8/20/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 83

Hujui kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu; hujui kwamba mambo yote na vitu vyote viko chini ya udhibiti Wangu! Maana ya kila kitu huumbwa na kukamilishwa na Mimi ni nini? Baraka au misiba ya kila mtu hutegemea utimilifu Wangu, matendo Yangu. Mwanadamu anaweza kufanya nini? Mwanadamu anaweza kufanikisha nini kwa kufikiri? Katika enzi hii ya mwisho, katika enzi hii potovu, katika dunia hii ya giza ambayo Shetani ameipotosha sana, ni kina nani wachache ambao wako jinsi Nipendavyo? Ikiwa ni leo, jana, au katika siku zijazo zisizo mbali, maisha ya kila mtu huamuliwa na Mimi.  Ikiwa wanapokea baraka au kupitia misiba, na kama wanapendwa au kuchukiwa na Mimi yote yaliamuliwa kabisa na Mimi kwa mkupuo mmoja. Nani kati yenu athubutuye kudai kuwa mwendo wako ni wa kujiamulia, kwamba majaliwa yako yako katika udhibiti wako, ni nani athubutuye kufanya hivyo? Ni nani athubutuye kuwa mwasi sana? Ni nani asiyeniogopa Mimi? Ni nani aliye mwasi Kwangu ndani yake? Ni nani athubutuye kutenda kama anavyopenda? Nitamwadibu wakati uo huo, bila shaka kutokuwa tena na huruma kwa wanadamu au kuwaokoa. Wakati huu, yaani, wakati ambapo umekubali jina Langu, ni mara ya mwisho ambapo Nitaonyesha upole kwa wanadamu. Yaani, Nimechagua sehemu ya wanadamu, ambao, hata kama baraka zao sio za milele, wamefurahia neema Yangu kiasi fulani; Kwa hivyo, hata kama haijaamuliwa kabla kuwa utabarikiwa milele, Sikutendei vibaya, na wewe ni bora zaidi kuliko wale ambao watapata msiba moja kwa moja.
Kwa kweli, hukumu Yangu tayari imefika kiwango cha juu, ikiingia katika eneo lisilo na kifani. Hukumu Yangu ii juu ya kila mtu, sasa ni hukumu ya ghadhabu. Hapo zamani ilikuwa hukumu adhimu, tofauti sana na sasa. Watu wa zamani hawakuanza kuhisi hofu kidogo hadi walipokutana na hukumu inayotolewa, sasa wakisikia neno moja tu wanaogopa sana; mtu hata anaogopa Mimi kufungua kinywa Changu. Lakini sauti Yangu ikitoka, Ninapoanza kuzungumza, anaogopa sana hivi kwamba hajui afanye nini, akitamani sana wakati huo kujificha katika shimo ardhini, lililofichwa katika kona lenye giza kuu zaidi. Mtu wa aina hii hawezi kuokolewa kwa sababu ana roho wabaya. Ninapohukumu joka kuu jekundu, Ibilisi, atakuwa mwenye hofu, hata ataogopa kuonwa na watu; kweli yeye ni uzao wa Shetani aliyezaliwa katika giza.
Hapo zamani mara nyingi Nilitumia maneno majaaliwa na uteuzi,” hii ina maana gani hasa? Je, Mimi hujaalia na kuchagua vipi? Kwa nini mtu asiwe mmoja wa waliojaaliwa na kuchaguliwa? Unawezaje kuelewa hili? Haya yote yanahitaji ufafanuzi wa wazi kutoka Kwangu na yote yanahitaji Mimi kunena moja kwa moja. Hili likifunuliwa ndani yenu, mtu mpumbavu wa aina hiyo ataamini kuwa ni wazo ambalo limetolewa na Shetani! Ningekashifiwa bila haki! Sasa Nitazungumza kwa uwazi, bila kuzuia kitu chochote: Nilipoumba vitu vyote, kwanza Niliumba vifaa hivyo vya kutumiwa na wanadamu (maua, nyasi, miti, mbao, milima, mito, maziwa, nchi na bahari, kila aina ya wadudu, ndege, wanyama, wengine ni kwa ajili ya watu kula, baadhi ni kwa ajili ya watu kuangalia), katika maeneo tofauti aina mbalimbali za nafaka ziliumbwa kwa ajili ya wanadamu; ni baada tu ya kuumba haya yote ndipo Nilianza kuwaumba wanadamu. Kuna aina mbili za watu: Aina ya kwanza ni wateule Wangu na waliojaaliwa; aina hiyo nyingine wana tabia ya Shetani. Aina hii waliumbwa kabla ya Mimi kuiumba dunia, lakini wamepotoshwa kabisa na Shetani kwa hivyo Nimewatelekeza. Kisha Nikaumba aina iliyochaguliwa na kuamuliwa kabla na Mimi, kila mmoja akiwa na tabia Zangu kwa kiasi tofauti; kwa hivyo, wale waliochaguliwa na Mimi leo kila mmoja ana tabia Zangu kwa kiasi tofauti. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, bado ni Wangu; kila hatua ni sehemu ya mpango Wangu wa usimamizi. Kwamba utawala wa uaminifu katika ufalme wote ulipangwa kabla ya wakati na Mimi; wale ambao ni wadanganyifu na wenye hila hawawezi kuwa waaminifu bila kujali lolote kwa sababu wao wamezaliwa kutoka kwa Shetani, wanamilikiwa na Shetani, daima ni watumishi wa Shetani walio chini ya amri yake, lakini yote ni kwa ajili ya kutimiza mapenzi Yangu. Nimefanya hilo liwe wazi ili kuondoa kukisia kwenu. Wale Ninaowakamilisha, Nitawatunza na kuwalinda; kwa wale Ninaowachukia, baada ya huduma yao kuisha wataondoka mahali Pangu. Watu hawa wanapotajwa Mimi hukasirika, watajwapo Ninataka sana kuwashughulikia wakati huo huo, lakini Ninajizuia katika vitendo Vyangu; Mimi ni mwenye kufikiria katika vitendo Vyangu na kauli Zangu. Naweza kuunyanyasa ulimwengu kwa hasira, lakini isipokuwa wale Niliowajaalia; baada ya kutulia Ninaweza kushikilia ulimwengu katika kiganja cha mkono Wangu, hiyo ni kusema Mimi hudhibiti kila kitu. Ninapoona ulimwengu umepotoshwa kwa kiasi hicho na Siwezi kuuvumilia, Nitauharibu mara moja. Je, si hilo litahitaji tu neno Langu moja?
Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe; Sifanyi ishara za ajabu na maajabu, lakini kila pahali hujaa kazi Zangu za ajabu. Njia iliyoko mbele itakuwa angavu mno. Ufunuo Wangu wa kila hatua ndio njia Ninayowaonyesha, mpango Wangu wa usimamizi. Hiyo ni kusema, baadaye ufunuo utakuwa mwingi zaidi na wazi zaidi. Hata katika Ufalme wa Milenia, katika siku zijazo zisizo mbali sana, ni lazima mwendelee kulingana na ufunuo Wangu na mwendo Wangu. Yote yamechukua umbo, yote yameandaliwa, waliobarikiwa wana baraka za milele zinazowasubiri; wale waliopigwa wana kuadibu kwa milele kunakowasubiri. Siri Zangu ni nyingi sana kwenu, yale ambayo Kwangu ni maneno rahisi zaidi yaweza yakawa magumu sana kwenu; kwa hiyo, Nasema zaidi na zaidi, kwa sababu ninyi huelewa kidogo sana, na mnahitaji Nieleze neno kwa neno, lakini msiwe na wasiwasi mwingi, Nitawanenea kulingana na kazi Yangu.
Soma Zaidi: Wimbo wa Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni