Ⅰ
Uliniinua kutoka kwa vumbi hadi ndani ya kumbatio Lako.
Uliamsha moyo wangu kutoka kwa usingizi wa usiku mrefu wa giza.
Nikitazama ndani ya ukungu wangu, naona uso Wako unaotabasamu.
Inauita moyo wangu na upendo wangu.
Sikufikiria kamwe ningeuona uso Wako.
Baraka iliyoje imenipata bila kutarajia.





