5/21/2018

Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno La Mungu Kuhusu “Fumbo La Kupata Mwili” (part 2)

16. Mungu anakuja tu duniani kukamilisha kazi Yake, na kwa hivyo Kazi Yake duniani ni ya muda mfupi. Haji duniani na nia ya Roho wa Mungu kukuza mwili Wake kuwa mkuu wa kipekee wa kanisa. Mungu anapokuja duniani, ni Neno ambalo kugeuka kuwa mwili; mwanadamu, hata hivyo, hajui kuhusu kazi Yake na kwa nguvu anaona Yeye kuwa sababu ya mambo. Lakini nyote mnapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Neno lililogeuka kuwa mwili, na sio mwili uliokuzwa na Roho wa Mungu ili kusimamia nafasi ya Mungu kwa ufupi. Mungu Mwenyewe hakuzwi, ila ni Neno kugeuka mwili, na leo hii Anatekeleza kazi Yake kirasmi miongoni mwenu.
17. Mungu hugeuka mwili ili tu Aiongoze enzi na Aanzishe kazi mpya. Lazima muelewe hoja hii. Hii ni tofauti kabisa na kazi ya mwanadamu, na mawili haya hayawezi kuzungumzwa kwa pamoja. Mwanadamu anahitaji muda mrefu wa kukuzwa na kufanywa mkamilifu kabla mwanadamu aweze kutumiwa kutekeleza kazi, na uanadamu wa hali ya juu unahitajika. Mwanadamu hapaswi kudumisha hali yake ya uanadamu wa kawaida tu, bali pia mwanadamu zaidi ya hapo lazima aelewe kanuni nyingi na sheria za tabia kabla ya mengine, na zaidi ya hayo lazima ajifunze zaidi kuhusu hekima na maadili ya mwanadamu. Haya ndiyo mwanadamu lazima kujengwa nayo. Hata hivyo, hivi sivyo ilivo na Mungu mwenye mwili, kwa maana kazi Yake haimwakilishi mwanadamu na wala si ya binadamu; bali ni dhihirisho la moja kwa moja la hali Yake na utekelezi wa moja kwa moja wa kazi Anayopaswa kufanya. (Kwa kawaida, kazi Yake hufanyika wakati inapaswa kufanyika, na sio tu wakati wowote kiholela. Badala Yake, kazi Yake hufanyika wakati ambapo ni wakati wa kukamilisha huduma Yake). Yeye hajihusishi katika maisha ya mwanadamu wala katika kazi ya mwanadamu, hiyo inamaanisha, uanadamu Wake haujengwi na yoyote kati ya haya (lakini hili haliathiri kazi Yake). Anatimiza huduma Yake tu ikiwa wakati umewadia wa kufanya hivyo; haijalishi hali Aliyomo, Yeye huendelea mbele na kazi Anayopaswa kufanya. Haijalishi mwanadamu anajua nini kumhusu, au maoni ya mwanadamu kumhusu, kazi Yake haiathiriki. Hii ni kama tu vile Yesu Alivyofanya kazi Yake; hakuna Aliyejua Yeye ni nani, lakini Aliendelea tu mbele na kazi Yake. Mambo haya hayakumuathiri katika utendaji wa kazi Yake Aliyopaswa kufanya. Kwa hivyo, Hakukiri au kutangaza kuwa Yeye ni nani, na Yeye Alimfanya mwanadamu Amfuate tu. Kwa kawaida, huu haukuwa tu uvumilivu wa Mungu; ilikuwa ni njia ambayo Yesu Anafanya kazi katika mwili. Angeweza tu kufanya kazi kwa namna hii, kwani mwanadamu hangeweza kumtambua Yesu kwa jicho la kawaida. Na hata kama mwanadamu angeweza, mwanadamu hangeweza kusaidia katika kazi Yake. Zaidi ya hayo, hakugeuka mwili ili mwanadamu apate kujua mwili huu Wake; ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi Yake na kukamilisha huduma Yake. Kwa sababu hii, hakutilia maanani hali ya kufanya Ajulikane. Alipokamilisha kazi Aliyopaswa kufanya, utambulisho Wake na hadhi Yake vilijulikana wazi kwa mwanadamu. Mungu mwenye mwili hukaa kimya na hafanyi matangazo yoyote. Yeye hajishughulishi na mwanadamu au vile mwanadamu anaendelea katika kumfuata, na yeye husonga tu mbele katika kutimiza huduma Yake na kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Hakuna Anayeweza kusimama mbele ya njia ya kazi Yake. Wakati muda unawadia wa kazi Yake kukamilika, ni muhimu kazi hiyo ikamilike na kufikishwa kikomo. Hakuna anayeweza kusema vinginevyo. Baada tu ya Yeye kuondoka kutoka kwa mwanadamu baada ya kukamilisha kazi Yake ndipo mwanadamu ataelewa kazi Anayofanya, ingawa hataifahamu kikamilifu. Na itachukua muda mrefu ndipo mwanadamu aelewe nia Yake Alipofanya kazi hiyo mara ya kwanza. Kwa maneno mengine, kazi ya enzi ambapo Mungu anageuka mwili imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu moja ni kupitia katika kazi na maneno ya Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Pindi tu huduma ya mwili Wake imetimika kikamilifu, sehemu nyingine ya kazi inatakiwa kutekelezwa na Roho Mtakatifu; basi utakuwa wakati wa mwanadamu kutimiza wajibu wake, kwa maana Mungu ameshafungua njia tayari, na lazima itembelewe na mwanadamu mwenyewe. Hiyo ni kusema, Mungu anageuka kuwa mwili ili kutekeleza sehemu moja ya kazi Yake, na inaendelezwa kwa urithi na Roho Mtakatifu na vile vile wale watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Kwa hivyo mwanadamu anapaswa kujua kazi ya msingi inayopaswa kutekelezwa na Mungu mwenye mwili katika hatua hii ya kazi. Mwanadamu lazima aelewe hasa umuhimu wa Mungu kugeuka kuwa mwili na kazi Anayopaswa kufanya, badala ya kumuuliza Mungu ni nini kinachotakiwa kwa mwanadamu. Haya ni makosa ya mwanadamu, na vile vile fikira, na zaidi ya hayo, ni kutotii kwake.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana Katika Mwili
19. Kazi ya kila enzi huanzishwa na Mungu Mwenyewe, lakini unapaswa kujua kwamba licha ya kazi yoyote ya Mungu, Yeye haji kuanzisha muungano au kufanya mikutano yoyote halisi au kuanzisha makundi ya aina yoyote kwa ajili yenu. Yeye huja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Kazi Yake haizuiliwi na mwanadamu yeyote. Yeye hufanya kazi Yake vile Anavyopenda; haijalishi kile mwanadamu anajua au kufikiri, Yeye hutilia maanani katika kutekeleza kazi Yake. Tangu kuumbwa kwa dunia, kumekuwa na hatua tatu za kazi; kutoka kwa Yehova mpaka kwa Yesu, na kutoka kwa Enzi ya Sheria mpaka kwa Enzi ya Neema, Mungu hajawahi kuitisha mkutano halisi kwa mwanadamu, wala hajawahi kuwakusanya wanadamu wote pamoja kufanya mkutano halisi wa ulimwengu ili kupanua kazi Yake. Yeye hufanya tu kazi ya mwanzo wa enzi nzima wakati muda na wakati na mahali uko sawa, na kupitia kwa hili Anaikaribisha enzi ili kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Mikutano halisi ni mikutano ya wanadamu; kuwakusanya watu pamoja kusherehekea siku kuu katika kazi za mwanadamu. Mungu hasherehekei siku kuu na, zaidi ya hayo, Anachukizwa nazo; Yeye haitishi mikutano halisi na zaidi ya hayo Anachukizwa nayo. Sasa lazima uelewe ni nini hasa kazi ya Mungu mwenye mwili!
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (3)" katika Neno Laonekana Katika Mwili
20. Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi ya Sheria tu, na zaidi ya hayo, ni katika wakati huu wa siku za mwisho. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inawakilisha hukumu, gadhabu na kuadibu. Kazi ifanywayo katika siku za mwisho haiwezi kuwekwa mbadala wa kazi ya Enzi ya Sheria ama ile ya Enzi ya Neema. Ingawa, hatua zote tatu zinaungana kuwa kitu kimoja na yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kawaida, utekelezaji wa kazi hizi umegawanyishwa katika enzi tofauti. Kazi iliyofanywa katika siku za mwisho inaleta kila kitu mpaka tamati; ile iliyofanywa katika Enzi ya Sheria ni ya mwanzo; na ile iliyofanywa katika Enzi ya Neema ni ya ukombozi. Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita, hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa. Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati. Katika siku za mwisho, kazi ya neno pekee inafanyika ili kuukaribisha Wakati wa Ufalme lakini haiwakilishi enzi zile zingine. Siku za mwisho sio zaidi ya siku za mwisho na sio zaidi ya Enzi ya Ufalme, ambayo haiwakilishi Enzi ya Neema au Enzi ya Sheria. Siku za mwisho ni wakati ambapo kazi zote ndani ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita inafichuliwa kwenu. Mafumbo kama hayo hayawezi kufichuliwa na mwanadamu yeyote. Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi, yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi, kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia. Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli, kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu, lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo, kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee, sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu, na mwanadamu hawezi kufumbu mafumbo ya kazi ya aina hiyo. Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu, iliyofichwa zaidi na isiyosahawishika kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama, Yeye Mwenyewe Aeleze na kumfungulia mwanadamu, vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele. Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini; kama hamngeambiwa leo, pia nyinyi hamngeweza kuelewa.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
21. Kazi katika siku za mwisho ni hatua ya mwisho kati ya hizo tatu. Ni kazi ya enzi nyingine mpya na haiwakilishi kazi ya usimamizi mzima. Mpango wa miaka elfu sita umegawawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya yote. Jina Yehova haliwezi kuwakilisha tabia yote ya Mungu. Ukweli kuwa Alitekeleza kazi katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kuwa Mungu Anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria. Yehova alitengeneza sheria kwa mwanadamu na kutoa amri, Akimuuliza mwanadamu ajenge hekalu na madhabahu; kazi Aliyofanya inawakilisha tu Enzi ya Sheria. Kazi Alioyoifanya haidhibitishi kuwa Mungu ni Mungu Anayemwamuru mwanadamu kufuata sheria, Mungu Aliye hekaluni, ama Mungu Aliye mbele ya madhabahu. Haya hayawezi kusemwa. Kazi chini ya sheria inaweza tu kuwakilisha enzi moja. Kwa hivyo, kama Mungu Alifanya kazi katika Enzi ya Sheria pekee, mwanadamu angemfafanua Mungu na kusema, "Mungu ni Mungu Aliye hekaluni. Ili kumtumikia Mungu, lazima tuvae mavazi ya kikuhani na tuingie hekaluni." Iwapo kazi katika Enzi ya Neema haingetekelezwa na Enzi ya Sheria ingeendelea mpaka wakati huu wa sasa, mwanadamu hangefahamu kuwa Mungu pia ni mwenye huruma na upendo. Iwapo kazi katika Enzi ya Sheria haingefanywa, na kwamba tu ile ya Enzi ya Neema ndiyo iliyofanywa, mwanadamu angefahamu tu kwamba Mungu Anakomboa mwanadamu na kumsamehe dhambi zake. Wangefahamu tu kuwa Yeye ni mtakatifu na asiye na hatia, kwamba Anaweza kujitoa kafara na kusulubishwa kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu angejua tu kuhusu haya na asiwe na ufahamu wa mambo mengine yoyote. Kwa hivyo kila enzi inawakilisha sehemu moja ya tabia ya Mungu. Enzi ya Sheria inawakilisha vipengelele vingine, Enzi ya Neema vipengele vingine na enzi hii vipengele vingine. Tabia ya Mungu inaweza tu kuonekana kwa mchanganyiko wa hatua zote tatu. Ni wakati tu mwanadamu anajua hatua hizi tatu ndipo anaweza kuipokea kikamilifu. Hakuna hatua kati ya hizo tatu ambayo inaweza kuachwa. Utaiona tu tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake mara tu utakapozijua hatua hizi tatu za kazi. Mungu kukamilisha kazi yake katika Enzi ya Sheria sio ushahidi kwamba Yeye ni Mungu chini ya sheria, na kukamilika kwa kazi Yake ya ukombozi haionyeshi kuwa Mungu Atamkomboa mwanadamu milele. Hizi zote ni hitimisho zilizofanywa na mwanadamu kuhusu jambo hilo. Enzi ya Neema imefika mwisho, lakini huwezi kusema kuwa Mungu ni wa msalaba tu na kuwa msalaba unawakilisha wokovu wa Mungu. Ukifanya hivyo, basi utakuwa unamfasili Mungu. Katika hatua hii, Mungu Anafanya zaidi kazi ya Neno, lakini huwezi kusema kuwa Mungu hajawahi kuwa Mwenye huruma kwa mwanadamu na kwamba yote Aliyoleta ni kuadibu na hukumu. Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao. Baada tu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilishwa ndipo mwanadamu atapata kuelewa tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake, kwani usimamizi Wake utakuwa umefika mwisho.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
22. Kazi yote iliyofanyika katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita imefika mwisho sasa. Ni baada tu ya kazi hii kubainika wazi kwa mwanadamu na kutekelezwa miongoni mwa wanadamu ndipo watakapofahamu tabia Yake na mali Yake na uwepo. Kazi za enzi hizi zitakapokamilika, mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu yatakuwa yamebainika, ukweli wote ambao haukuwa unaeleweka utawekwa wazi, na mwanadamu atakuwa ameambiwa njia na hatima ya baadaye. Hii ndio kazi yote inayopaswa kufanyika katika hatua hii.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
24. Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini haimaanishi kuwa mwanadamu hana dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia potovu za zamani za kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwena Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na uonekano wa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendeleaa na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupuwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
25. Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu ataskia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mwanadamu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" katika Mwili Neno Laonekana
28. Kile ambacho mwanadamu amepata sasa—kimo cha mwanadamu leo, maarifa yao, upendo, uaminifu, utiifu, na pia kuona kwao—ni matokeo yanayopatikana kupitia hukumu kwa neno. Kwamba unaweza kuwa na uaminifu na kubaki umesimama mpaka siku hii ipatikane kwa kupita neno. Hivi sasa mwanadamu anaona kuwa kazi ya Mungu kupata mwili ni ya ajabu kweli. Kuna mengi ambayo hayawezi kupatikana na mwanadamu; ni mafumbo na maajabu. Kwa hivyo, wengi wamejiwasilisha. Wengine hawajawahi kujiwasilisha kwa mwanadamu yeyote kutoka siku za kuzaliwa kwao, ilhali wanapoyaona maneno ya Mungu siku hii, wanajiwasilisha kikamilifu bila kujua wamefanya vile, na hawajaribu kuchunguza au kusema chochote kingine. Mwanadamu ameanguka chini ya neno na chini ya hukumu kupitia kwa neno. Kama Roho wa Mungu angemwongelesha mwanadamu moja kwa moja, wote wangejiwasilisha kwa sauti hiyo, na kuanguka chini bila maneno ya ufunuo, vile Paulo alivyoanguka chini kukiwa na nuru alipokuwa akisafiri kwenda Damasko. Mungu angeendelea kufanya kazi kwa njia hii, mwanadamu hangeweza kutambua upotovu wake kupitia kwa hukumu katika neno na kupata wokovu. Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili wa Mungu; Ananena na kutekeleza hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili. Inafanyika kuonyesha mamlaka ya Mungu mwenye mwili, matokeo yanayopatikana na kazi ya neno, na kwamba Roho Amekuja kwa mwili; Anaonyesha mamlaka Yake kupitia hukumu juu ya mwanadamu kwa neno. Ingawa mwili Wake ni hali ya nje ya mwanadamu wa kawaida, ni matokeo ambayo neno Lake linapokea ndiyo yanamwonyesha mwanadamu kuwa Amejaa mamlaka, kwama ni Mungu Mwenyewe na kwamba maneno Yake ni uelezo wa Mungu Mwenyewe. Hii inaonyesha wanadamu wote kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe Aliyekuwa mwili, na kwamba Hawezi kukosewa na yeyote. Hakuna anayeweza kuepuka hukumu Yake kupitia kwa neno, na hakuna nguvu ya giza inayoweza kutamalaki juu ya mamlaka Yake.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
29. Anakuwa mwili kwani mwili pia unaweza kuwa na mamlaka, na Anaweza kutekeleza kazi kati ya wanadamu katika halii ya njia halisi, inayoonekana na kuguswa na mwanadamu. Kazi kama hii ni ya ukweli kuliko kazi ingine yoyote ifanywayo moja kwa moja na Roho wa Mungu Aliye na mamlaka yote, na matokeo Yake ni dhahiri pia. Hii ni kwa sababu mwili Wake unaweza kuongea na kufanya kazi kwa njia halisi; hali ya nje ya mwili Wake haina mamlaka yoyote na inaweza kukaribiwa na mwanadamu. Dutu Yake inabeba mamlaka, lakini mamlaka Yake hayaonekani kwa yeyote. Anaponena na kufanya kazi, mwanadamu hana uwezo wa kutambua uwepo wa mamlaka Yake; hili ni nzuri kwa kazi Yake hata zaidi. Na kazi yote kama hiyo inaweza kupata matokeo. Ingawa hakuna mwanadamu anayefahamu kuwa Anayo mamlaka ama kuona kuwa hawezi kukosewa ama kuona hasira Yake, kupitia mamlaka Yake yaliyofichika na hasira na hotuba ya uma, Anapata matokeo yaliyotarajiwa ya neno Lake. Kwa maneno mengine, kupitia kwa tani ya sauti Yake, ukali wa hotuba Yake, na hekima ya maneno Yake, mwanadamu anashawishika kabisa. Kwa njia hii, mwanadamu anawasilisha kwa neno la Mungu mwenye mwili wa Mungu, ambaye anaonekana kutokuwa na mamlaka, hivyo kufikia lengo Lake la wokovu kwa mwanadamu. Huu ndio umuhimu mwingine wa kuingia Kwake katika mwili: kuongea na ukweli zaidi na kukubali ukweli wa neno Lake kuwa na athari juu ya mwanadamu ili kushuhudia nguvu ya neno la Mungu. Kwa hivyo kazi hii, isipofanywa kupitia kupata mwili, haitakuwa na matokeo hata kidogo na haitaweza kuokoa watenda dhambi kikamilifu. Mungu Asipokuwa mwili, Atabaki kama Roho bila kuonekana au kuguswa na mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe wa mwili, na mwanadamu na Mungu ni wa dunia mbili tofauti na ni tofauti kwa asili. Roho wa Mungu hana uuwiano na mwili wa mwanadamu, na hakuna uhusiano unaoweza kuwepo kati yao; pia, mwanadamu hawezi kuwa roho. Hivyo, Roho wa Mungu lazima ageuke mmoja wa viumbe na kufanya kazi yake ya asili. Mungu anaweza kujipandisha mahali pa juu zaidi na pia aweze kunyenyekea na kuwa mwanadamu aliyeumbwa, kufanya kazi na kuishi kati ya wanadamu, laikini mwanadamu hawezi kupanda juu na kuwa roho na pia kuteremka chini. Kwa hivyo, Mungu lazima awe mwili ili atekeleze kazi Yake. Kama ilivyokuwa wakati wa kuingia katika mwili mara ya kwanza, mwili wa Mungu mwenye mwili pekee ndio unaoweza kumkomboa mwanadamu kupitia kusulubiwa, ilhali hakuna uwezo wa Roho wa Mungu kusulubiwa kama sadaka ya dhambi kwa mwanadamu. Mungu Angekuwa mwili moja kwa moja ili kuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, lakini mwanadamu hangepanda mbinguni moja kwa moja kuchukua sadaka ambayo Mungu alikuwa amewaandalia. Hivyo, lazima Mungu asafiri kwenda na kurudi kati ya mbingu na nchi, badala ya kumwacha mwanadamu apande mbinguni kuchukua wokovu huu, kwani mwanadamu alikuwa ameanguka na hangepanda mbinguni, ama hata kupata sadaka ya dhambi. Kwa hivyo, ilikuwa lazima kwa Yesu kuja kati ya wanadamu na binafsi kufanya kazi ambayo mwanadamu hangeweza kukamilisha. Kila wakati ambapo Mungu aligeuka kuwa mwili, ilikuwa lazima kabisa Afanye hivyo. Iwapo hatua yoyote ingetekelezwa moja kwa moja na Roho wa Mungu, Hangevumilia ukosefu wa hadhi unaoambatana na kupata mwili.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
30. Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumua kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na kujua dutu yao. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Hafanyi hivyo pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya. Manabii waliongelea unabii pekee, ya kile kitakachotendeka hapo baadaye, lakini sio kazi ambayo Mungu angefanya katika wakati huo. Hawakuongea kuongoza mwanadamu katika maisha yao, kuhifadhi ukweli juu ya mwanadamu ama kumfichulia mwanadamu mafumbo, ama hata kutawaza maisha. Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu. Maneno ya wakati huu sio kama unabii wa manabii. Hii ni hatua ya kazi isioya unabii ila ya maisha ya mwanadamu, kubadili tabia ya maisha ya mwanadamu. Hatua ya kwanza ilikuwa kazi ya Yehova kutengeneza njia ya mwanadamu kuabudu Mungu duniani. Ilikuwa kazi ya kuanzisha kutafuta chanzo cha kazi duniani. Wakati huo, Yehova aliwafunza Waisraeli kuiheshimu Sabato, kuwaheshimu wazazi wao na kuishi kwa amani na wengine. Kwa kuwa wanadamu wa wakati huo hawakuwa wanaelewa kiini cha mwanadamu, wala hawakuelewa wanavyopaswa kuishi duniani, ilikuwa lazima Kwake katika hatua ya kwanza ya kazi kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Yote yale Yehova aliwazungumzia hayakuwa yamewahi kujulikana kwa binadamu ama kuwa katika umiliki wao. Wakati huo, manabii wengi walisimamishwa kuongelea unabii, yote kutengenezwa chini ya uongozi wa Yehova. Hii ilikuwa sehemu ya kazi hiyo. Katika hatua ya kwanza, Mungu hakuwa mwili, hivyo Alizungumza na makabila yote na mataifa kupitia kwa manabii. Yesu alipofanya kazi Yake katika huo wakati, Hakuzungumza sana kama wakati huu wa leo. Kazi hii ya neno katika siku za mwisho haijafanyika katika enzi na vizazi vilivyopita. Ingawa Isaya, Danieli na Yohana walitabiri utabiri mwingi, unabii huo ulikuwa tofauti kabisa na maneno yazungumzwayo sasa. Walichoongelea ulikuwa unabii pekee, lakini maneno ya sasa sio unabii. Iwapo Ningebadilisha Ninayoongea sasa yawe unabii, je mngeweza kuyaelewa? Iwapo ningezungumzia mambo ya usoni, maneno ya baada ya mimi kuondoka, utawezaje kupata kuelewa? Kazi ya neno haikuwahi kufanyika wakati wa Yesu ama Enzi ya Sheria. Labda wengine wanaweza kusema, "Je Yehova hakuzungumza maneno pia katika wakati wa kazi Yake? Juu yaa kuponya magonjwa, kukemea mapepo na kufanya ishara na maajabu, je Yesu hakuzungumza katika wakati huo?" Kuna tofauti katika vile maneno yananenwa. Ni nini ndiyo ilikuwa dutu ya maneno yaliyonenwa na Yehova? Alikuwa tu anawaongoza wanadamu katika maisha yao duniani, ambayo hayakuwa yanahusiana na mambo ya kiroho katika maisha. Ni kwa nini inasemekana kuwa maneno ya Yehova yalitangazwa katika sehemu zote? Neno "kutangazwa" linamaanisha kutoa maelezo kamili na maelezo ya moja kwa moja. Hakupa mwanadamu maisha; ila, Alimchukua mwanadamu kwa mkono na kumfunza jinsi ya kumheshimu sana. Hakukuwa na mafumbo. Kazi ya Yehova katika Israeli haikuwa kushughulika na ama kumwadhibu mwanadamu ama kutoa hukumu na kuadibu; ilikuwa kuongoza. Yehova alimwambia Musa awaeleze watu Wake wakusanye mana jangwani. Kila asubuhi kabla ya jua kuchomoza, walikuwa wakusanye mana, iliyotosha tu kuliwa siku hiyo. Mana haingewekwa hadi siku inayofuata, kwani ingeoza. Hakuwafunza wanadamu kufichua asili zao, na Hakufichua mawazo yao na fikira. Hakuwabadilisha wanadamu ila tu aliwaongoza katika maisha yao. Katika wakati huo, mwanadamu alikuwa kama mtoto; mwanadamu hakuelewa chochote na angefanya hatua za kuelekezwa; kwa hivyo, Yehova aliamuru tu sheria kuongoza watu. Iwapo unataka kueneza injili ili wale wote wanaotafuta kwa moyo wa kweli wapate maarifa ya kazi inayofanywa katika siku hii na kushawishika kabisa, basi lazima uielewe hadithi ya ndani, dutu na umuhimu wa kazi iliyofanywa katika kila hatua. Kwa kusikia ushirika wako, wataelewa kazi ya Yehova na kazi ya Yesu na, zaidi ya hayo, kazi yote inayofanywa wakati huu, na vilevile uhusiano na tofauti kati ya hatua hizo tatu za kazi, ili kwamba, baada ya wao kisikiza, wataona kuwa hakuna hatua yoyote kati ya hizo tatu inahitilafiana na nyingine. Kwa hakika, yote yamefanywa na Roho mmoja. Ingawa Walitekeleza kazi tofauti katika enzi tofauti na kuzungumza meneno yasiofanana, kanuni ambazo Walifuata katika kazi hizi zilikuwa sawa. Haya ndiyo maono makuu zaidi ambayo watu wote wanapaswa kuelewa.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili(4)" Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Neno la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni