Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Bwana. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Bwana. Onyesha machapisho yote

9/10/2017

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani"

Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani


Nimerudi kwa familia ya Mungu, mchangamfu na mwenye furaha.
Mikono yangu imemshika mpendwa wangu, moyo wangu ni miliki Yake.
Japo nimepitia Bonde la Machozi, nimeyaona mapenzi ya Mungu.
Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku, Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu.
Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu.
Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.

9/08/2017

Umeme wa Mashariki | Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" (Video Rasmi ya Muziki)

Nitampenda Mungu Milele

Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.
Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.
Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.
Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,
na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.
Lakini Hujawahi kuniacha.
Uliniongoza kupitia matatizo mengi, Umeniweka kupitia hatari nyingi.
Sasa najua ya kuwa Wewe Umenipenda.

Ee Mungu! Waniongoza kwa maisha mapya.
Nikifurahia Maneno yako, Nimeelewa mapenzi yako.
Maneno yako hunihukumu na kuniadibu, na kutakasa upotovu wangu.
Kupitia majaribio nimejifunza kukutii Wewe.
Kukua katika neno la Mungu, nimekuja kumjua Mungu.
Niko tayari kufanya wajibu wangu kwa shahidi Wako na utukufu.

9/06/2017

Umeme wa Mashariki | Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

 Umeme wa Mashariki |1. Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake


Kama wale mamia ya mamilioni ya wengine wanaomfuata Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa pia wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kuwa kwenye njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni.