kukamilishwa na Mungu,ndugu na dada |
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Uzoefu
Mwenyezi Mungu alisema, Katika uzoefu mzima wa Petro, alikuwa amevumilia mamia ya majaribio. Ijapokuwa watu sasa wanajua neno “jaribio” hawaelewi kabisa maana yake halisi au hali. Mungu huichovya uamuzi wa mwanadamu, husafisha ujasiri wake, na hufanya kila sehemu yake kuwa kamili, kufikia hili hasa kwa njia ya majaribio. Majaribio pia ni kazi ya siri ya Roho Mtakatifu. Inaonekana kwamba Mungu amemtelekeza mwanadamu, na hivyo mwanadamu, kama si makini, atayaona kama majaribu ya Shetani. Kwa kweli, majaribu mengi yanaweza kuchukuliwa kama majaribu, na hii ndiyo kanuni na amri ya kazi ya Mungu. Ikiwa mtu huishi kwa kweli mbele ya Mungu, atayaona kama majaribio ya Mungu na asiyaache yapite.