Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mabadiliko-Katika-Tabia. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mabadiliko-Katika-Tabia. Onyesha machapisho yote

4/01/2018

Sura ya 39. Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia

Mwenyezi Mungu alisema, Ni nini mnafahamu kuhusu mabadiliko katika tabia? Asili ya mabadiliko katika tabia na mabadiliko katika mwenendo ni tofauti, na mabadiliko katika matendo pia ni tofauti—yote ni tofauti kwa asili. Watu wengi wanaweka mkazo maalum kwa tabia yao katika imani yao kwa Mungu, matokeo yakiwa mabadiliko yanayofanyika katika mienendo yao. Baada ya kuamini katika Mungu, wanakoma kubishana na wengine, wanakoma kupigana na watu na kuwatukana, wanakoma kuvuta sigara na kunywa, hawaibi mali ya uma—hata iwe msumari ama kipande cha mbao pekee—na hata wanaenda kiasi cha kutoipeleka kotini wanapopata hasara ama wamekosewa.