
Mwenyezi Mungu alisema,Watu wengi wana hali hizi ambazo tumejadiliana hapo awali, hata ingawa si wazi kama hapo awali. Hii ni kwa sababu watu hawakuwa na ufahamu wowote wa ukweli wakati huo, na hawakuelewa chochote. Siku hizi, unasikiliza zaidi, na kwa kiwango cha chini kabisa, nyote mnaelewa baadhi ya mafundisho. Hata hivyo, una hali fulani zilizojikita ndani ambazo hazijafunuliwa. Una uwezo wa kuuona upotovu kwa wazi ambao mara nyingi hufunuliwa na kuwa na ufahamu mara tu unapofunuliwa; unajua asili ya malengo yako yaliyofunuliwa, maneno, na vitendo. Lakini sasa hivi, hujui mambo yaliyo ndani yako, mambo yaliyofichwa zaidi na vitu vinavyowasilisha asili ya kibinadamu.