10/01/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 32

Mwanga ni nini? Katika siku za nyuma kwa kweli mliuona mbadiliko wa kazi ya Roho Mtakatifu kama mwanga. Kuna mwanga wa kweli wakati wote, unaojumuisha ninyi kupata kile Mungu alicho kupitia kwa kunikaribia na kushirikiana na Mimi; kuwa na utambuzi katika maneno ya Mungu na kufahamu mapenzi ya Mungu katika maneno Yake—yaani, mnapokula na kunywa, mnahisi Roho wa maneno ya Mungu na kupokea maneno ya Mungu ndani yenu; mkielewa kile Alicho kupitia uzoefu na kupokea mwangaza wa Mungu huku mkizungumza na Yeye; na pia kupewa nuru na kuwa na utambuzi mpya katika maneno ya Mungu wakati wote huku mkifikiria na kutafakari. Ukielewa neno la Mungu na uhisi mwanga mpya, basi hutakuwa na nguvu katika huduma yako? Ninyi hujitia wasiwasi sana katika huduma yenu! Hiyo ni kwa sababu ninyi hamjagusa ukweli, hamna uzoefu wa kweli au utambuzi. Kama ungekuwa na utambuzi wa kweli, basi si ungejua jinsi ya kuhudumu? Wakati masuala mengine yanakujia, lazima uyapitie kwa bidii. Ikiwa, katika mazingira rahisi na yenye starehe, unaweza pia kuishi katika mwanga wa uso wa Mungu, basi utauona uso wa Mungu kila siku. Ungeuona uso wa Mungu na uwasiliane na Mungu, je, hungekuwa na mwanga? Ninyi hamuingii katika hali halisi, na daima mko upande wa nje mkitafuta; kutokana na hili hampati chochote na maendeleo yenu katika maisha yanacheleweshwa.
Msizingatie upande wa nje; mkisonga tu karibu na Mungu kwa ndani, muwasiliane kwa kina vya kutosha, na mhisi mapenzi ya Mungu, basi hamtakuwa na njia katika huduma yenu? Mnapaswa kuwa makini kwa bidii na kutii. Mkifanya tu mambo yote kulingana na maneno Yangu na kuingia katika njia ambazo Ninaonyesha, basi hamtakuwa na njia? Ukipata njia ya kuingia katika uhalisi, basi pia una njia ya kumtumikia Mungu. Ni rahisi! Njoo katika uwepo wa Mungu zaidi, tafakarini maneno ya Mungu zaidi, na utapata kile ambacho umepungukiwa nacho. Utakuwa pia na utambuzi mpya, nuru mpya, na utakuwa na mwanga.

Unaweza Pia Kupenda: Ni Wale Wanaokubali Ukweli Tu Ndio Wanaweza Kuisikia Sauti ya Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni