Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nane
Kotekote katika uzoefu wa wanadamu umbo Langu halijakuwepo, wala kuwepo kwa uongozi wa maneno Yangu, na kwa hiyo Nimemuepuka mwanadamu kwa umbali kila mara na kisha Nikaondoka kwake. Nadharau uasi wa wanadamu. Sijui kwa nini. Inaonekana Nimemchukia mwanadamu tangu mwanzo, na bado Nahisi huruma kubwa kwake. Na kwa hiyo mwanadamu ananiangalia na mioyo miwili, kwani Nampenda mwanadamu, na pia Namchukia mwanadamu.