Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-akipenda. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-akipenda. Onyesha machapisho yote

10/08/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 30


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 30

Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri. Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya. Msiwe wenye shaka tena na msiogope kuwa na uhakika!

10/07/2019

Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians πŸŽ΅πŸŽ΅πŸ‘πŸ‘




Wimbo wa Injili | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" | The Great Mission of Christians


I

Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, ni jukumu letu
kutoa akili zetu na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

8/31/2019

Neno la Mungu | Sura ya 115


Neno la Mungu | Sura ya 115

Moyo Wangu utakufurahia mno, Nitacheza kwa furaha juu yako, na Nitakupa baraka zisizo na mwisho, kwa kuwa kabla ya uumbaji, ulitoka Kwangu, na leo lazima urejee upande Wangu, kwa kuwa wewe si wa dunia ama ulimwengu bali, badala yake, wewe ni Wangu. Nitakupenda milele, Nitakubariki milele na Nitakulinda milele. Ni wale tu ambao wametoka Kwangu wanaoyajua mapenzi Yangu, na ni wao tu wataudhukuru mzigo Wangu na kufanya kile ambacho Ninataka kukifanya.

8/17/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85


Mimi huwatumia watu tofauti kufanikisha mapenzi Yangu. Laana Zangu hufanikishwa kwa wale Ninaowaadibu na baraka Zangu kufanikishwa kwa wale ambao Ninawapenda. Ambao sasa hukutana na baraka Zangu na ambao hupitia laana Zangu kwa neno Langu moja na tamko Langu. Unajua kuwa yeyote Ninayekuwa mzuri kwake sasa hakika atakutana na baraka Zangu wakati wote (kumaanisha kuwa wale wanaokuja kunijua polepole na wanaokuwa na uhakika zaidi kunihusu polepole, wale walio na mwanga mpya na ufunuo na walio na uwezo wa kwenda mwendo sawa na wa kazi Yangu).

8/16/2019

Kazi na Kuingia (3)

Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; maarifa ya juujuu ya utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni.

8/08/2019

Neno la Mungu | Sura ya 57

Je, umechunguza kila fikira na mawazo yako, na kila tendo lako? Uko wazi kuhusu gani kati ya haya yanalingana na mapenzi Yangu na gani hayalingani? Huna uwezo wa kutambua haya! Mbona hujaja mbele Yangu? Je, ni kwa sababu Sitakuambia, au ni kwa ajili ya sababu nyingine? Unapaswa kujua hili! Kujua kwamba wale walio wazembe hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu kabisa au kupokea mwangaza na ufunuo mkuu.

8/05/2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 58

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 58

Ukiielewa nia Yangu, utaweza kuufikiria mzigo Wangu na unaweza kupata mwanga na ufunuo, na kupata ufunguliwaji na uhuru, kuuridhisha moyo Wangu, kuyaruhusu mapenzi Yangu kwa ajili yako kutekelezwa, kuwaletea watakatifu wote ujenzi wa maadili, na kuufanya ufalme Wangu duniani kuwa imara na thabiti. Jambo la muhimu sasa ni kuelewa nia Yangu, hii ni njia mnayopaswa kuingia katika na hata zaidi ni wajibu wa kutimizwa na kila mtu.