3/01/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

(I) Mhutasari juu ya Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Na ya tatu? (Utakatifu wa Mungu.) Tumejadili mara ngapi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, imekuwa na matokeo? (Mara mbili.) Vipi kuhusu tabia ya haki ya Mungu? (Mara moja.) Idadi ya safari tulizojadili utakatifu wa Mungu pengine imeacha wazo kwako, lakini maudhui mahususi tuliyojadili kila mara yamekuwa na matokeo? Katika sehemu ya kwanza "mamlaka ya Mungu," kitu kipi kimeacha wazo wa kina sana kwako, ni sehemu gani imekuwa na matokeo makubwa kwako? (Mamlaka ya neno la Mungu na Mungu kama Mtawala wa vitu vyote.) Zungumza juu ya hoja muhimu. (Kwanza, Mungu alizungumza juu ya mamlaka na nguvu ya neno la Mungu; Mungu ni mwema kama neno Lake na neno Lake litakuwa kweli. Hiki ndicho kiini kabisa cha Mungu.) (Mamlaka ya Mungu yapo katika uumbaji Wake wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Hakuna mtu anaweza kugeuza mamlaka ya Mungu. Mungu ni Mtawala wa vitu vyote na Anadhibiti vitu vyote.) (Mungu anatumia upinde wa mvua na maagano pamoja na mwanadamu.) Haya ni maudhui mahususi. Kulikuwa na kitu kingine? (Maagizo ya Mungu kwa Shetani kwamba anaweza kumjaribu Ayubu, lakini hawezi kuchukua uhai wake. Kutokana na hili tunayaona mamlaka ya neno la Mungu.) Huu ni uelewa mlioupata baada ya kusikia ushirika, sio? Je, kuna kitu kingine cha kuongeza? (Hasa tunatambua kwamba mamlaka ya Mungu yanawakilisha hali na nafasi ya kipekee ya Mungu, na hakuna viumbe vilivyoumbwa au ambavyo havijaumbwa vinaweza kuwa na mamlaka Yake.) (Mungu anazungumza kuweka agano na mwanadamu na Anazungumza kuweka baraka Zake juu ya mwanadamu, hii yote ni mifano ya mamlaka ya neno la Mungu.) (Tunayaona mamlaka ya Mungu katika uumbaji wa mbingu na nchi, na vitu vyote kupitia neno Lake, na kwa Mungu katika mwili tunaona pia neno Lake linabeba mamlaka ya Mungu, hizi zote ni alama za upekee wa Mungu. Tunayaona pale ambapo Bwana Yesu alipomwamuru Lazaro kutoka kaburini: Uhai na kifo vipo chini ya udhibiti wa Mungu, ambapo Shetani hana uwezo wa kudhibiti; haijalishi kazi ya Mungu inafanyika katika mwili au katika Roho, mamlaka Yake ni ya pekee.) Je, mna kitu chochote kingine cha kuongezea? (Tunaona kwamba muungano wa mambo sita ya maisha huamuliwa na Mungu.) Vizuri sana! Kingine zaidi? (Baraka za Mungu kwa mwanadamu pia huwakilisha mamlaka Yake.) Tunapuzungumza kuhusu mamlaka ya Mungu, mnaelewa nini kuhusu neno "mamlaka"? Ndani ya mawanda ya mamlaka ya Mungu, katika kile ambacho Mungu anafanya na kufichua, watu wanaona nini? (Tunauona ukuu na hekima ya Mungu.) (Tunaona kwamba mamlaka ya Mungu yapo siku zote na kwamba kweli, kweli yapo.) (Tunayaona mamlaka ya Mungu kwa upana kwenye utawala Wake juu ya mbingu, na tunayaona kwa ufinyu kadri anavyodhibiti maisha ya binadamu. Kutokana muunganiko wa mambo sita ya maisha tunaona kwamba Mungu ni kweli anapanga na kudhibiti kila kipengele cha maisha yetu.) (Aidha, tunaona kwamba mamlaka ya Mungu yanamwakilisha Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, na hakuna viumbe vilivyoumbwa au ambavyo havijaumbwa vinaweza kuwa nayo. Mamlaka ya Mungu ni alama ya hadhi Yake.) "Alama za hadhi ya Mungu na nafasi ya Mungu," mnaonekana kuwa na uelewa wa kimafundisho wa maneno haya. Nimewauliza swali gani, mnaweza kulirudia? (Katika kile ambacho Mungu anafanya na kufichua, tunaona nini?) Unaona nini? Inaweza kuwa unaona tu mamlaka ya Mungu? Je, mlihisi tu mamlaka ya Mungu? (Tunauona uhalisia wa Mungu, hali ya ukweli wa Mungu, hali ya uaminifu wa Mungu.) (Tunaiona hekima ya Mungu.) Hali ya uaminifu wa Mungu, hali ya ukweli wa Mungu, na baadhi walisema hekima ya Mungu. Kuna kingine kipi? (Uweza wa Mungu.) (Kuiona haki na wema wa Mungu.) Bado hamjagusa kiini chenyewe, hivyo fikirieni kidogo zaidi. (Mamlaka na nguvu za Mungu vinafichuliwa na kuakisiwa katika kumwajibikia, kumwongoza, na kumsimamia binadamu. Hii ni halisi kabisa na kweli. Siku zote anafanya kazi Yake na hakuna viumbe vilivyoumbwa na ambavyo havikuumbwa vinaweza kuwa na mamlaka na nguvu hizi.) Ninyi nyote mnaangalia kwenye matini zenu? Je, kweli una maarifa yoyote ya mamlaka ya Mungu? Kuna yeyote kati yenu ambaye kweli ameelewa mamlaka Yake? (Mungu ametuangalia na kutulinda tangu tukiwa wadogo, na tunayaona mamlaka ya Mungu katika hilo. Siku zote hatukuwa tukielewa hali zilizokuwa zinatukuta, lakini Mungu siku zote alikuwa anatulinda kisiri; haya pia ni mamlaka ya Mungu.) Vizuri sana, imesemwa vyema!
Tunapozungumza kuhusu "mamlala ya Mungu," mkazo upo wapi, hoja kuu? Kwa nini tunahitaji kujadili maudhui haya? Kwanza, watu wanaweza kuelewa, kuona na kuhisi mamlaka ya Mungu. Kile unachokiona na kukihisi yote yanatokana na matendo ya Mungu, maneno ya Mungu na udhibiti wa Mungu wa ulimwengu. Hivyo, yote ambayo watu wanayaona kupitia mamlaka ya Mungu, yote ambayo wanajifunza kupitia mamlaka ya Mungu, au yale wanayoyatambua kupitia mamlaka ya Mungu, ni uelewa gani wa kweli unaopatikana kupitia haya? Kwanza, kusudi la kujadili maudhui haya ni kwa ajili ya watu kuyakinisha hadhi ya Mungu kama Muumbaji na nafsi Yake miongoni mwa vitu vyote. Pili, watu wanapoona yote ambayo Mungu amefanya na kusema na kuyadhibiti kupitia mamlaka Yake, inawafanya wao kuona nguvu na hekima ya Mungu. Inawafanya waone nguvu kuu ya Mungu kudhibiti kila kitu na jinsi gani alivyo mwenye hekima na kadri Anavyofanya hivyo. Je, hili si lengo na hoja kuu ya mamlaka ya pekee ya Mungu ambayo tulijadili hapo awali? Sio muda mrefu umepita na baadhi ya watu tayari wameshasahau hili, kitu kinachothibitisha kwamba hamjaelewa kikamilifu mamlaka ya Mungu; mtu anaweza hata kusema kwamba hujayaona mamlaka ya Mungu. Sasa mnaelewa hili angalau kidogo? Unapoyaona mamlaka ya Mungu katika vitendo, utahisi nini hasa? Mmeihisi kweli nguvu ya Mungu? (Tumehisi.) Unaposoma maneno ya Mungu kuhusu uumbaji Wake wa ulimwengu unaihisi nguvu Yake, unauhisi uweza Wake. Unapoona utawala wa Mungu juu ya hatima ya wanadamu, unahisi nini? Je, unaihisi nguvu Yake na hekima Yake? (Ndiyo.) Ikiwa Mungu hakuwa na nguvu hii, ikiwa hakuwa na hekima hii, je, angekuwa na sifa za kutawala ulimwengu na kuwa na utawala juu ya hatima ya wanadamu? (Asingekuwa na sifa.) Ikiwa mtu hana uwezo wa kufanya kazi yake, hana uwezo unaotakiwa na anakosa ujuzi na maarifa yanayotakiwa, anaweza kuwa na sifa ya kufanya kazi yake? Hakika hawawezi kuwa na sifa; uwezekano wa mtu kufanya mambo makubwa unategemea uwezo wao ni mkubwa kiasi gani. Mungu ana nguvu hizo na vile vile hekima, na hivyo Ana mamlaka; hii ni ya kipekee. Je, umewahi kumjua kiumbe yeyote au mtu ulimwenguni ambaye ana nguvu kama alizonazo Mungu? Je, kuna mtu yeyote au kitu chochote chenye nguvu za kuumba mbingu na nchi na vitu vyote vile vile kuvithibiti na kuvitawala? Je, kuna mtu yeyote au kitu chochote kinachoweza kutawala na kuwaongoza wanadamu wote na kuwapo siku zote na chenye uweza? (Hapana, hakuna.) Sasa unaelewa maana ya kweli ya yale yote yaliyomo katika mamlaka ya kipekee ya Mungu? Je, mna uelewa kiasi fulani? (Ndio, tunao.) Sasa tumemaliza kupitia hoja za mamlaka ya Mungu ya kipekee.
Sehemu ya pili tuliyozungumza ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.) Hatukujadili mambo mengi kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Kwa nini? Kuna sababu moja kuhusu hili: Kazi ya Mungu katika hatua hii kimsingi ni ya hukumu na kuadibu. Tabia ya haki ya Mungu imefichuliwa wazi katika Enzi ya Ufalme, kwa umahususi kabisa. Amesema maneno ambayo hajawahi kuyasema kutoka wakati wa uumbaji; na katika maneno Yake watu wote, wote ambao wameliona neno Lake, na wote ambao wamepitia uzoefu wa neno Lake wameiona tabia Yake ya haki ikifichuliwa. Siyo? Sasa hoja kuu ya kile tunachokijadili kuhusu tabia ya haki ya Mungu ni nini? Je, mmekuza ufahamu wa kina wa kile ambacho mmejifunza? Je, mmepata uelewa kutokana na uzoefu wenu wowote? (Mungu kuitekekeza Sodoma kwa moto ilikuwa ni kwa sababu watu wa wakati huo walikuwa waovu sana na hivyo wakaichochea ghadhabu ya Mungu. Ni kutokana na hili ndipo tunaiona tabia ya haki ya Mungu.) Kwanza, hebu tuangalie: Ikiwa Mungu asingeiangamiza Sodoma, je, ungeweza kuijua tabia Yake ya haki? Bado ungeweza kujua. Siyo? Unaweza kuiona kupitia maneno Aliyoyaeleza katika Enzi ya Ufalme, na pia kwa hukumu Yake, kuadibu, na laana zilizotolewa dhidi ya mwanadamu. Je, mnaiona tabia ya haki ya Mungu kwa kuacha kuiangamiza Ninawi? (Ndiyo.) Katika enzi hii, tunaweza kuona hali ya rehema, upendo na uvumilivu wa Mungu. Tunaweza kuiona pale ambapo wanadamu wanatubu na Mungu anakuwa na badiliko la moyo kwa wanadamu. Kwa kutumia mifano hii miwili kama kauli gezi kujadili tabia ya haki ya Mungu, iko wazi kabisa kuona kwamba tabia Yake ya haki imefichuliwa. Hata hivyo, katika uhalisia hii haiko tu kwa kile kilichorekodiwa katika visa viwili hivi vya Biblia. Kutokana na kile sasa umejifunza na kuona kupitia neno la Mungu na kazi Yake, kutokana na uzoefu wako wa sasa juu yao, tabia ya haki ya Mungu ni nini? Jadili kutokana na uzoefu wako binafsi. (Katika mazingira ambayo Mungu aliwatengenezea watu, pale wanapoweza kuutafuta ukweli na kutenda chini ya mapenzi ya Mungu, wanauona upendo na rehema Yake. Mungu huwaongoza, huwapa nuru, na kuwafanywa wahisi mwangaza ndani yao. Watu wanapokwenda kinyume cha Mungu na kumpinga na kwenda kinyume cha mapenzi Yake, kunakuwa na giza ndani yao, kana kwamba Mungu amewatelekeza. Kutokana na hili tumepitia utakatifu wa tabia ya haki ya Mungu; Mungu huonekana katika ufalme mtakatifu na Amefichwa katika maeneo ya uchafu.) (Kutokana na uzoefu wetu tunaiona tabia ya haki ya Mungu katika kazi ya Roho Mtakatifu. Tunapokuwa baridi, au hata kwenda kinyume na kumpinga Mungu, Roho Mtakatifu yupo, amefichwa na hachukui hatua yoyote. Wakati fulani tunaomba na hatumhisi Mungu, au hata tunaomba lakini hatujui nini cha kumwambia, lakini pale ambapo hali ya mtu inabadilika na wanakuwa tayari kushirikiana na Mungu na kuweka pembeni mawazo yao na kuweka pembeni dhana zao na kujitahidi kujiboresha, hapa ndipo uso wa tabasamu wa Mungu unaanza kuonekana taratibu.) Je, una kitu chochote kingine cha kuongeza? (Mungu anajificha pale ambapo mwanadamu Anamsaliti na Anampuuza mwanadamu.) (Ninaiona tabia ya haki ya Mungu kwa vile anavyowachukulia watu. Kaka zetu na dada zetu wanatofautiana katika kimo na ubora wa tabia, na kile ambacho Mungu anakitaka kutoka kwa kila mmoja wetu hutofautiana vile vile. Wote tunaweza kupokea nuru ya Mungu kwa viwango tofauti, na kwa namna hii ninaiona haki ya Mungu. Hii ni kwa sababu mwandamu hawezi kumtendea mwanadamu kwa namna hii hii, ni Mungu pekee ndiye anaweza kufanya hivyo.) Mm, nyote mmeongea maarifa ya kiutendaji.
Je, unaielewa hoja kuu kuhusu kuifahamu tabia ya haki ya Mungu? Kuhusiana na hili, tuna maneno mengi kutokana na uzoefu, lakini kuna hoja chache ambazo Napaswa kukuambia. Kuielewa tabia ya haki ya Mungu, kwanza mtu anapaswa kuelewa hisia za Mungu: kile Anachokichukia, kile Anachokichukia kabisa, na kile Anachokipenda. Mtu anapaswa kujua ambaye Anamvumilia, ambaye Anamrehemu, na mtu anapaswa kujua ni aina gani ya mtu anayepokea rehema hiyo. Hii ni hoja ya msingi kufahamu. Aidha, mtu anapaswa kuelewa kwamba haijalishi Mungu ni mwenye upendo kiasi gani, haijalishi ni Mwenye rehema na upendo kiasi gani kwa watu, Mungu hamvumilii mtu yeyote anayekosea hali na nafasi Yake, wala Hamvumilii mtu yeyote anayekosea heshima Yake. Ingawa Mungu anawapenda watu, Hawadekezi. Anawapatia watu upendo Wake, rehema Yake, na uvumilivu Wake, lakini hajawahi kuwakuwadia; Ana kanuni Zake na mipaka Yake. Bila kujali ni kwa kiwango gani umeuhisi upendo wa Mungu ndani yako, bila kujali upendo huo ni wa kina kiasi gani, mtu hapaswi kumchukulia Mungu kama ambavyo angemchukulia mtu mwingine. Ingawa ni kweli kwamba Mungu anawachukulia watu kama wako karibu Naye, ikiwa mtu anamwangalia Mungu kama mtu mwingine, kana kwamba kana kwamba alikuwa ni kiumbe mwengine wa uumbaji, kama rafiki au kama kitu cha kuabudu, Mungu atawaficha uso Wake na kuwatelekeza. Hii ndiyo tabia Yake, na hamvumilii mtu yeyote anayemchukulia kiholela katika suala hili. Hivyo mara nyingi tabia ya Mungu inasemwa katika neno Lake: Haijalishi umesafiri njia nyingi kiasi gani, umefanya kazi kubwa kiasi gani au umevumilia kiasi gani kwa ajili ya Mungu, mara tu unapoidhihaki tabia ya Mungu, Atamlipa kila mmoja wenu kulingana na kile ulichokifanya. Je, mmeiona? (Ndiyo, tumeiona.) Mmeiona, sio? Hii inamaana kwamba Mungu anaweza kuwaona watu kama wapo karibu na Yeye, lakini watu hawapaswi kumchukulia Mungu kama rafiki au ndugu. Usimchukulie Mungu kama rafiki yako. Hiajalishi ni upendo kiasi gani umepokea kutoka Kwake, haijalishi Amekuvumilia kwa kiasi gani, hupaswi kabisa kumchukulia Mungu kama rafiki tu. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu. Unaelewa, sio? (Ndiyo.) Je, kuna haja ya Mimi kusema zaidi kuhusu hili? Je, una uelewa wowote wa awali kuhusiana na suala hili? Kwa ujumla, hili ndilo kosa rahisi sana ambalo watu wanafanya bila kujali kama wanaelewa mafundisho, au kama hawajafikiria chochote kuyahusu hapo awali. Watu wanapomkosea Mungu, inaweza isiwe kwa tukio moja, au kitu kimoja walichokisema, bali ni kwa sababu ya mtazamo walionao na hali waliyomo. Hili ni jambo la kutisha sana. Baadhi ya watu wanaamini kwamba wana uelewa juu ya Mungu, kwamba wanamjua, hata wanaweza kufanya baadhi ya mambo ambayo yanaweza kumpendeza Mungu. Wanaanza kuhisi wako sawa na Mungu na kwamba kwa werevu wamekuwa na urafiki na Mungu. Aina hizi za hisia sio sahihi kabisa. Ikiwa huna uelewa wa kina juu ya hili, ikiwa hutambui vizuri hili, basi ni rahisi sana kumdhihaki Mungu na kudhihaki tabia Yake ya haki. Ninadhani unalielewa hili sasa, sio? (Ndiyo.) Je, tabia ya haki ya Mungu sio ya kipekee? Je, ni sawa na utu wa binadamu? Je, ni sawa na tabia binafsi za mwanadamu? Sivyo kabisa, sio? (Ndiyo.) Hivyo, hupaswi kusahau kwamba haijalishi ni kwa namna gani Mungu anawachukulia watu, hijalishi ni namna gani Anafikiri juu ya watu, nafasi, tabia na hadhi ya Mungu kamwe havibadiliki. Kwa binadamu, Mungu siku zote ni Bwana wa wote na Muumbaji! Unaelewa, sio? (Ndiyo.)
Umejifunza nini kuhusu utakatifu wa Mungu? Licha ya kuwa kinyume cha uovu wa Shetani, mada kuu katika kujadili utakatifu wa Mungu ilikuwa ni nini? Sio kwamba kile ambacho Mungu anacho na alicho. Je, kile ambacho Mungu anacho na alicho ni vya kipekee kwa Mungu Mwenyewe? (Ndiyo.) Hakuna chochote katika viumbe vyake kina hii, hivyo tunasema kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee, kitu ambacho unaweza kujifunza. Tulikuwa na mikutano mitatu juu ya utakatifu wa Mungu. Unaweza kufafanua kwa maneno yako mwenyewe, kwa uelewa wako mwenyewe, kile unachoamini ni utakatifu wa Mungu? (Mara ya mwisho ambapo Mungu aliwasiliana na sisi tulifanya kitu: Tulisujudu mbele Yake. Tulisikia pale anaposimama na tuliona kwamba tumepungukiwa na matakwa Yake; kusujudu kwetu mbele ya Mungu kwa kulazimishwa hakukuafikiani na mapenzi Yake na katika hili tuliona utakatifu wa Mungu.) Kweli kabisa, sio? Je, kuna kitu chochote kingine? (Katika neno la Mungu kwa mwanadamu, tunaona kwamba Anazungumza kwa wazi na kwa kueleweka, Analenga moja kwa moja kwenye hoja ya msingi. Shetani anazungumza kwa kuzungukazunguka na ni mwenye uongo mwingi. Kutokana na kile kilichotokea wakati uliopita wakati tuliposujudu kifudifudi mbele ya Mungu, tuliona kwamba maneno Yake na matendo Yake siku zote yanaongozwa na kanuni. Siku zote yupo wazi na wa kueleweka Anapotuambia jinsi gani tunavyopaswa kutenda, tunachopaswa kushikamana nacho, na jinsi gani tunavyopaswa kuchukua hatua. Lakini watu hawapo hivi; baada ya binadamu kuharibiwa na Shetani, watu walitafuta kufikia matakwa yao binafsi, na tamaa zao binafsi katika matendo na maneno yao. Kutokana na namna ambayo Mungu anamwangalia binadamu, kutokana na uangalizi na ulinzi Anaowapatia, tunaona kwamba yote ambayo Mungu anafanya ni mazuri, hii iko wazi kabisa. Ni kwa namna hii ndipo tunaona ufunuo wa kiini cha utakatifu wa Mungu.) Imewekwa vizuri! Kuna mtu yeyote wa kuongezea juu ya hili? (Tunauona utakatifu wa Mungu pale anapouweka wazi uovu wa Shetani na mara tu Mungu atuonyeshapo asili yake ni bora tumtambue ili tubainishe chanzo cha mateso yote ya mwanadamu. Hapo nyuma tulikuwa hatuna habari ya mateso chini ya utawala wa Shetani. Ni pale tu ambapo Mungu Alifanya ifahamike ndipo tuliona kwamba mateso yote yanayotokana na kuutafuta umaarufu na utajiri yote yametengenezwa na Shetani. Ni kupitia hili tu ndipo tunahisi kwamba utakatifu wa Mungu ni wokovu wa kweli wa binadamu. Aidha, Mungu anaandaa mazingira kwa ajili yetu ili kupokea wokovu; ingawa Anaweza asitufanye tuzaliwe katika familia ya kitajiri, Anahakikisha kwamba tumezaliwa katika familia inayofaa na katika mazingira yanayofaa. Aidha hatuachi tuteseke na madhara na ukandamizaji wa Shetani, ili kwamba tuwe na mazingira, tuwe na mawazo ya kawaida, na fikra za kawaida katika kuukubali wokovu wa Mungu katika siku za mwisho. Katika haya yote tunaona pia usahihi wa mipango ya Mungu, mipangilio Yake, na namna anavyoiweka katika utekelezaji. Tunaweza kuona vizuri kazi ya kina ya Mungu katika kutuokoa sisi kutoka katika ushawishi wa Shetani na tunauona utakatifu wa Mungu na upendo Wake kwa binadamu.) Kuna kitu chochote cha kuongezea hapo? (Kwa sababu hatuelewi kiini cha utakatifu wa Mungu, kulala kwetu chini mbele Yake katika ibada kumeghushiwa, kuna makusudi yaliyofichika na kwa kukusudia, kitu kinachomfanya Mungu asiwe na furaha. Ni kutokana na hili ndipo pia tunauona utakatifu wa Mungu. Mungu yupo tofauti sana na Shetani; Shetani anawataka watu kumsujudia na kujipendekeza kwake na kumwabudu. Shetani hana kanuni.) Vizuri sana! Kutokana na kile tulichoshiriki kuhusu utakatifu wa Mungu, je, mmeuona ukamilifu wa Mungu? (Tumeuona.) Ni kitu gani kingine unachokiona? Je, mnaona jinsi ambavyo Mungu ni chanzo cha mambo yote mazuri? Je, mnaweza kuona jinsi ambavyo Mungu ni mfano halisi wa ukweli na haki? Je, mnaona jinsi ambavyo Mungu ni chanzo cha upendo? Je, mnaona jinsi ambavyo yote ambayo Mungu anayafanya, yote ambayo anayatoa, na yote ambayo Anayafichua hayana makosa? (Tunaona hili.) Mifano hii kadhaa yote ni hoja kuu kuhusu utakatifu wa Mungu ambao Nauzungumzia. Unaweza kuchukulia maneno haya kama mafundisho tu, lakini siku moja utakapopita uzoefu na kumshuhudia Mungu wa kweli Mwenyewe kutoka katika neno Lake au kazi Yake, utasema kutoka katika moyo wako kwamba Mungu ni mtakatifu, kwamba Mungu ni tofauti na binadamu, na kwamba moyo Wake ni mtakatifu na tabia Yake ni takatifu, na asili Yake ni takatifu. Utakatifu huu unamruhusu mwanadamu kuuona ukamilifu Wake na vile vile humfanya mwanadamu kuona kwamba asili ya utakatifu wa Mungu haina mawaa. Asili ya utakatifu wake inaamua kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe wa kipekee, na inamwonyesha mwanadamu, na kuthibitisha kwamba ni Mungu Mwenyewe wa kipekee. Je, hii si hoja kuu? (Ni hoja kuu.)
Leo tumefanya muhtasari wa sehemu kadhaa za maudhui kutoka katika mikutano iliyotangulia. Tutakamilisha muhtasari wetu hapa. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wenu ataweka moyoni hoja kuu za kila kipengele na mada. Usizifikirie tu kuwa ni mafundisho; zisome zote na jaribu kuzitafakari pale unapopata muda. Zikumbuke katika moyo wako na ziweke katika vitendo na hakika utajifunza yote ambayo Nimesema kuhusu ufunuo wa kweli wa tabia ya Mungu na kile anacho na alicho. Hata hivyo hutaweza kuzielewa ikiwa utaziandika tu bila kuzisoma zote au kuzifikiria tena. Nina ukakika unaelewa! Baada ya kuviwasilisha vipengele hivi vitatu, watu watakuwa wamepata uelewa wa jumla au hata mahususi juu ya hadhi ya Mungu, asili Yake, na tabia Yake. Je, watakuwa na uelewa kamili juu ya Mungu lakini? (Hapana.) Sasa, katika uelewa wenu binafsi juu ya Mungu, je, kuna maeneo mengine ambapo mnahisi mnahitaji uelewa wa kina? Hiyo ni kusema, baada ya kuwa umepata uelewa wa mamlaka ya Mungu, tabia Yake ya haki, na utakatifu Wake, pengine umeyakinisha katika akili yako mwenyewe utambuzi wa hadhi na nafasi Yake ya kipekee, lakini kupitia uzoefu wako unapaswa kufahamu na kutambua matendo Yake, uwezo Wake, na asili Yake kabla ya kuweza kupata uelewa wa kina. Sasa mmesikiliza ushirika huu hivyo mnaweza kuweka moyoni mwako makala haya ya imani: Mungu kweli yupo na ni ukweli kwamba Anaendesha vitu vyote. Hakuna mwanadamu anayepaswa kuidhihaki tabia Yake ya haki na utakatifu Wake ni hakika kiasi kwamba mwanadamu hawezi kuushuku. Huu ni ukweli. Ushirika huu unafanya hadhi na nafasi ya Mungu kuwa na msingi katika mioyo ya watu. Baada ya msingi huu kuanzishwa, watu wanapaswa kutafuta zaidi uelewa wa kumjua kabisa Mungu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni