12/22/2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Uzoefu

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Biblia
kukamilishwa na Mungu,ndugu na dada

                                      Umeme wa Mashariki | Kuhusu Uzoefu

Mwenyezi Mungu alisema, Katika uzoefu mzima wa Petro, alikuwa amevumilia mamia ya majaribio. Ijapokuwa watu sasa wanajua neno “jaribio” hawaelewi kabisa maana yake halisi au hali. Mungu huichovya uamuzi wa mwanadamu, husafisha ujasiri wake, na hufanya kila sehemu yake kuwa kamili, kufikia hili hasa kwa njia ya majaribio. Majaribio pia ni kazi ya siri ya Roho Mtakatifu. Inaonekana kwamba Mungu amemtelekeza mwanadamu, na hivyo mwanadamu, kama si makini, atayaona kama majaribu ya Shetani. Kwa kweli, majaribu mengi yanaweza kuchukuliwa kama majaribu, na hii ndiyo kanuni na amri ya kazi ya Mungu. Ikiwa mtu huishi kwa kweli mbele ya Mungu, atayaona kama majaribio ya Mungu na asiyaache yapite. Ikiwa mtu anasema kwamba kwa sababu Mungu yu pamoja naye Shetani hakika hawezi kumkaribia, hii siyo sahihi kabisa. Inawezaje kuelezwa kwamba Yesu alikabiliwa na majaribu baada ya Yeye kufunga jangwani kwa siku arobaini? Kwa hivyo ikiwa mtu ameyaweka sawa maoni yake juu ya kumwamini Mungu, atayaona mambo mengi kwa uwazi zaidi na hatakuwa na ufahamu wa kuegemea upande mmoja na wa uongo. Ikiwa mtu amefanya uamuzi wa kweli kukamilishwa na Mungu, anahitaji kukabiliana na masuala ambayo yeye hukabiliwa nayo kutoka katika pembe nyingi tofauti, wala asiegemee upande wa kushoto wala wa kulia. Ikiwa huna ufahamu wa kazi ya Mungu, hutajua jinsi ya kushirikiana na Mungu. Ikiwa hujui kanuni za kazi ya Mungu na haujui jinsi Shetani anavyofanya kazi kwa mwanadamu, hutakuwa na njia ya kutenda. Ufuatiliaji wa bidii tu hautakuwezesha kupata matokeo ambayo Mungu anataka. Njia kama hiyo ya uzoefu ni sawa na ile ya Lawrence, haitofautishi na kulenga tu uzoefu, bila kujua kabisa kazi ya Shetani ni nini, ya kazi ya Roho Mtakatifu ni nini, jinsi mtu alivyo bila uwepo wa Mungu, na ni watu wa aina gani ndio Mungu anataka kuwakamilisha. Jinsi ya kutenda kwa watu tofauti, jinsi ya kufahamu mapenzi ya Mungu ya sasa, jinsi ya kujua tabia ya Mungu, kwa watu wapi, mazingira gani, na umri gani, huruma ya Mungu, uadhama Wake na haki huelekezwa—hawezi kutenganisha haya. Ikiwa mtu hana maono mengi kama msingi wake, msingi wa uzoefu wake, basi maisha hayawezekani, seuze uzoefu; yeye kwa upumbavu anaendelea kutii kila kitu, akivumilia kila kitu. Watu wote kama hao ni vigumu sana kufanywa wakamilifu. Inaweza kusemwa kuwa bila ya maono yoyote yaliyoguswa hapo juu ni ushahidi mzuri unakuwa mpumbavu, sawa na nguzo ya chumvi, daima imesimama katika Israeli. Watu kama hawa ni bure, wao ni wasio na umuhimu wowote! Watu wengine hutii kwa upofu, daima wanajijua wenyewe na hutumia njia zao za kutenda wakati wa kushughulikia masuala mapya, au kutumia "hekima" kushughulikia mambo madogo madogo ambayo hayastahili kutajwa, hao ni watu ambao hawana utambuzi, kana kwamba kwa asili walikuwa wamekubali bila malalamiko shida, daima kuwa vile vile, kamwe hawabadiliki; huyu ni mpumbavu bila ufahamu wowote. Halinganishi vipimo kwa mazingira au kwa watu tofauti. Watu kama hawa hawana uzoefu. Ninaona kwamba watu wengine wanajijua kwa kiasi fulani kwamba wakati wanakabiliwa na wale ambao wana kazi ya roho mbaya wao hata huinamisha vichwa vyao na kukubali kuwa na hatia, wasithubutu kusimama na kuwahukumu. Wakati wanakabiliwa na kazi dhahiri ya Roho Mtakatifu, hawathubutu kutii, pia, kuamini kwamba roho wabaya pia wako mikononi mwa Mungu, na hawajaribu hata kidogo kuinuka na kupinga. Hawa ni watu ambao hawana heshima ya Mungu, na kwa hakika hawawezi kubeba mizigo mizito kwa ajili ya Mungu. Watu waliochanganyikiwa kama hawa hawatofautishi. Njia hii ya uzoefu kwa hivyo inapaswa kuachwa kwa sababu haiwezi kutetewa machoni pa Mungu.
Mungu kwa kweli Anafanya kazi nyingi kwa watu, wakati mwingine Akiwajaribu, wakati mwingine Akifanya mazingira ya kuwachovya, na wakati mwingine kuzungumza maneno ili kuwaongoza na kurekebisha upungufu wao. Wakati mwingine Roho Mtakatifu huwaongoza watu kwenye mazingira yaliyoandaliwa na Mungu kwao ili watambue bila kujua mambo mengi ambayo hawana. Kupitia katika kile ambacho watu husema na kufanya, njia ambayo watu huwatendea wengine na kushughulikia vitu, bila ya wao kujua, Roho Mtakatifu anawapa nuru kuelewa mambo mengi ambayo hayakueleweka hapo awali, Akiruhusu kuelewa mambo mengi au watu kwa kina zaidi, Akiwaruhusu wao kung’amua mambo mengi ambayo walikuwa awali hawajui. Ikiwa unawasiliana na ulimwengu, hatua kwa hatua unakuwa na ubaguzi zaidi juu ya mambo ya ulimwengu, na unapokaribia kifo unaweza kufikiri: "Kweli ni vigumu kuwa mtu." Ukipata uzoefu kwa muda fulani mbele ya Mungu, na kufahamu kazi ya Mungu na tabia Yake, utapata utambuzi mkubwa bila kujua, na kimo chako kitakua polepole. Utaelewa mambo mengi ya kiroho vizuri zaidi, na utakuwa wazi zaidi kuhusu kazi ya Mungu hasa. Utaweza kukubali maneno ya Mungu, kazi ya Mungu, kila kitendo cha Mungu, tabia ya Mungu, na kile Mungu anacho na alicho kama maisha yako mwenyewe. Ikiwa yote unayofanya ni kutembea ulimwenguni, mabawa yako yatakuwa magumu na magumu zaidi, na kipengele chako ambacho kinampinga Mungu kitakuwa kikubwa zaidi. Itakuwa vigumu kwa Mungu kukutumia. Kwa sababu kuna mengi sana ya hicho kipengele cha "kama ninavyoona" ndani yako, ni vigumu kwa Mungu kukutumia. Kadri ulivyo mbele ya Mungu, ndivyo utakavyoupata uzoefu zaidi. Ikiwa bado uko ulimwenguni kama mnyama, kinywa chako kikikiri kuwa na imani kwa Mungu lakini moyo wako ukiwa mahali pengine, na kujifunza falsafa za kidunia za maisha, je, hili halitakuwa kufuta kazi yote ya awali? Kwa hivyo, kadri watu walivyo katika uwepo wa Mungu ndivyo ilivyo rahisi zaidi kufanywa wakamilifu na Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi Yake. Ikiwa huelewi hili, haitawezekana kwako kuingia katika njia sahihi, na kukamilishwa na Mungu hakutakuwepo. Hutaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho, na utakuwa kama mlemavu, na kazi yako mwenyewe ya bidii tu na bila kazi yoyote ya Mungu. Je, hiki hakitakuwa kitu kibaya na uzoefu wako? Si lazima uombe ili uwe mbele ya Mungu. Wakati mwingine ni katika kutafakari kwako kwa Mungu au kutafakari kazi Yake, wakati mwingine katika kushughulikia jambo fulani, na wakati mwingine kwa kufichuliwa kwako katika tukio, ndiyo unakuja mbele ya Mungu. Watu wengi husema, je, mimi siko mbele ya Mungu, kwani mara nyingi ninaomba? Watu wengi huomba bila kukoma "katika uwepo wa Mungu." Sala zinaweza kuwa daima kwenye midomo yao, lakini hawaishi kwa kweli mbele ya Mungu. Mtu wa aina hii anaweza tu kudumisha hali yake ya kuwepo mbele ya Mungu kwa njia hii. Hawezi kuwasiliana na Mungu kwa moyo wake daima, au kutumia utaratibu wa uzoefu kuja mbele ya Mungu, iwe kupitia kufikiri, kutafakari kwa kimya ndani ya moyo wake, au kuwasiliana na Mungu wa moyo wake kwa moyo wake mwenyewe kwa kuzingatia mzigo wa Mungu. Anatoa sala hadi mbinguni kwa mdomo wake. Watu wengi sana hawana Mungu mioyoni mwao, na wana Mungu wakati wanapomkaribia Mungu pekee, lakini mara nyingi hawana Mungu hata kidogo. Je, Haya si maonyesho ya kutokuwa na Mungu katika moyo wa mtu? Ikiwa kweli ana Mungu, je, angeweza kufanya mambo ambayo wanyang’anyi au wanyama hufanya? Ikiwa mtu humcha Mungu kwa kweli, ataleta moyo wake wa kweli kuwasiliana na Mungu, na fikira zake na mawazo yake yatamilikiwa na maneno ya Mungu daima. Kutakuwa na uwezekano mdogo kwake kufanya makosa katika mambo ya nje ambayo watu wana uwezo wa kufanikisha, bila kufanya chochote kinachompinga Mungu kwa wazi. Hiki tu ndicho kiwango cha kuwa muumini.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
 Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni