Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wajibu-wa-Mwanadamu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Wajibu-wa-Mwanadamu. Onyesha machapisho yote

11/29/2017

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde mnapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia wako utakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kazi yako. Kwa njia hiyo, tajriba na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua ukweli wote, hutapoteza kitu maishani na hutapotea.Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo. Huwezi kugeuka baada ya siku chache tu na hutaweza kuipata njia mwafaka hata katika majuma machache.