Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ujenzi-wa-kanisa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ujenzi-wa-kanisa. Onyesha machapisho yote

8/11/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 41

Kuhusu shida zinazoibuka kanisani, usiwe na mashaka mengi. Kanisa linapojengwa haiwezekani kuepuka makosa, lakini usiwe na wasiwasi unapokabiliwa na shida hizo; kuwa mtulivu na makini. Sijawaambia hivyo? Omba Kwangu mara nyingi, na Nitakuonyesha kwa wazi nia Zangu. Kanisa ni moyo Wangu na ni lengo Langu la msingi, Nawezaje kutolipenda? Usiogope, mambo kama haya yanapotendeka kanisani, yote yanaruhusiwa na Mimi. Simama na uwe sauti Yangu.