Maneno Husika ya Mungu:
Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.
kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu.
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja.
kutoka katika “Kuhusu Majina na Utambulisho” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema kwamba kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu? Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa.
Kutokana na maneno yaliyonenwa na Mungu inaweza kuonekana kwamba tayari Ameulaani mwili wa mwanadamu. Je, haya maneno, basi, ni maneno ya laana? Maneno yaliyonenwa na Mungu hufichua tabia halisi ya mwanadamu, na kupitia ufichuzi kama huo unahukumiwa, na unapoona kwamba huwezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, ndani unahisi huzuni na majuto, unahisi kwamba unapaswa kumshukuru Mungu sana, na usiyetosha kwa ajili mapenzi ya Mungu. Kuna nyakati ambapo Roho wa Mungu hukufundisha nidhamu kutoka ndani, na nidhamu hii hutoka kwa hukumu ya Mungu; kuna nyakati ambapo Mungu hukushutumu na kuuficha uso Wake kutoka kwako, wakati ambapo hakusikilizi, na Hafanyi kazi ndani yako, akikuadibu bila sauti ili kukusafisha. Kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu ni hasa ili kuweka wazi tabia Yake yenye haki. Ni ushuhuda gani ambao mwanadamu hatimaye huwa nao kwa Mungu? Yeye hushuhudia kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba tabia yake ni haki, ghadhabu, kuadibu, na hukumu; mwanadamu hushuhudia kwa tabia yenye haki ya Mungu. Mungu hutumia hukumu Yake kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, Amekuwa Akimpenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu—lakini ni kiasi gani kiko ndani ya upendo Wake? Kuna hukumu, uadhama, ghadhabu, na laana. Ingawa Mungu alimlaani mwanadamu katika wakati uliopita, Hakumtupa mwanadamu kabisa ndani ya shimo la kuzimu, lakini Alitumia njia hiyo kuisafisha imani ya mwanadamu; Hakumuua mwanadamu, lakini alitenda ili kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Kiini cha mwili ni kile ambacho ni cha Shetani—Mungu alikisema sahihi kabisa—lakini ukweli unaotekelezwa na Mungu haukamilishwi kufuatana na maneno Yake. Yeye hukulaani ili uweze kumpenda, na ili uweze kujua kiini cha mwili; Yeye hukuadibu ili uweze kuamshwa, kukuruhusu wewe ujue kasoro zilizo ndani yako, na kujua kutostahili kabisa kwa mwanadamu. Hivyo, laana za Mungu, hukumu Yake, na uadhama na ghadhabu Yake—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Yote ambayo Mungu anafanya leo, na tabia yenye haki ambayo Yeye huifanya kuwa wazi ndani yenu—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na huo ndio upendo wa Mungu.
kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inavyozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi. Kuzindua roho za watu hawa waliopotoka pakubwa na kudanganywa kabisa ndiyo shabaha ya aina hii ya hukumu. Mwanadamu hana roho, yaani, roho yake ilikufa kitambo na hajui kwamba kuna mbingu, hajui kwamba kuna Mungu, na bila shaka hajui kwamba yeye mwenyewe anang’ang’ana kwenye lindi kuu la kifo; anaweza kujuaje kwamba anaishi katika kuzimu hii yenye maovu hapa ulimwenguni? Angewezaje kujua kwamba maiti hii yake ambayo imeoza, kwa kupotoshwa na shetani, imeanguka Kuzimuni kwenye kifo? Angewezaje kujua kwamba kila kitu hapa ulimwenguni kimeharibiwa kitambo kiasi cha kutokarabatika na mwanadamu? Na angewezaje kujua kwamba Muumba amekuja ulimwenguni leo na anatafuta kundi la watu waliopotoka ambao Anaweza kuokoa? Hata baada ya mwanadamu kupitia kila usafishaji na hukumu inayowezekana, ufahamu wake wa chini unashtuka kwa shida na kwa kweli hauitikii chochote. Binadamu wamezoroteka kweli! Ingawa aina hii ya hukumu ni kama mvua katili ya mawe inyeshayo kutoka mbinguni, ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa binadamu. Kama isingekuwa ya kuhukumu watu hivi, kusingekuwa na matokeo yoyote na haingewezekana kabisa kuwaokoa watu dhidi ya janga la umaskini. Kama isingekuwa kwa kazi hii, ingekuwa vigumu sana kwa watu kutoka Kuzimuni kwa sababu mioyo yao imekufa kitambo na roho zao kukanyagiwa kitambo na Shetani. Kuwaokoa nyinyi ambao mmeanguka kwenye kina kirefu cha uozo kunahitaji kuwaita kwa bidii sana, kuwahukumu kwa bidii sana, na kwa kufanya hivi tu ndipo mioyo hiyo yenu migumu itakapozinduka.
kutoka katika “Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani.
kutoka katika “Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. … Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kubainisha mwanadamu na kuleta mwanadamu katika utawala mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaobaki watatakaswa na kufurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani waingiapo ulimwengu wa juu wa binadamu; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. … Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Kwa nini lazima Mungu ahukumu na kuwaadibu wanadamu wapotovu, na ni nini maana ya Mungu kuwahukumu na kuwaadibu wanadamu wapotovu? Ukweli huu ni muhimu hasa, kwani hili linahusisha ukweli kuhusu maono ya kazi ya Mungu. Ikiwa watu hawana maono katika imani yao, hawajui jinsi ya kumwamini Mungu; hata kama wanamwamini Mungu, hawawezi kuchagua njia sahihi. Basi Mungu kuwahukumu na kuwaadibu wanadamu wapotovu wanaompinga na kumsaliti utakuwa na umuhimu upi? Lazima kwanza tuwe wazi kuhusu hili—Mungu ndiye Muumba, na Ana mamlaka ya kutawala, kuhukumu, na kuadibu walioumbwa. Pia, tabia ya Mungu ni ya haki na takatifu. Hawaruhusu wale wanadamu wanaompinga na kumsaliti kuishi katika uwepo Wake, Mungu haruhusu vitu vichafu na vipotovu kuishi katika uwepo Wake. Kwa hiyo, Mungu kuwahukumu na kuwaadibu wanadamu wapotovu ni sahihi na kufaao, na kunaamuliwa na tabia ya Mungu. Sote tunajua kwamba Mungu ni mwenye haki, kwamba Mungu ni ukweli. Tayari tumeona hili kutoka kwa tabia ambayo Anafichua. Maneno yote ya Mungu ni ukweli. Mungu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote kupitia maneno Yake. Maneno ya Mungu yanaweza kuumba vitu vyote, na maneno ya Mungu pia ni ukweli unaoweza kuhukumu vitu vyote. Mungu anatenda kazi ya kuhukumu na kuadibu wanadamu wapotovu katika siku za mwisho. Wengine wanaweza kuuliza: “Je, Mungu ametenda kazi ya hukumu awali?” Kweli Amefanya kazi nyingi ya hukumu na kuadibu; ni kwamba tu watu hawajaishuhudia. Kabla ya wanadamu kuwapo, Shetani alimpinga na kumsaliti Mungu, na Mungu alimhukumu vipi Shetani? Alimfukuza Shetani chini hadi duniani, na wale malaika wote waliomfuata Shetani walirushwa duniani pamoja na Shetani. Mungu aliwatupa chini hadi duniani kutoka mbinguni—hii haikuwa hukumu dhidi ya Shetani? Ilikuwa hiyo na pia kumwadibu. Kwa hiyo, kabla ya wanadamu kuwapo, Mungu alikuwa ashamhukumu na kumwadibu Shetani. Tunaweza kuona hili kutoka katika Biblia. Kabla ya wanadamu hawa kuwapo, je, kulikuwa na wanadamu wengine au viumbe wengine waliopitia hukumu na kuadibu kwa Mungu? Tunaweza kusema na uhakika kwamba wale wote ambao wameangamizwa na Mungu walikuwa watu waliopinga na kuasi dhidi ya Mungu, na kwamba wote walipitia hukumu na kuadibu Kwake. Kwa hiyo, hukumu na kuadibu kwa Mungu kumeendelea kuwapo tangu Alipoumba mbingu na nchi na vitu vyote. Hiki ni kipengele kimoja cha kazi ya Mungu katika kutawala vitu vyote, kwa sababu tabia ya Mungu ni isiyogeuka—haiwezi kubadilika kamwe. Tunaweza kuona kwamba tangu kuwe na wanadamu wamemsaliti Mungu na kumfuata Shetani; wote wameishi chini ya laana ya Mungu. Watu wengi sana wamefariki chini ya kuadibu kwa Mungu kwa sababu ya kutenda kwao maovu wenyewe, na wengine wameangamizwa. Kumekuwa na wengi sana wanaomwamini Mungu lakini wanampinga Mungu, na hatimaye wote wameangamia. Wengine wameadhibiwa katika ulimwengu wa kiroho wakati wengine wameadibiwa wakiwa hai bado. Hii ndiyo maana wanadamu wamefupisha hili: “Wema utatuzwa na wema, na uovu kwa uovu.” Haya yote ni hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho ni kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu wapotovu. Katika kukubali kazi ya Mungu, tunakubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Wale wote wanaoasi dhidi ya Mungu na kutomtii Mungu wakati wanapitia kazi Yake wanapokea hukumu na kuadibu Kwake. Watu sanasana wanapitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, lakini wakati mwingine pia wanapokea hukumu na kuadibu kwa ukweli unaowajia na pia adhabu za Mungu. Sote tumeona hili. Wengine wanasema, “Wasioamini hawajawahi kukubali kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu, kwa hiyo wataweza kuepuka hukumu na kuadibu kwa Mungu?” Bila kujali iwapo watu wanakubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, wote watapitia hukumu na kuadibu kwa Mungu. Hakuna mtu anayeweza kuyaepuka—huu ni ukweli. Wale walio ndani ya dini hawajakubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, lakini hawawezi kuyaepuka. Hakuna mtu anayeweza kuepuka kuadibu ambako Mungu amemwamulia mwanadamu kabla—ni suala la wakati tu, kwa sababu kila mtu ana matokeo yake mwenyewe binafsi, na matokeo haya pia yanaamuliwa na Mungu. Tunaweza kuona ni aina gani ya hukumu na kuadibu ambayo kila mtu hupata kutoka kwa matokeo yake. Wengine wanakubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, wanapata utakaso kutoka kwa Mungu, wanamgeukia kabisa, na matokeo yao ni hatima nzuri—kuingia katika ufalme na kupata uzima wa milele. Mtu wa aina hiyo anapata wokovu. Wale wasiokubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, yaani, wale wasiokubali kazi ya Mungu watapitia mateso ya milele na maangamizi hatimaye. Hii ndiyo hukumu na kuadibu ambavyo vimeamuliwa kabla na Mungu na pia matokeo yao ya mwisho ambayo yameamuliwa na hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa sasa kuna viongozi wengi ndani ya jamii ya dini wanaompinga Mungu—matokeo yao ya mwisho yatakuwa yapi? Wasipotubu, hatimaye watalazimika kuzama katika maangamizi na mateso ya milele, kwani hakuna mtu anayeweza kuepuka hukumu na kuadibu kwa Mungu. Hili ni bila shaka. Tumekubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, ambalo linamaanisha tumekubali kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu. Tunakubali na kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa njia chanya, tukikuza toba ya kweli, hatimaye kutimiza maarifa ya Mungu na kubadili tabia yetu ya maisha. Kwetu, aina hii ya hukumu na kuadibu ni wokovu wetu. Kuhusu wale wanaokataa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, matokeo yao yatakuwa adhabu, na lazima hatimaye wakabiliwe na mateso ya milele na maangamizi. Haya ndiyo matokeo ya kuepuka hukumu na kuadibu kwa Mungu.
kutoka katika “Mungu Kutenda Kazi kwa Njia Tofauti ili Kuwaokoa Wanadamu Kuna Maana Nzuri Sana” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni