Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba Mungu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. Iwapo Mungu angefanya hili kweli, basi Mungu angekuwa mwenye haki? Mungu huamua matokeo ya watu kulingana na kanuni: Mwishowe matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na utendaji wao wa kibinafsi na tabia.
Huoni tabia ya Mungu yenye haki, na daima unamwelewa Mungu visivyo na kugeuza nia Zake, ambayo hukufanya daima uwe bila rajua na kupoteza matumaini. Je, hili si la kujiadhibu? Kwa kweli, unaelewa kweli, na una uhakika wa nia za Mungu? Daima umetumia “Majaaliwa ya Mungu” kusawiri na kukana maneno ya Mungu. Huku ni kumuelewa Mungu visivyo kukuu! Huelewi kazi ya Mungu na huyaelewi mapenzi ya Mungu katu; hata zaidi, huelewi nia nzuri ambazo Mungu ameweka katika miaka Yake 6,000 za kazi ya usimamizi! Unakuwa na moyo wa kukata tamaa, kubahatisha na kuwa na shaka na Mungu; unaogopa kwa kina kuwa mtendaji-huduma, ukifikiri, “Hakuna jambo kuu kunihusu; mbona nimepandishwa daraja ili kuifanya kazi hii? Je, Mungu ananitumia? Je, ni kwamba Ananifanya nitoe huduma na kisha kunifukuza wakati ambapo sina faida tena?” Je, si maoni haya yanambainisha Yeye na wale walio mamlakani? Daima umemwelewa Mungu visivyo; umewaza maovu kumhusu Mungu na kumchukia. Hujawahi kuyaamini maneno ya Mungu na kusema Kwake ukweli, umeanza mwenyewe kutafuta kuwa mtendaji-huduma, umeanza mwenyewe kutembea katika njia ya watendaji-huduma, lakini hujatafuta kubadili tabia yako wala hujapitia dhiki ili kuuweka ukweli kwenye vitendo. Mwishowe, umeyasukuma majukumu yako kwa Mungu, ukisema kuwa hukuwa umejaaliwa na Mungu, na kwamba Mungu hajakuwa wazi nawe. Je, tatizo ni lipi? Unayaelewa visivyo madhumuni ya Mungu, huyaamini maneno ya Mungu, huuweki ukweli kwenye vitendo wala kujitolea unapotimiza wajibu wako. Je, unawezaje kuyaridhisha mapenzi ya Mungu? Kwa huu mwelekeo wa matendo, hujahitimu hata kidogo kuwa mtendaji-huduma, hivyo unawezaje kuhitimu kujadiliana na Mungu? Ikiwa unafikiri kuwa Mungu si mwenye haki, basi kwanini unamwamini? Daima umetaka kusikia Mungu akikuambia, “Nyinyi ni watu wa ufalme na hili halitawahi kubadilika” kabla ya hamjajitahidi kwa ajili ya familia ya Mungu. Mungu asingesema hili, basi usingepeana moyo wako wa kweli kwa Mungu. Mtu wa aina hii ni mkaidi kiasi gani! Nimewaona watu wengi ambao hawajawahi kulenga kubadilisha tabia zao, hata zaidi hawajalenga kuuweka ukweli kwenye vitendo. Wao tu hutilia maanani kuuliza ikiwa watapata hatima nzuri ya mwisho, jinsi Mungu atakavyowashughulikia, ikiwa Ana majaaliwa yao kuwa watu Wake na mambo mengine ya uvumi. Je, watu hawa ambao hawajashughulika na kazi ya kweli wanawezaje kupata uzima wa milele? Je, wanawezaje kusalia katika familia ya Mungu? Sasa Ninawaambia kwa taadhima: Mtu aliyejaaliwa na Mungu asipouweka ukweli katika vitendo, basi ataondolewa mwishowe; na mtu anayetumia rasilmali yake na kufanya vyema ili kuuweka ukweli katika vitendo—hata ikiwa watu humwona kama mtu asiyejaaliwa kusalia—atakuwa na hatima nzuri zaidi kuwaliko wale wanaoitwa watu waliojaaliwa ambao hawajakuwa na kujitolea, kwa sababu ya tabia ya Mungu yenye haki. Je, unayaamini maneno haya? Iwapo huna uwezo wa kuyaamini maneno haya na unaendela na shughuli zako kwa njia mbaya, basi Ninakuambia kuwa hutaweza kusalia, kwa sababu humtaki Mungu kwa kweli na hujauzoea ukweli. Kwa vile ni hivi, kudura ya Mungu kwa watu si ya maana. Ninasema hili kwa sababu mwishowe, Mungu ataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji wao na mienendo; hata hivyo, tukizungumza bila upendeleo, majaaliwa ya Mungu yana kazi ndogo tu na hayana umuhimu mkubwa. Je, unayaelewa maneno haya?
2. Kazi ya Mungu katika Siku za Mwisho si kwa Madhumuni ya Kuwahukumu Watu, lakini badala yake Kuwaokoa Watu
Watu wengine husema: “Asili yangu si nzuri, yaache mambo yalivyo!” Je, huna uwezo wa kuunyima mwili? Je, huna moyo na akili? Je, mnaombaje kila siku? “Mwili, toka nje! Yaache mambo yalivyo, Mungu ameujaalia; sihitaji kufanya lolote.” Je, hili ndilo ombi lako? La! Basi kwanini hufanyi kazi na Mungu? Baadhi ya watu ambao wamelifanya kosa dogo watasema: Je, nitaangushwa na Mungu? Mungu hakuja wakati huu ili kuwaangusha watu, lakini badala yake kuwaokoa watu kwa kiwango kikubwa kiwezekanacho. Je, ni nani asiyefanya makosa kabisa? Je, kila mtu akiangushwa, basi unawezaje kuitwa wokovu? Makosa mengine hufanywa kimakusudi na makosa mengine kufanywa bila kupenda. Kwa mambo ya bila kupenda, unaweza kubadilika baada ya kuyatambua, hivyo Mungu angekugonga kabla hujabadilika? Je, hivi ndivyo Mungu huwaokoa watu? Si hivyo! Bila kujali iwapo unakosea bila kupenda ama kutokana na asili ya uasi, kumbuka tu: Harakisha na uuzindukie uhalisi! Endelea kwa bidii; bila kujali ni hali gani inayotokea, lazima uendelee kwa bidii. Mungu anafanya kazi ili kuwaokoa watu na Hatawagonga watu Anaotaka kuwaokoa bila taratibu. Bila kujali kiasi chako cha mgeuzo, hata kama Mungu angekuangusha mwishowe, basi Mungu angefanya hivyo kwa uhaki; wakati huo utakapofika, Atakufanya uelewe. Sasa hivi jukumu lako la pekee ni kuendelea kwa bidii, kutafuta kubadilishwa na kutafuta kumridhisha Mungu; unapaswa kujali tu kuhusu kuutimiza wajibu wako kulingana na mapenzi ya Mungu. Hapana kosa katika hili! Mwishowe, bila kujali jinsi Mungu anavyokushughulikia, hilo daima hufanywa katika uhaki; hupaswi kushuku hili au kuwa na wasiwasi nalo; hata kama huwezi kuelewa uhaki wa Mungu hivi sasa, kutakuwa na siku ambayo utaridhishwa. Hakika Mungu si kama mkuu wa serikali ama mfalme wa ibilisi! Mkijaribu kuelewa kipengele hiki kwa makini, basi mwishowe mtaamini kwa udhabiti kuwa kazi ya Mungu ni kuwaokoa watu na kubadilisha tabia za watu. Kwa kuwa ni kazi ya kuzibadilisha tabia za watu, watu wasipofichua tabia zao, basi hakuna linaloweza kufanywa na hakutakuwa na matokeo yoyote. Lakini baada ya kufichua tabia yako, kuendelea hivyo kutakuwa kwa taabu, kutakosea amri za utawala na kumkosea Mungu. Mungu atatoa adhabu za kiasi tofauti, na utalipa gharama kwa dhambi zako. Mara chache wewe hupotoka bila kufahamu na Mungu hukuonyesha, hukupogoa, na kukushughulikia; ukifanya vyema, Mungu hatakulaumu. Hii ndio namna ya kawaida ya mgeuzo; umuhimu wa kweli wa kazi ya wokovu unajitokeza katika mchakato huu. Huu ndio ufunguo! Chukua kwa mfano mipaka kati ya wanaume na wanawake; leo unatenda kwa ajili ya raghba ya kuushika mkono wa mtu, lakini unaporudi unatafakari: Je, hii sio tabia potovu? Je, hii sio dhambi? Je, hii sio tahayari kwa Mungu wakati ambapo mipaka kati ya wanaume na wanawake hauzingatiwi? Je, ninawezaje kufanya kitu cha aina hii? Kisha unakuja mbele za Mungu na kuomba: “Ee Mungu! Nimekosa tena; jambo hili halipatani na ukweli na nauchukia mwili uliopotoka.” Baadaye, unaweka azimio la kutowashika au kuwakaribia sana. Je, huu si mgeuzo? Ikiwa una mbadiliko wa aina hii, je, Mungu bado atakuhukumu kwa kuwashika mkono? Ikiwa uliishika mikono yao na hukuhisi vyema kuhusu hilo, na usiikiri dhambi yako kwa Mungu, ukifkiri kuwa halikuwa jambo la aibu, na hujidharau, kuwa mwangalifu, ama kuwa na azimio, basi baadaye hutaishika mikono yao tu, utawakumbatia! Mambo yatakuwa mazito zaidi na zaidi na yatakupelekea kufanya dhambi, na katika kufanya hivyo, Mungu atakuhukumu kwa dhambi zako; utafanya dhambi tena na tena, haina tiba. Kama kwa kweli ungefichua sehemu ndogo ya tabia iliyopotoka pasipo kutaka, ukiweza kutubu, basi Mungu hatakuhukumu na bado unaweza kuokolewa. Mungu anataka kuwaokoa watu, na haiwezekani kwa asili za watu kutofichuliwa kwa kiasi fulani; hata hivyo, unapaswa kuzingatia kutubu na kubadilika kwa haraka. Je, hili halingeridhisha mapenzi ya Mungu? Watu wengine hawaamini haya na daima wanakuwa na mtazamo wa kujihadhari kumhusu Mungu; mtu wa aina hii atateseka siku moja.
Imetajwa hapo awali: Matukio yaliyopita yanaweza kufutwa kwa alama ya kalamu; siku za baadaye zaweza kuchukua nafasi ya yaliyopita; uvumilivu wa Mungu hauna mipaka. Lakini maneno haya yana kanuni ndani yake; si kweli kwamba bila kujali umetenda dhambi kuu kiasi gani mwishowe, Mungu anaweza kuifuta kwa alama moja; kazi yote ya Mungu ina kanuni. Zamani kulikuwa na aina hii ya amri ya utawala: Yule ambaye alifanya dhambi fulani kabla ya kulikubali jina la Mungu, mwache ajiunge; akifanya dhambi hiyo tena baada ya kuingia, mshughulikie kwa njia fulani; akirudia kufanya dhambi iyo hiyo tena, basi mfukuze. Mungu daima amewasamehe watu kwa kiwango kikubwa sana kinachowezekana katika kazi Yake; kutoka kwa mtazamo huu, inaweza kuonekana kuwa kazi hii kweli ni kazi ya kuwaokoa watu. Lakini katika hatua hii ya mwisho ukifanya dhambi isiyosameheka bado, hutaweza kuponywa ama kuweza kubadilika. Mungu ana mchakato wa kubadilisha tabia za watu na wa kuwaokoa watu. Kupitia kwa mchakato wa watu kufichua tabia zao, Mungu atawabadilisha; kupitia njia ya watu kufichua na kubadilisha tabia zao siku zote, Mungu hupata lengo Lake la wokovu. Baadhi ya watu hufikiri: Kwa kuwa ni asili yangu, basi nitaionyesha zaidi iwezekanavyo! Baadaye, nitaitambua na kuuweka ukweli kwenye vitendo. Je, huu mchakato ni wa lazima? Ikiwa kwa kweli wewe ni mtu unayeuweka ukweli kwenye vitendo, na ukiona kwamba pia una matatizo ambayo wengine wanayo, basi utafanya bidii kuepuka kuyafanya mambo hayo. Je, huu si mgeuzo usio wa moja kwa moja? Wakati mwingine, unafikiri kufanya namna ile, lakini kabla ya kufanya, unafahamu na kuiacha. Je, hili halipati matokeo ya wokovu? Kuna mchakato wa kuuweka ukweli wote kwenye vitendo; ni vigumu kwako kuwa mtimilifu na kutokuwa na mawazo ya kighushi unapoanza kutenda. Bado kuna vitu kadha ambavyo kwavyo unategemea mawazo yako mwenyewe kabisa, lakini baada ya kushughulikiwa na kupogolewa, mwishowe utatenda kulingana na nia na maneno ya Mungu kikamilifu. Haya ni mbadiliko na mgeuzo.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni