Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote

11/17/2019

Watu wanafaa kupitiaje hukumu na adabu ya Mungu ili kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:

Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu.Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji. 

11/16/2019

Kwa nini inamlazimu Mungu kuwahukumu na kuwaadibu watu?

Maneno Husika ya Mungu:

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

11/15/2019

Hukumu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

10/26/2019

Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days


Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days


Chen Peng alikuwa mchungaji katika kanisa la nyumba fulani. Alikuwa akimtumikia Bwana kwa bidii, na mara nyingi alifanya kazi kama mhubiri, akiwasaidia wafuasi wake, na kulibebea kanisa mizigo mizito. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kanisa lilizidi kuwa tupu zaidi na zaidi. Waumini walikuwa na roho dhaifu na wavivu, wakikosa mkutano baada ya mkutano. Na hivyo Mchungaji Chen aliona giza likiangukia nafsi yake, kana kwamba kisima cha roho yake kilikuwa kikavu, na hakuweza kuhisi uwepo wa Bwana. Katika mikutano, aligundua kwamba hakuwa na kitu alichoweza kuhubiri. ... Alifanya kila kitu alichoweza kufikiria ili kuimarisha kanisa, lakini jitihada zake zote zilikuwa bure. ... Chen Peng alikuwa amesitikika, amepotea, na hakuweza kuelewa kwa nini kanisa lake lilikuwa linajawa na ukiwa sana, na kwa nini walikuwa wamepoteza uwepo wa Bwana.