V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema
3. Kuna tofauti ipi kati ya maisha ya kanisa katika Enzi ya neema na maisha ya kanisa katika Enzi ya Ufalme?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na wakati walipokuwa wakila, Yesu alichukua mkate, na akaubariki, na kuumega, na akawapa wanafunzi wake, na kusema, Chukueni, kuleni; huu ni mwili wangu. Naye akakichukua kikombe, na kushukuru, na kuwapa akisema, Ninyi nyote kunyweni kutoka katika kikombe hiki; Kwa kuwa hii ni damu yangu ya agano jipya, ambayo inamwagwa kwa ajiki ya msamaha wa dhambi” (Mathayo 26:26-28).
“Nami nikaenda kwa yule malaika, na kumwambia, Nipe kile kitabu kidogo. Naye akaniambia, Kichukue, na ukile; na kitafanya tumbo lako kuwa chungu, lakini kitakuwa kitamu mithili ya asali ndani ya kinywa chako” (Ufunuo 10:9).
Maneno Husika ya Mungu:
Wakati ambapo, katika Enzi ya Neema, Mungu alirudi kwa mbingu ya tatu, kazi ya Mungu ya kuwakomboa wanadamu wote ilikuwa kwa kweli tayari imeendelea katika tendo lake la kumaliza.
Vyote vilivyobaki duniani vilikuwa msalaba ambao Yesu aliubeba, sanda ya kitani ambayo Yesu alifungiwa ndani, na taji ya miiba na joho la rangi nyekundu ambavyo Yesu alivaa (hivi vilikuwa vitu ambavyo Wayahudi walitumia kumdhihaki Yeye). Yaani, kazi ya kusulubiwa kwa Yesu ilikuwa imesababisha ghasia kwa muda na kisha ikatulia. Tangu wakati huo na kuendelea, wanafunzi wa Yesu wakaanza kuendeleza kazi Yake, wakiyachunga na kunyunyizia katika makanisa kila mahali. Maudhui ya kazi yao yalikuwa haya: kuwafanya watu wote watubu, waungame dhambi zao, na wabatizwe; mitume wote wakieneza hadithi ya ndani ya kusulubiwa kwa Yesu na kile kilifanyika kwa kweli, kila mtu asiweze kujizuia kuanguka chini mbele za Yesu kuungama dhambi zake, na zaidi ya hayo mitume wakieneza kila mahali maneno yaliyonenwa na Yesu na sheria na amri Alizozianzisha. Kuanzia wakati huo ujenzi wa makanisa ulianza katika Enzi ya Neema.
kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi yote inayofanywa na mwanadamu ni kufanya wajibu wake kama mmoja wa viumbe na inafanywa akiguswa au kupewa nuru na Roho Mtakatifu. Uongozi ambao watu hao hupeana ni jinsi ya kuzoea katika kila siku ya maisha ya mwanadamu na jinsi mwanadamu anapaswa kutenda kwa maelewano na mapenzi ya Mungu. Kazi ya mwanadamu haihusishi usimamizi wa Mungu ama kuwakilisha kazi ya Roho. Kama mfano, kazi ya Witness Lee na Watchman Nee ilikuwa ni kuongoza njia. Njia iwe mpya au nzee, kazi ilifanywa kwa misingi ya kanuni ya kutozidi Biblia. Haijalishi kama makanisa ya mitaa yalirejeshwa yalivyokuwa awali au yalijengwa, kazi yao ilikuwa ni kuanzisha makanisa. Kazi waliyofanya iliendeleza kazi ambayo Yesu Kristo na mitume Wake walikuwa hawajamaliza au kuendeleza zaidi kwenye Enzi ya Neema. Kile walichofanya katika kazi yao kilikuwa ni kurejesha kile ambacho Yesu Kristo Alikuwa Ameomba katika kazi Yake ya vizazi vitakavyokuja baada Yake Yeye, kama vile kuhakikisha kwamba vichwa vyao vimefunikwa, ubatizo, umegaji mkate, au unywaji wa mvinyo. Inaweza kusemekana kwamba kazi yao ilikuwa kubakia tu kwenye Biblia na kutafuta njia zinazotokana tu na Biblia. Hawakupiga hatua yoyote mpya kamwe. Hivyo basi, mtu anaweza kuona tu ugunduzi wa njia mpya ndani ya Biblia, pamoja na mazoea bora zaidi na yenye uhalisia zaidi. Lakini mtu hawezi kupata katika kazi yao mapenzi ya sasa ya Mungu, isitoshe hawezi kupata kazi mpya ambayo Mungu Atafanya kwenye siku za mwisho. Hii ni kwa sababu njia ambayo walitembelea ilikuwa bado ile nzee; hakukuwa na maendeleo yoyote na kitu chochote kipya. Waliendelea kuufuata ukweli wa “kule kusulubishwa kwa Yesu,” mazoea ya “kuwaomba watu kutubu na kukiri dhambi zao,” msemo kwamba “yule atakayevumilia hata mwisho ataokoka,” na msemo kwamba “mwanamume ndiye kichwa cha mwanamke, na mwanamke lazima amtii mume wake.” Aidha, waliendeleza dhana ya kitamaduni kwamba “akina dada hawawezi kuhubiri, na wanaweza tu kutii.”
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika mikutano maalum ya zamani au mikutano mikuu iliyokuwa katika sehemu mbalimbali, ni kipengele kimoja tu cha vitendo kilichozungumziwa. Vitendo kama hivyo ni vile vilivyotiwa katika vitendo katika Enzi ya Neema na hapakuwa na mfanano wowote na ufahamu wa Mungu kwani maono ya Enzi ya Neema yalikuwa tu maono ya kusulubiwa kwa Yesu, na hapakuwa na maono ya juu zaidi. Mwanadamu hakuhitajika kujua zaidi ya kazi Yake ya ukombozi wa mwanadamu kupitia kusulubiwa, na kwa hivyo katika Enzi ya Neema hapakuwa na maono mengine ya kufahamiwa na mwanadamu. Kwa njia hii, mwanadamu alikuwa na ufahamu mdogo sana wa Mungu na mbali na upendo na huruma za Yesu, kulikuwa na vitu vichache tu vya mwanadamu kuweka katika vitendo, vitu ambavyo vilikuwa tofauti na hali ya leo. Zamani, haikujalisha ni aina gani ya mkutano, mwanadamu hakuwa na uwezo wa kuzungumzia ufahamu wa vitendo wa kazi ya Mungu, aidha hapakuwa na yeyote aliyeweza kusema kwa dhahiri njia iliyokuwa sawa ya utendaji kwa mwanadamu kuiingilia. Aliongeza tu mambo kidogo katika msingi wa stahamala na uvumilivu; hapakuwa na mabadiliko yoyote katika kiini cha vitendo vyake kwani katika enzi hiyo Mungu hakufanya kazi yoyote mpya na matakwa ya pekee Aliyomwekea mwanadamu yalikuwa stahamala na uvumilivu, au kuubeba msalaba. Mbali na vitendo kama hivyo, hapakuwa na maono ya juu zaidi kuliko yale ya kusulubishwa kwa Yesu.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanauliza, “Dada, umeshinda vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kuridhisha matakwa ya moyo Wake.” Mwingine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kumkidhi.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha mambo maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inampinga Mungu. Wale ambao huzingatia uhalisi huwasilisha vyovyote vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao daima huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwingine anaimba, yeye anaanza kukatika, bila hata kugundua kuwa wali katika sufuria yake umeshaungua. Watu wa aina hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni maonyesho ya ukosefu wa ukweli! Wakati watu wengine wanawasiliana kuhusu masuala ya maisha katika roho, ingawa hawasemi kuhusu kuwa wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika uhalisi, si kwa bidii au maonyesho ya nje.
kutoka katika “Kumwamini Mungu Kunapaswa Kulenge Uhalisi, Si Kaida za Kidini” katika Neno Laonekana katika Mwili
“Kushiriki na kuwasiliana kuhusu uzoefu” kunamaanisha kuzungumza kuhusu kila wazo katika moyo wako, hali yako, uzoefu wako na maarifa ya maneno ya Mungu, na pia tabia potovu ndani yako. Na baada ya hayo, wengine wanatambua mambo haya, na kukubali mazuri na kutambua kile kilicho hasi. Huku tu ndiko kushiriki, na huku tu ndiko kuwasiliana kwa kweli. Hakumaanishi tu kuwa na umaizi katika maneno ya Mungu ama sehemu ya wimbo wa kidini, na kuwasiliana upendavyo na kisha kutofanya mengine zaidi, na kutosema chochote kuhusu maisha yako halisi. Kila mtu huongea kuhusu maarifa ya mafundisho na ya nadharia, na hawasemi chochote kuhusu maarifa yaliyotoka kwa uzoefu halisi. Nyote mnaepuka kuzungumza kuhusu vitu kama hivyo, kuhusu maisha yenu binafsi, kuhusu maisha yenu katika kanisa pamoja na ndugu zenu, na kuhusu dunia yenu ya ndani. Kwa kufanya hili, kunawezaje kuwa na kuwasiliana kwa kweli kati ya watu? Kunawezaje kuwa na imani ya kweli? Hakuwezi kuwa hata kidogo! Ikiwa ndugu wanaweza kuambiana siri, kusaidiana, na kuruzukiana wakiwa pamoja, basi kila mtu lazima azungumze kuhusu uzoefu wake binafsi wa kweli. Usipozungumza kuhusu uzoefu wako binafsi wa ukweli, na unazungumza tu maneno yenye kuvutia, na maneno ambayo ni ya mafundisho na ya juu juu, basi wewe si mtu mwaminifu, na huna uwezo wa kuwa mwaminifu.
kutoka katika “Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mnapomshuhudia Mungu, mnapaswa kuzungumza hasa kuhusu jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwaadibu watu, ni majaribio yapi anayoyatumia kuwasafisha wanadamu na kubadilisha tabia za wanadamu, mmestahimili kiasi gani, ni kiasi gani cha uasi na upotovu ambacho kimefichuliwa ndani yenu, na ni kwa njia zipi ambazo mmemkataa Mungu. Kisha mnaweza kuzungumzia jinsi ambavyo hatimaye mnashindwa na Mungu na jinsi mnavyopaswa kumlipa Mungu. Wekeni umuhimu katika lugha ya aina hii, na muiweke kwa njia rahisi. Msijiandae na nadharia zinazoonekana kuu, zilizo tupu ili kujionyesha wenyewe. Hilo linaonekana kama jambo lenye majivuno sana na lisilo na maana. Kuzungumza zaidi kuhusu mambo ya kweli kutoka kwa uzoefu wa vitendo, kuhusu maneno kutoka mioyoni mwenu ndiko kunakowafaidi wengine zaidi na kunakofaa zaidi kwao kuona. Ninyi mlikuwa wale waliompinga Mungu zaidi, wale ambao waliegemea kumtii Mungu kwa kiasi kidogo zaidi, lakini leo mmeshindwa—msisahau hilo kamwe. Masuala ya kipengele hiki yanahitaji kutafakari kwa bidii. Fikirieni zaidi juu ya mambo haya, msije mkafanya vitendo vya aibu na vya kipumbavu.
kutoka katika “Akili ya Msingi Ambayo Mwanadamu Anapaswa Kumiliki” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno halisi ya Mungu: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno halisi ya Mungu. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno halisi ya Mungu, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. … “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli.
kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni