Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Amri-ya-Yehova-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Amri-ya-Yehova-Mungu. Onyesha machapisho yote

11/24/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo.Mnaelewa? Rudieni nyuma Yangu: kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu.