12/31/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 80

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 80

Kila kitu kinahitaji mawasiliano halisi na Mimi ili kupata nuru na kuangazwa; aidha, ni kwa njia hii tu ndio roho inaweza kuwa na amani. La sivyo, haitakuwa na amani. Sasa ugonjwa mbaya zaidi kati yenu ni kutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida kutoka kwa uungu Wangu kamili; aidha, wengi wenu huweka mkazo kwa ubinadamu Wangu wa kawaida, kama kwamba kamwe hawajui kuwa Mimi nina uungu kamili pia. Hii inanikufuru Mimi!

12/30/2018

Swahili Gospel Movie Clip (3) - Ili Kuchunguza Kurudi kwa Bwana Tunapaswa Kusikiliza Sauti ya Mungu


Kimsingi unabii wote uliotajwa katika Biblia kuhusiana na kurudi kwa Bwana tayari umetokea. Watu wengi wamehisi kwamba Bwana tayari amerudi, hivyo, tunapaswa kuchunguza vipi ili kuhakikisha kuhusu suala la ikiwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi au la? Tunapaswa kufanya uamuzi wetu kulingana na unabii wa Biblia au tunapaswa kuchunguza moja kwa moja neno na kazi ya Mwenyezi Mungu?

12/29/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 45

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 45

Mnawahukumu ndugu zenu hadharani kana kwamba si kitu. Hakika hamjui mema na maovu; hamna aibu! Je, hii si tabia mbaya ya kifidhuli, ya kutojali? Kila mmoja wenu amechanganyikiwa na ni mwenye moyo mzito; mnabeba mizigo mingi na hakuna sehemu Yangu ndani yako. Watu vipofu! Ninyi ni wakatili namna gani—hili litakoma lini?

12/28/2018

Gospel Video "Rekodi ya Kazi ya Mungu ya Kuumba Ulimwengu na Kuwaongoza na Kuwakomboa Wanadamu"



        Je, unataka kujua jinsi Mungu alivyouumba ulimwengu? Je, unataka kujua jinsi Mungu amewaongoza wanadamu hatua kwa hatua hadi leo? Sehemu hii ya ajabu kutoka kwa filamu ya Kikristo, "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu Ya Kila Kitu", imerekodi kazi ya Mungu ya kuumba ulimwengu na kuwaongoza na kuwakomboa wanadamu. Itakufichulia majibu haya.

Yaliyopendekezwa : Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

12/27/2018

Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo;

12/26/2018

Filamu za Kikristo | "Mazungumzo" | Christian Testimony of Overcoming Satan


Jiang Xinyi na Wakristo wengine walikamatwa na serikali ya CCP; wao huwatesa Wakristo kwa ukatili ili kutwaa fedha za kanisa na kuwakamata viongozi zaidi wa kanisa. Kisha, ili kuwalazimisha kuikataa imani yao, wao huzindua kampenii moja baada ya nyingine ya kuwatia kasumba, lakini kwa uongozi wa maneno ya Mungu, wao huweza kuyashinda mateso na udanganyifu wote wa Shetani. Wao hutegemea ukweli kushiriki katika vita vikali na serikali ya CCP …

Yaliyopendekezwa: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

12/25/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini na Sita

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini na Sita

Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wameondolewa kabisa kutoka duniani.

12/24/2018

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Upendo Safi Bila Dosari


I
Upendo ni hisia safi, safi bila dosari.
Tumia moyo, tumia moyo,
kupenda, kuhisi, kutunza.
Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga.
Tumia moyo, Tumia moyo,
kupenda, kuhisi, kutunza.
Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki,
hutazamii kupata kitu, cha malipo.
Ukipenda utajitolea, ukubali taabu,
kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.

12/23/2018

Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)


Mwenyezi Mungu anasema, "Punde tu kazi ya ushindi imekwisha kamilika, mwanadamu ataletwa katika dunia nzuri. Haya maisha, bila shaka, bado yatakuwa duniani, lakini yatakuwa tofauti kabisa na jinsi maisha ya mwanadamu yalivyo leo. Ni maisha ambayo mwanadamu atakuwa nayo baada ya wanadamu kwa ujumla kushindwa, itakuwa mwanzo mpya kwa mwanadamu hapa duniani, na kwa wanadamu kuwa na maisha kama hii ni ushahidi kwamba wanadamu wameingia katika milki jipya na nzuri.

12/22/2018

Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

1. Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake.

12/21/2018

Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?


Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alitabiri, "Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki" (Mathayo 25:6). "Tazama, nasimama mlangoni, na kubisha: mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja na yeye, na yeye pamoja na mimi" (Ufunuo 3:20). Kwa miaka elfu mbili iliyopita, waumini katika Bwana wamekuwa makini na wakingoja Bwana abishe mlango, kwa hivyo, Atabishaje mlango wa binadamu 2Atakaporudi?

12/20/2018

Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele


I
Maneno ya Mungu ni ukweli, yasiobadilika milele.
Mungu ndiye mtoaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Thamani na maana ya maneno Yake yanabainishwa na kiini chao,
sio kama mwanadamu anayakubali ama kuyatambua.
Hata kama hakuna mwanadamu ulimwenguni anayepokea maneno Yake,
thamani yao na usaidizi kwa mwanadamu hayapimiki.

12/19/2018

Swahili Christian Skit | "Baba Yangu, Mchungaji" | A Debate on the Bible in a Family


Swahili Christian Skit | "Baba Yangu, Mchungaji" | A Debate on the Bible in a Family

Chi Shou, mchungaji wa dini ambaye amekuwa muumini wa Bwana kwa miaka arubaini, daima ameshikilia mitazamo kwamba "maneno na kazi yote ya Bwana yako ndani ya Biblia," na kwamba "imani katika Bwana haiwezi kuacha Biblia, na kuiamini Biblia humaanisha kumwamini Bwana." Inapojulikana kwamba binti yake ameikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, anafanya mpango na mke wake kumkomesha. Katika siku hii, binti yao anarudi nyumbani kushuhudia injili ya kurudi kwa Bwana, na mjadala mkali, mcheshi, ilhali mzito wa familia unatokea ...