Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumhusu-Petro. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumhusu-Petro. Onyesha machapisho yote

2/23/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu. Nimetembea ulimwenguni kwa miguu Yangu, Nikinyoosha macho Yangu juu ya anga yake nzima, na Nimetembea miongoni mwa wanadamu wote, Nikionja ladha tamu, ya asidi, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu, lakini mwanadamu hakuwahi kweli kunitambua, wala hakuniona Nikitembea ng’ambo.