8/14/2019

Neno la Mungu | Sura ya 116

Kati ya maneno Yangu, mengi huwafanya watu kuhisi woga, mengi huwafanya watu watetemeke kwa hofu; bado mengine mengi sana huwafanya watu kuteseka na kukata tamaa, na bado mengine mengi husababisha uangamizaji wa watu. Wingi wa maneno Yangu, hakuna mtu anayeweza kuelewa au kufahamu vizuri. Ni wakati tu Ninapowaambia maneno Yangu na kuyafichua kwenu sentensi baada ya sentensi ndipo mnaweza kujua hali ya jumla; ukweli wa mambo maalum ya hakika, bado hamuelewi. Basi, Nitatumia ukweli kufichua maneno Yangu yote, hivyo kuwaruhusu mpate ufahamu wa juu zaidi. Ilivyoonekana kutoka kwa mbinu ya usemi Wangu, Sineni tu kwa maneno Yangu, lakini hata zaidi kutenda kwa maneno Yangu; hii tu ndiyo maana ya kweli ya maneno na ufanikishaji kutendeka sawia. Kwani na Mimi kila kitu ni bure, na kila kitu kinaachiliwa, na kwa msingi huu, yote Ninayoyafanya yamejazwa na hekima. Sineni kiholela, na Sitendi kiholela. (Bila kujali iwapo ni katika ubinadamu au uungu, Nanena na kutenda kwa hekima, kwa sababu ubinadamu Wangu ni sehemu isiyotenganika ya Mimi Mwenyewe.) Ilhali Ninaponena, hakuna anayezingatia sauti ya usemi Wangu; Ninapotenda, hakuna anayezingatia mbinu ya kazi Yangu. Huu ni upungufu wa mwanadamu. Nitafichua nguvu Yangu juu ya wanadamu wote, sio tu kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, ila hata zaidi Nitafichua nguvu Yangu ndani ya mataifa yote na watu wote; huu tu ndio ushuhuda wa nguvu wa kumwaibisha Shetani. Sitendi kwa upumbavu; watu wengi hufikiri kwamba ili Nishuhudie wazaliwa wa kwanza ni makosa, wanasema kwamba kuna Mungu wengine kando na Mimi, kwamba Natenda bila akili, kwamba Najishusha hadhi; hivyo kutoka kwa upotovu wa mwanadamu mengi zaidi yanafunuliwa. Inaweza kuwa kwamba ili kushuhudia wazaliwa wa kwanza ni makosa Yangu? Mnasema kwamba Nimekosea, mnaweza kushuhudia? Isingelikuwa kwa sababu kuinuliwa na Mimi, ushuhuda Wangu, bado mngemponda Mwana Wangu chini yenu, bado mngemtendea kwa kutojali kwa dharau, bado mngemtendea kama mtumishi wenu. Kundi hili la wanyama! Nitawamaliza mmoja mmoja! Hakuna atakayeachiliwa! Niambieni, kutolingana na mtu wa ubinadamu wa kawaida, haya ni mambo gani? Bila shaka ni wanyama! Siwezi kuwavumilia kabisa. Ningesubiri ushuhuda wenu, kazi Yangu tayari ingekuwa imecheleweshwa! Kundi hili la wanyama! Hamna ubinadamu kabisa hata kidogo! Sikuhitaji wewe unihudumie! Ondoka hapa sasa hivi! Umemdhulumu Mwana Wangu kwa muda mrefu sana; Nitakukanyaga sana! Thubutu tu kuwa mshenzi tena, thubutu tu kuniaibisha tena! Tayari Nimekamilisha kazi Yangu kuu, na ni wakati wa kugeuka kuondoa kundi hili la wanyama!
Vyote vinakamilishwa mikononi Mwangu (kwa wale Ninaowapenda), na vyote pia vinaangamizwa mikononi Mwangu (kwa wale wanyama ambao Ninachukia, wale watu, masuala na mambo Ninayodharau). Ninawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza kuona yote Ninayotaka kufanya, Ninawaruhusu waelewe kikamilifu, kutoka hapo waone yote ambayo Nimefanya tangu kutoka Sayuni. Baada ya hapo, tutaingia pamoja katika Mlima wa Sayuni, kuingia mahali petu pa kuwa kabla ya enzi, na kuishi maisha yetu upya. Kuanzia hapo kuendelea, hakutakuwa na mawasiliano tena na dunia na kundi hili la wanyama, ila badala yake uhuru kamili, yote hayatazuiliwa na hayatakuwa na kizuizi. Ni nani anayethubutu kumkataa yeyote kati ya wazaliwa Wangu wa kwanza? Ni nani anayethubutu kuwapinga wazaliwa Wangu wa kwazana? Sitamsamehe kwa urahisi! Bila kujali jinsi ambavyo umenicha zamani, leo lazima uwache wazaliwa Wangu wa kwanza vivyo hivyo. Usiwe namna moja mbele Yangu, na namna nyingine nyuma Yangu; Naona jinsi kila mtu yuko kwa uwazi dhahiri. Kutokuwa mwaminifu kwa Mwana Wangu ni kutokuwa na mapenzi ya mtoto kwa mzazi Kwangu, ambao ni ukweli dhahiri, kwani Sisi ni wa mwili mmoja. Ikiwa mtu ni mzuri Kwangu lakini ashikilie mtazamo tofauti kuelekea kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, basi bila shaka ni uzao wa kawaida wa joka kuu jekundu, kwa sababu anavunja mwili wa Kristo; dhambi hii haiwezi kusameheka kamwe! Kila mmoja wenu lazima aone hili. Ni wajibu wenu kunishuhudia, na hata zaidi ni wajibu wenu kuwashuhudia wazaliwa wa kwanza. Hakuna mmoja wenu atakwepa jukumu lake, yeyote atakayeingilia, Nitammaliza mara moja! Usifikiri wewe ni bora sana zaidi. Nakwambia! Kadiri unavyozidi kuwa jinsi hii, ndivyo unavyozidi kuwa mlengwa wa adhabu Yangu kali! Kadiri unavyozidi kuwa jinsi hii, ndivyo unavyozidi kuwa asiye na matumaini na ndivyo unavyozidi kuwa mwana wa kuangamia kabisa, na Nitakuadibu milele!
Kazi Yangu yote inafanywa binafsi na Roho Wangu, na Siruhusu yeyote wa namna ya Shetani kuingilia, ili kuepuka kuvuruga mipango Yangu. Mwishowe, Nitawaacha watu wazima na watoto wote wainuke na kunisifu na wazaliwa Wangu wa kwanza, wasifu matendo Yangu ya ajabu, na kusifu kuonekana kwa nafsi Yangu. Nitaacha sauti ya sifa ingurume kwa miisho ya ulimwengu, ikitikisa milima, mito na vitu vyote, na Nitamwaibisha Shetani kikamilifu; Nitatumia ushuhuda Wangu kuharibu dunia nzima nzee chafu na ovu, na kutengeneza dunia mpya takatifu na safi. (Kwa kusema kwamba jua, mwezi, nyota na sayari za juu hazitabadilika baadaye, Simaanishi kwamba dunia nzee bado iko, ila badala yake kwamba dunia nzima itaharibiwa na dunia nzee itabadilishwa. Sitabadilisha ulimwengu.) Ni hapo tu ndiyo itakuwa dunia inayolingana na mapenzi Yangu; ndani yake hakutakuwa na aina hii ya uonevu leo, tukio la unyonyaji, na itakuwa haki na akili ndani ya mwili kabisa. (Ingawa Nasema itakuwa ya haki na akili, itakuwa ndani ya mwili; ikilinganishwa na ufalme Wangu, itakuwa tofauti sana, tofauti kama mbingu na dunia; hakuna njia ya kulinganisha kabisa—hata hivyo dunia ya binadamu ni dunia ya binadamu, dunia ya roho ni dunia ya roho.) Wakati huo, wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tutatumia mamlaka juu ya dunia kama hiyo (katika dunia hii hakutakuwa na vurugu kutoka kwa Shetani, kwa sababu Shetani atakuwa ameondolewa kabisa na Mimi), lakini maisha yetu bado yatakuwa maisha ya ufalme, na hakuna mtu anayeweza kukana hili. Katika enzi zote, mwanadamu (bila kujali jinsi alivyo mwaminifu) hajawahi kupitia maisha ya aina hii, kwa sababu katika enzi zote hakujawahi kuwa na mtu wa kuchukua wajibu wa mzaliwa Wangu wa kwanza, na bado atanitolea huduma baadaye. Ingawa hawa watendaji huduma ni waaminifu, wao hatimaye ni uzao wa Shetani ambao wameshindwa na Mimi, hivyo baada ya kifo cha mwili bado wanazaliwa ndani ya dunia ya binadamu kufanya huduma kwa ajili Yangu; hii ndiyo maana ya kweli ya “wana hata hivyo ni wana, na watendaji huduma hata hivyo ni uzao wa Shetani.” Katika enzi zote haijulikani ni watu wangapi waliopo wa kufanya huduma kwa ajili ya wazaliwa wa kwanza wa leo; kati ya watendaji huduma wote, hakuna anayeweza kutoroka, na Nitawafanya wanihudumie milele. Na kuhusu asili zao, wote ni wana wa Shetani, wote hunipinga Mimi, na ingawa wananifanyia huduma, wote wanalazimishwa, wote hawana mbadala, kwa sababu kila kitu kinadhibitiwa na mkono Wangu; watendaji huduma Ninaowatumia lazima wanihudumie hadi mwisho. Hivyo, bado kuna watu wengi leo ambao wana asili sawa na manabii na mitume katika enzi zote, kwa sababu wao ni wa roho moja. Hivyo, bado kuna watendaji huduma wengi waaminifu wanaokimbia kwa ajili Yangu, lakini mwishowe (kwa zaidi ya miaka elfu sita wamekuwa wakinihudumia siku zote, kwa hivyo watu hawa ni miongoni mwa watendaji huduma), hakuna mtu anayeweza kupata kile ambacho wale katika enzi zote wamekitumainia, kwa kuwa kile ambacho Nimetayarisha si kwa ajili yao.
Kila kitu Changu tayari kimekamilishwa mbele ya macho; Nitawafanya wazaliwa Wangu wa kwanza warudi nyumbani Kwangu, warudi kwa upande Wangu na wapatane. Kwa sababu Nimerudi kwa shangwe na ushindi na Nimepata utukufu kikamilifu, Naja kuwarudisha. Zamani, watu wengine wamefanya utabiri kuhusu “mabikira watano wenye busara, mabikira watano wapumbavu”; ingawa utabiri huo si sahihi, si wenye makosa kabisa, kwa hiyo Naweza kuwapa ninyi maelezo fulani. Mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu hakika hawawakilishi idadi ya watu, wala hawawakilishi watu wa aina moja mtawalia. Mabikira watano wenye busara wanamaanisha idadi ya watu, mabikira watano wapumbavu wanawakilisha watu wa aina moja, lakini hakuna kati ya hivi viwili vinarejelea wazaliwa wa kwanza, na badala yake vinawakilisha uumbaji. Hii ndiyo maana wameulizwa waandae mafuta katika siku za mwisho. (Uumbaji hauna sifa Yangu; kama wanataka kufanya wale wenye busara wanahitaji kuandaa mafuta, na hivyo wanahitaji kujitayarisha na maneno Yangu.) Mabikira watano wenye busara wanawakilisha wana Wangu na watu Wangu kati ya wanadamu ambao Niliumba. Kuwaita[a] “mabikira” ni kwa sababu ingawa wamezaliwa duniani, bado wanapatwa na Mimi; mtu anaweza kusema kwamba wamekuwa watakatifu, kwa hivyo wanaitwa “mabikira.” “Watano” liliotajwa awali linawakilisha idadi ya wana Wangu na watu Wangu ambao Nimewajaalia. “Mabikira watano wapumbavu” linarejelea watendaji huduma. Wananifanyia huduma bila kuweka kiwango kidogo zaidi cha umuhimu kwa maisha, wakifuatilia mambo ya nje pekee (kwa sababu hawana sifa Yangu, bila kujali kile wanachokifanya ni jambo la nje), na hawawezi kuwa wasaidizi Wangu wenye uwezo, kwa hiyo wanaitwa “mabikira wapumbavu.” “Watano” lililotajwa awali linamwakilisha Shetani, na wao kuitwa[b] “mabikira” kunamaanisha kwamba wameshindwa na Mimi na wanaweza kunifanyia huduma, lakini mtu wa aina hii si mtakatifu, kwa hivyo wanaitwa watendaji huduma.
Tanbihi:
a. Maandiko ya awali hayana neno “Kuwaita.”
b. Maandiko ya awali hayana maneno “wao kuitwa.”
Chanzo: Sura ya 116
"Umeme Kutoka Mashariki Unaangaza Kwelekea Magharibi
Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, Kumeleta Enzi Mpya"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni