10/24/2017

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu
Kufahamu kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu. Mungu anaposemekana kuwa anajumuisha yote na tele zaidi, ni nini kinachomaanishwa na kujumuisha yote? Na nini kinachomaanishwa na tele? Iwapo huelewi haya, basi huwezi kuchukuliwa kuwa muumini wa Mungu.

10/22/2017

Umeme wa Mashariki | 5. Ole Wao Wale Wamsulubishae Mungu Mara Nyingine Tena

Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili katika nchi ya China kufanya kazi, na Ameonyesha mamilioni ya maneno, Akishinda na kuokoa kundi la watu kwa neno Lake na kuikaribisha enzi mpya ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Leo, kuenea kwa kazi ya Mungu katika siku za mwisho kumefikia kilele chake katika China Bara. Wengi wa watu katika Kanisa Katoliki na madhehebu yote ya Kikristo na makundi ya kidini ambayo yanafuatilia ukweli wamerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Mungu mwenye mwili Amekamilisha kazi ya "ujio wa siri wa Mwana wa Adamu" Aliyetabiriwa katika Biblia, na hivi karibuni Ataonekana kwa umma katika kila taifa na sehemu ulimwenguni. Watu wote katika kila taifa na sehemu walio na kiu cha kuonekana kwa Mungu watatarajia kuonekana kwa Mungu hadharani.

Umeme wa Mashariki | Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote
Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Uyahudi, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kwa kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi tu, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Wanaisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaokomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Wanaisraeli pekee, na si Mungu wa Wayahudi pekee;

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia
Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo utamjua Yesu Atakaporejea? Je, mtaelewa kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. Nyote mmetazamia wakati wa kurudi, na uaminifu wenu ni wa kusifika, na imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: wingu hili jeupe linaashiria nini?

Wimbo wa Injili | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Best Swahili Christian Worship Song

Kama Nisingeokolewa na Mungu


Kama mimi nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,

nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.

Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,

kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.

10/21/2017

Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme

Umeme wa Masharik,Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme
1. Mwanadamu hapasi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.
2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupasi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.
3. Pesa, vitu vya dunia, na mali yote ambayo yako katika kaya ya Mungu ni sadaka ambazo zinapasa kutolewa na binadamu. Sadaka hizi hazifai kufurahiwa na binadamu yeyote ila kasisi na Mungu Mwenyewe, kwani sadaka zinazotolewa na binadamu ni za kufurahiwa na Mungu, Mungu pekee ndiye Anayeweza kumgawia kasisi sadaka hizi, na hakuna mwengine yeyote aliyehitimu wala kuwa na haki ya kufurahia sehemu yoyote ya sadaka hizi.

10/20/2017

Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo
Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya ubinadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova hakuwa amepanga bado awamu ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; awamu ya pili ya kazi, ile ya neema; au awamu ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kuanzia hapa Angeweza kushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima ya usimamizi ya miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, Hakuwa ameandika mpango kama huo kama Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Ubinadamu kabla ya kuumba ulimwengu. Katika kazi ya Mungu, Anaeleza moja kwa moja Yeye ni nani;

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana "Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu"



Ha … nyimbo ni nyingi na ngoma ni za madaha;

ulimwengu na miisho ya dunia zinakuwa bahari inayosisimka.

Ha … mbingu ni mpya na dunia ni mpya.

Eneo kubwa la ulimwengu limejaa kusifu; tunapiga ukelele na kuruka kwa shangwe.

Milima yajiunga na milima na maji mengi kujiunga na maji mengi, ndugu wote wa kiume na kike ni wandani.

Twamsifu Mungu bila kukoma. Viumbe wampenda Mungu,

wakija, mbele ya kiti chake cha enzi kwa furaha kuabudu pamoja.

Umeme wa MasharikiKazi | Kazi Katika Enzi ya Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa
Umeme wa MasharikiKazi | Katika Enzi ya Sheria
Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Alichagua watu Alioona kwamba walifaa ili kuwawekea mipaka upana wa kazi Yake. Israeli ndipo mahali ambapo Mungu Aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka kwenye vumbi la mahali hapo, Yehova Alimwumba mwanadamu; ndio msingi wa kazi Yake ya hapo ulimwenguni. Waisraeli, ambao ni kizazi cha Nuhu na Adamu, ndio waliokuwa msingi wa kazi ya Yehova ulimwenguni.

10/19/2017

Ngurumo Saba Zatoa Sauti- Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili

Ngurumo Saba Zatoa Sauti- Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mimi hueneza kazi Yangu katika mataifa. Katika ulimwengu mzima unang’aa utukufu Wangu; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi Ninayosambaza. Kuanzia sasa, Ninaingia enzi mpya na kuleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Ninaporudi katika "nchi Yangu," Ninaanza sehemu nyingine ya kazi katika mpango Wangu wa awali ili mwanadamu aje kujua zaidi kunihusu. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, hivyo Mimi Nasafiri huku na kule kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Ni enzi mpya, licha ya yote, na Ninaleta kazi mpya ili niwachukue watu wapya zaidi katika enzi mpya na kuwatupa kando zaidi ya wale Nitakaowaondoa. Katika taifa la joka kubwa jekundu, Ninatekeleza hatua ya kazi isiyoweza kueleweka na mwanadamu na kuwafanya kutingika katika upepo, ambapo baadaye wengi kwa kimya watabebwa na upepo unaovuma.

10/18/2017

Umeme wa Mashariki | Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Kiini cha imani ya watu wengi katika Mungu ni imani za kidini: Hawana uwezo wa kumpenda Mungu, na wanaweza kumfuata Mungu tu kama roboti, bila kuweza kumtamani Mungu, ama kumwabudu. Wanamfuata tu kimyakimya. Watu wengi wanamwamini Mungu, lakini wapo wachache sana ambao humpenda Mungu; wanamheshimu tu Mungu kwa sababu wanaogopa majanga, au hata wanamstahi Mungu kwa sababu ni Mwenye nguvu na aliye juu—lakini katika kumheshimu na kuvutiwa kwao hakuna upendo au kutamani kwa kweli. Katika matukio wanayoyapitia wanataka chembe za ukweli, au hata miujiza fulani isiyokuwa na maana. Watu wengi hufuata tu, wanapitia njia mbaya ili tu kupokea baraka; hawataki ukweli, wala kumtii Mungu kwa kweli ili kupokea baraka za Mungu. Maisha ya imani kwa Mungu ya watu wote hayana maana, hayana thamani, na katika imani yao mna fikira na kazi zao za kibinafsi; hawaamini katika Mungu ili kumpenda Mungu, lakini kwa ajili ya kutaka kubarikiwa. Watu wengi hutenda jinsi wapendavyo, hufanya wanachokitaka, na kutojali anachopenda Mungu, au kama wanachokifanya ni kulingana na mapenzi ya Mungu.

10/17/2017

Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli

kanisa,ukombozi,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Bwana asifiwe
Umeme wa Mashariki | Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli
Hapo awali sana, umuhimu wa kuwa na maisha sahihi ya kanisa ulitajwa katika mahubiri. Kwa hivyo ni kwa nini maisha ya kanisa hayajaboreka bado, na bado ni kile kitu kimoja tu cha zamani? Mbona hakuna njia mpya na tofauti kabisa ya maisha? Je, inaweza kuwa sahihi kwa mtu wa miaka ya tisini kuishi kama mfalme wa enzi iliyopita? Ingawa chakula na vinywaji vinaweza kuwa vyakula vitamu vilivyoonjwa mara chache katika enzi zilizopita, hapajakuwa na mabadiliko makubwa katika hali kanisani. Imekuwa kama kuweka divai ya kale katika kiriba kipya. Je, kuna haja gani basi ya Mungu kusema sana? Makanisa katika maeneo mengi hayajabadilika kabisa. Mimi nimeliona kwa macho Yangu na ni wazi katika moyo Wangu; Hata kama sijapata uzoefu wa maisha ya kanisa Mimi Mwenyewe, Nazijua hali za mikusanyiko ya kanisa kama mgongo wa mkono Wangu. Hawajafanya maendeleo mengi. Inarejelea msemo—ni kama kutia divai ya kale katika kiriba kipya. Hakuna kilichobadilika, siyo hata kidogo! Wakati mtu anapowachunga wao huwaka kama moto, lakini wakati hakuna mtu hapo kuwafadhili, wao ni kama pande kubwa la barafu.