Wakati wa upanuzi wa kikoloni wa Uingereza, elimu na kuwaza kwa hali ya juu katika nyanja kama vile mifumo ya kisiasa ya Magharibi, utamaduni, dini, elimu, na dawa zilianzishwa katika koloni. Utaratibu wa zamani wa kutawala wa nchi zilizotiwa ukoloni ulipinduliwa, na itikadi zilizokuwepo kabla za kikabaila ziliangamizwa. Hili liliweka msingi kwa koloni bila kujua kuanzisha njia ya demokrasia ya kikatiba…
Mwenyezi Mungu alisema, Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu.
Na hivyo majaliwa ya nchi pasipo kujua yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kukosa mwanga wa jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu...
kutoka kwa Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu—Bwana Yesu aliyerudi—Kristo wa siku za mwisho, na pia chini ya hukumu Yake ya haki na kuadibu. Kanisa limejumuisha wale wote ambao wanaikubali kwa kweli kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na wameshindwa na kuokolewa na neno la Mungu. Liliasisiwa kabisa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, na linaongozwa na kuchungwa binafsi na Yeye, na kamwe halikuanzishwa na mtu yeyote. Huu ni ukweli unaokubaliwa na watu wote waliochaguliwa katika Kanisa la Mwenyezi Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni