani sijui lolote hili? Unadhani unaweza kunisababishia Mimi matatizo na hakuna kitakachotokea? Unadhani sijui unapojaribu kubomoa kazi Yangu bila Mimi kufahamu? Unadhani kwamba hila zako ndogo zinaweza kushikilia nafasi ya hulka yako? Wewe kila mara unaonekana kuwa mtiifu lakini wewe ni mdanganyifu kisirisiri, unaficha mawazo mabaya ndani ya moyo wako, na hata kifo si adhabu ya kutosha kwa watu kama wewe. Unadhani kwamba kazi kidogo inayofanywa na Roho Mtakatifu ndani yako inaweza kuchukua nafasi ya uchaji wako Kwangu? Unafikiri ulipata nuru kupitia kwa kuiita Mbinguni? Wewe huna aibu! Wewe huna thamani kabisa! Unafikiria kwamba "matendo yako mema" yamegusa Mbinguni, ambayo imefanya jambo la pekee na imekupa vipawa vya asilia vilivyokufanya uwe na lugha ya kushawishi, iliyokukubalia kuwadanganya wengine, na kunidanganya Mimi? Wewe ni mkosa urazini kweli! Je, wajua mahali ambapo nuru yako inatoka? Je, hujui ulikula chakula cha nani ulipokuwa unakua? Wewe ni wa kupita kiasi kweli! Wengine miongoni mwenu hawajabadilika hata baada ya miaka minne au mitano ya kushughulikiwa; mnaelewa kuhusu mambo haya, mnapaswa kuelewa asili yenu—na kwa hiyo msipinge wakati ambapo, siku moja, mtatelekezwa. Wengine, ambao hudanganya wale walio juu na chini yao katika huduma yao, wamepitia ushughulikiaji mwingi sana; wengine, kwa sababu ni wenye tamaa ya pesa, wamepitia ushughulikiaji mwingi sana; wengine, kwa sababu hawaweki mipaka iliyo wazi baina ya wanaume na wanawake, wamepitia ushughulikiaji mwingi sana, wengine kwa sababu ni wavivu, wanaofikiria tu juu ya mwili, na hawatendi haki wanapofika kanisani, wamepitia ushughulikiaji mwingi sana, wengine kwa sababu hukosa kuwa na ushuhuda popote waendapo, na hutenda dhambi na kukosa adabu kwa makusudi, wamekumbushwa mara nyingi; wengine huzungumza kuhusu maneno na mafundisho ya dini wanapofika kanisani, wanajiona wao ni wa cheo cha juu kuliko wengine wote, na hawana uhalisi hata kidogo sana, huku ndugu wakila njama miongoni mwao wenyewe, wakishindana wenyewe kwa wenyewe—wamefichuliwa mara kwa mara kwa sababu ya hili. Nimezungumza maneno haya kwenu mara nyingi sana, na leo, Sitazungumza tena kuhusu hili—fanyeni mtakalo! Fanyeni uamuzi wenu wenyewe! Watu wengi hawajapitia tu ushughulikiaji huu kwa mwaka mmoja au miwili tu, kwa wengine imekuwa miaka mitatu au minne, na wengine wamepitia hili kwa zaidi ya mwongo mmoja, wakiwa wamepitia ushughulikiaji walipogeuka kuwa waumini, lakini kufikia sasa kumekuwa na mabadiliko madogo ndani yao. Unasema nini, wewe sio kama nguruwe? Je, huku ni kukuonea wewe? Msifikiri kwamba kazi ya Mungu haitamalizika ikiwa hamwezi kufikia kiwango fulani. Je, Mungu bado atawangoja ikiwa hamwezi kutimiza matakwa Yake? Nawaambia waziwazi—sivyo hivyo! Usiwe na mtazamo kama huo wa kutia matumaini kuhusu mambo! Kuna muda maalum kwa kazi ya leo hii, Mungu hachezi tu na wewe! Hapo awali, ilipofikia kupitia majaribio ya watendaji huduma, watu walifikiri kwamba kwa wao kusimama imara katika ushuhuda wao kwa Mungu, walitakiwa kushindwa kwa kiwango fulani—walitakiwa kuwa watendaji huduma kwa hiari na kwa furaha, na walitakiwa kumsifu Mungu kila siku, na wasiwe wazembe au wa harara hata kidogo. Walifikiri kwamba ni wakati huo tu ndipo wangekuwa watendaji huduma kweli, lakini hali ni hiyo kwa kweli? Wakati huo, kulikuwa na kila aina ya maonyesho ndani ya watu. Wengine walikimbia, wengine walimpinga Mungu, wengine walifuja pesa za kanisa, na ndugu walikula njama dhidi yao wenyewe, wakilaani na kutukanana wenyewe kwa wenyewe. Ulikuwa ukombozi mkubwa kweli, lakini kulikuwa na kitu kimoja kizuri kulihusu: Hakuna aliyerudi nyuma. Hiki ni kitu bora zaidi kinachoweza kusemwa kulihusu. Walikuwa na ushuhuda mbele ya Shetani kwa sababu ya hili, na baadaye walipata utambulisho wa watu wa Mungu na wakafaulu hata kufikia leo. Kazi ya Mungu haitekelezwi unavyofikiria. Muda ukiisha, kazi hiyo itaisha, haijalishi vile ulivyo. Watu wengine huenda wakasema: Kwa kutenda hivi Huwaokoi watu, au kuwapenda—Wewe si Mungu mwenye haki. Nakwambia waziwazi: Kiini cha kazi Yangu leo ni kukushinda wewe na kukufanya uwe na ushuhuda. Kukuokoa wewe ni kiongezo tu; kama unaweza kuokolewa au la hutegemea ufuatiliaji wako mwenyewe, na hakuhusiani na Mimi. Ilhali lazima Nikushinde wewe; usijaribu kila mara kunidhibiti Mimi—leo Ninakufinyanga, sio vinginevyo!”

 kutoka katika Utendaji (3)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni