7/13/2018

Ambua Barakoa, na Uanze Maisha Upya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda

Chen Dan    Mkoa wa Hunan
Mwishoni mwa mwaka jana, kwa sababu sikuweza kuzindua kazi ya injili katika eneo langu, familia ya Mungu ilimhamisha ndugu mmoja wa kiume kutoka eneo jingine ili kuchukua kazi yangu. Kabla ya haya sikuwa nimearifiwa, bali nilisikia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa dada mmoja niliyekuwa mbia naye. Nilifadhaika sana. Nilishuku kwamba mtu aliyekuwa madarakani hakuwa ameniarifu kwa kuhofia kwamba singekubali kuiacha nafasi yangu na ningeshindana.

7/12/2018

Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

3. Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Njoo Mbele Ya Mungu Mara kwa Mara

Chukua fursa unapokuwa na wakati, keti kimya mbele ya Mungu.
Soma neno Lake, jua ukweli Wake, rekebisha makosa na dhambi ndani yako.
Majaribu huja, yakabili; ijue nia ya Mungu na utakuwa na nguvu.
Mwambie ni vitu gani unavyokosa, shiriki ukweli Wake kila mara.
Roho yako ina furaha unapomwabudu Yeye.
Njoo mara kwa mara mbele ya Mungu, usipinge tena.
Kujali kwako mwili, kunamuumiza Yeye sana.

7/11/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nane


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nane 


Kotekote katika uzoefu wa wanadamu umbo Langu halijakuwepo, wala kuwepo kwa uongozi wa maneno Yangu, na kwa hiyo Nimemuepuka mwanadamu kwa umbali kila mara na kisha Nikaondoka kwake. Nadharau uasi wa wanadamu. Sijui kwa nini. Inaonekana Nimemchukia mwanadamu tangu mwanzo, na bado Nahisi huruma kubwa kwake. Na kwa hiyo mwanadamu ananiangalia na mioyo miwili, kwani Nampenda mwanadamu, na pia Namchukia mwanadamu.

2018 Best African Worship Song "Miaka Elfu Mbili ya Kungoja" | Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu



Kwamba Mungu amekuwa mwili 
hutikisa ulimwengu wa kidini,
inavuruga utaratibu wa kidini,
na inakoroga roho za wale 
wanaongoja kuonekana kwa Mungu.
Nani asiyeshangazwa na haya?
Ni nani asiye na hamu ya kumwona Mungu?
Mungu ameishi kwa miaka mingi kati ya binadamu, 
lakini binadamu hafahamu.

7/10/2018

Ninaona Ukweli wa Upotovu wa Watu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Li Heng    Jiji la Suqian, Mkoa wa Jiangsu
Miongoni mwa maneno ambayo kwayo Mungu humfichua mwanadamu nilipata kifungu hiki, “Ilisemwa hapo awali kwamba watu hawa ni uzao wa joka kubwa jekundu. Kwa kweli, ili kuwa wazi, wao ni mfano halisi wa joka kubwa jekundu” (“Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Sita” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilidhani hili halikunihusu. Ilionekana kwangu kwamba Mungu alifichua maneno haya kwa wale wanaomiliki mamlaka, kwa sababu wao ni joka kubwa jekundu lililobadilishwa;

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

7/09/2018

Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

1. Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Yixin    Jiji la Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei
Kabla, ningewasikia mara kwa mara ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema, "Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya matokeo mazuri; ndiyo yote wanayohitaji watu." Nilikubali hili na kukubaliana nalo, lakini sikuwa na ufahamu wowote kupitia uzoefu wangu mwenyewe. Baadaye nilipata ufahamu kiasi kwa njia ya mazingira ambayo Mungu aliniumbia.

7/08/2018

"Mji Utaangushwa" (5) - Mji mkuu wa dini wa Babeli Umekusudiwa Kuangamia Chini ya Ghadhabu ya Mungu!


Ulimwengu wa dini humkaidi na kumlaani Mwenyezi Mungu, ukitenda matendo maovu yasiyohesabika, na wamekuwa kambi ya Shetani ambayo humpinga Mungu vikali. Mji mkuu wa dini wa Babeli umekusudiwa kuangamia chini ya ghadhabu ya Mungu! Ufunuo unatabiri, "Ole, ole ule mji mkuu Babeli, ule mji ulio na uwezo! kwani hukumu yako imekuja katika saa moja" (Ufunuo 18:10). Mwenyezi Mungu asema, "Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu.

Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

2. Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake?

7/07/2018

Kuukaribisha Uso Wako Unaotabasamu Unapoonekana Mbele Yangu

Uliniinua kutoka kwa vumbi hadi ndani ya kumbatio Lako.
Uliamsha moyo wangu kutoka kwa usingizi wa usiku mrefu wa giza.
Nikitazama ndani ya ukungu wangu, naona uso Wako unaotabasamu.
Inauita moyo wangu na upendo wangu.
Sikufikiria kamwe ningeuona uso Wako.
Baraka iliyoje imenipata bila kutarajia.

Nilipitia Wokovu wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wakristo
Cheng Hao    Mji wa Yongzhou, Mkoa wa Hunan
Kwa neema ya Mungu, mimi na mke wangu tulipandishwa vyeo hadi kwa timu ya injili ya pili ili kutimiza wajibu wetu. Muda mfupi uliopita, mke wangu alipandishwa cheo kuwa mkurugenzi wa timu, huku mimi, kutokana na kiburi changu mwenyewe na utukutu wangu, nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kupelekwa nyumbani kutafakari juu ya matendo yangu.