5/08/2018

Sura ya 19. Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu anapata mwili ili ateseke kwa niaba ya mwanadamu, na kwa kufanya hivyo atasababisha hatima iliyo ya ajabu ambayo itafuata kwa ajili ya mwanadamu. Hatua hiyo ya kazi iliyokamilishwa na Yesu ilikuwa tu kuwa Kwake mfano wa mwili wenye dhambi na kusulubiwa, kuhudumu Kwake kama sadaka ya dhambi na kuwakomboa wanadamu wote, na hii iliweka msingi wa kuingia kwa baadaye kwa mwanadamu katika hatima iliyo ya ajabu. Alizichukua dhambi zote za mwanadamu juu Yake na akawa mfano wa mwili wenye dhambi na akasulubiwa; Alisulubiwa kwa niaba ya wanadamu wote, na baada ya hapo wanadamu wote walikombolewa. Alitumia kusulibiwa Kwake na damu Yake ya thamani kuwakomboa wanadamu. Damu Yake ya thamani ilitumiwa kama sadaka ya dhambi, kumaanisha kwamba ilitumiwa kama ushuhuda kwamba mwanadamu anaweza kuwa bila dhambi na anaweza hatimaye kuja mbele za Mungu: Ilikuwa ni njia ya kumgeuzia Shetani mashambulizi katika vita dhidi ya Shetani. Sasa katika hatua hii, Mungu atakamilisha kazi Yake na kuifanya enzi nzee kufika tamati. Atawaleta wale kati ya wanadamu walioachwa katika hatima yao iliyo ya ajabu. Hivyo Mungu kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na, kama pamoja na kumshinda mwanadamu, Amekuja kustahimili mateso fulani kwa niaba ya mwanadamu ili kwamba mateso yao hatimaye yataondolewa kutoka kwao. Mateso yote ya mwanadamu yataondolewa kutoka kwao kwa njia ya ushuhuda, tendo hili, ambalo ni Mungu kujishuhudia Mwenyewe na kutumia ushuhuda huu na kushuhudia huku kumwangamiza Shetani, kumuaibisha ibilisi, na kuufichua hatima ya ajabu ya mwanadamu. Watu wengine husema: “Kazi ya kupata mwili bado inafanywa na Mungu Mwenyewe. Sio mwili huu ndio uifanyayo, inafanywa chini ya udhibiti wa Roho iliyomo ndani.” Ni sahihi kusema hivi? Sio sahihi. Imesemwa awali kwamba kazi ya ushindi ya Mungu mwenye mwili inafanywa katika ubinadamu wa kawaida, kwamba unachoweza kuona ni ubinadamu wa kawaida, ilhali kwa hakika ni Mungu Mwenyewe anayeifanya kazi hiyo, na kwamba kazi ambayo mwili huu unafanya inafanywa na Mungu Mwenyewe. Kwa kueleza na kufanya ushirika kwa njia hii, watu mara nyingi hudhani kuwa mwili huu ni chombo au ganda tu. Kama Mungu ndani Yake anazungumza ama Anamdhibiti, basi mwili huu unazungumza au unatenda, na haufanyi chochote bila udhibiti wa Mungu. Ikiwa Amedhibitiwa kusema jambo basi Anasema jambo, la sivyo Anasalia kimya. Je, hii ndiyo hali? La, siyo. Maelezo ya nguvu zaidi sasa ni haya: Kipengele kimoja cha Mungu kuwa mwili wakati huu ni kwamba Amekuja kufanya kazi ya ushindi na kuileta enzi hii hadi tamati yake; kipengele kingine ni kwamba mwili kupitia uchungu wa dunia ni Mungu Mwenyewe kuja kupitia uchungu wa dunia—mwili wa Mungu na Mungu Mwenyewe ni kitu kimoja. Mwili huu sio chombo kama watu wanavyomfikiria Yeye kuwa, wala Yeye si ganda tu. Wala Yeye si kitu cha kimwili ambacho kinaweza kudhibitiwa, kama wanavyofikiri watu. Mwili huu ni mfano halisi wa Mungu Mwenyewe. Watu kwa kweli huulewa kwa kawaida sana. Ukifanyiwa ushirika kwa njia hiyo, basi watu watautenga mwili kutoka kwa Roho kwa urahisi. Sasa watu wanafaa kuelewa kipengele kingine: Mungu mwenye mwili amekuja kupitia uchungu wa dunia; taabu na magonjwa yote ambayo kupata mwili kunayapitia ni mambo ambayo Hapaswi kupitia. Watu wengine hufikiri kwamba, kwa sababu Yeye ni mwili wa kawaida, basi mateso haya hayawezi kuepukika. Wanafikiri: “Watu wataumwa na kichwa na kuwa na joto mwilini, na Yeye pia atakuwa na haya. Hili ni jambo ambalo haliwezi kuepukika, kwani Yeye ni mwili wa kawaida. Yeye si wa kuvuka mipaka. Yeye ni mtu wa kawaida na Anapaswa kupitia mateso ambayo watu wanayapitia. Lazima Ahisi joto vile watu wanavyohisi na lazima Ahisi baridi jinsi watu wanavyohisi; Lazima apatwe na mafua jinsi watu wanavyopatwa nayo....” Ukifikiri hivi, basi unaona tu ukawaida wa mwili. Mwili huu wa kawaida ni kama tu mwanadamu bila tofauti yoyote. Kwa ukweli wa hakika, kila mateso anayoyapitia yana maana. Watu kwa kawaida watakuwa wagonjwa, au wapate mateso mengine, na haya ni yale ambayo watu wanapaswa kupitia. Watu wapotovu wanapaswa kuteseka kwa njia hii, na hii ni kanuni ya kawaida. Ni kwa nini Mungu mwenye mwili anastahimili mateso haya? Yesu alifaa kusuluubiwa? Yesu alikuwa mtu mwenye haki. Kulingana na sheria za wakati huo na mambo yote Aliyoyafanya, Yeye hakufaa kusulubiwa. Hivyo ni kwa nini Alisulubiwa? Alisulubiwa ili wanadamu wote waweze kukombolewa. Je, uchungu na mateso ambayo mwili wa sasa umepitia yamefanyika bila kutarajiwa? Au Mungu ameyapanga yote kwa makusudi? Si kwamba Mungu ameyapanga kwa makusudi, wala hayajafanyika bila kutarajiwa. Ni kwamba yamefanyika kulingana na sheria za kawaida. Ni kwa nini Nasema hivi? Ni kwa sababu Mungu amejiweka Mwenyewe miongoni mwa wanadamu ili kwamba Aweze kufanya kazi Yake kwa uhuru. Katika kufanya kazi Yake Yeye ni kama tu mwanadamu na anateseka kama mwanadamu. Kama Angepanga awe na uchungu kwa makusudi, basi Angeteseka kwa siku chache, lakini kwa kawaida hangehuzunishwa. Hiyo ni kusema kwamba Mungu huifanya kazi Yake—Yeye kuupitia uchungu wa dunia haijapangwa kwa makusudi, na hata zaidi uchungu wenyewe unapitiwa bila kufahamu. Ni kwamba Amekuja kuupitia uchungu wa dunia, kujiweka Mwenyewe miongoni mwa mwanadamu, kujiweka Mwenyewe kati ya mwanadamu na kustahimili uchungu sawa na ule wanaoupitia, atendewe sawa na wao, na Asiachiliwe kutoka kwa chochote. Kama tu jinsi ninyi mmepitia mateso, je, Kristo pia hapitii mateso? Jinsi ninyi mnavyowindwa na kufuatiliwa, je, si Kristo pia anawindwa na kufuatiliwa? Watu wanateseka kwa ajili ya magonjwa, hivyo je, mateso Yake yanapunguzwa? Yeye hasemehewi. Je, jambo hili ni rahisi kuelewa? Kuna wengine pia ambao hufikiri kwamba Mungu anafaa kustahimili uchungu huu kwani Alikuja kufanya kazi katika taifa la joka kubwa jekundu. Je, si hili pia sio sahihi? Kwa Mungu, hakuna ubishi kuhusu iwapo anafaa au hafai uchungu wowote; Mungu alisema kuwa Alitaka kuupitia uchungu wa dunia na kwamba, kwa wakati uo huo wa kupitia uchungu huu, Angeupitia kwa niaba ya mwanadamu. Kisha Angewaleta wanadamu mpaka katika hatima yao ya ajabu, na Shetani angeshawishika kabisa. Kwa Mungu, ni muhimu kwamba Apitie mateso haya. Kama Hangetaka kupitia mateso katika hatua hii, kama Angetaka tu kuufahamu uchungu wa mwanadamu na si chochote zaidi ya hayo, basi Angewatumia watu kadhaa wafanye haya kwa niaba Yake. Angewatumia mitume kadhaa au wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu kuichukua nafasi Yake na wapige ripoti Kwake, wakimwambia kuhusu uchungu wenu. Au Angewatumia watu maalum kuwa mashahidi, kuwafanya wastahimili uchungu mbaya zaidi duniani na, iwapo wangeustahimili, basi wangekuwa na ushahidi huu na Shetani angeshawishika kabisa, na siku za baadaye pale ambapo mwanadamu hangeteseka tena zingesababishwa. Je, Mungu angeweza kufanya hili? Ndio, Angeweza kufanya hili. Lakini kazi ya Mungu Mwenyewe inaweza tu kufanywa na Yeye. Ingawa mwanadamu angeshuhudia vizuri, ushuhuda wao usingejulikana pote na Shetani, na angesema: “Kwa kuwa Umekuwa mwili, kwa nini Usipitie uchungu wa dunia Mwenyewe? ...” Hiyo ni kusema, iwapo Mungu hangeifanya kazi hii Mwenyewe, basi mwanadamu kuwa na ushuhuda hakungekuwa na nguvu za kutosha. Kazi ya Mungu lazima ifanywe na Yeye Mwenyewe; hii tu ndio njia ya utendaji. Inaweza pia kuonekana kutoka katika hatua hii ya kazi ya Mungu kwamba kila ambacho Mungu anafanya kina maana, kwamba kila uchungu unaostahimiliwa na kupata mwili una maana. Unaweza kuona kwamba hakuna kile ambacho Mungu anafanya kinafanywa kwa kubahatisha au kwa kupenda, na kwamba Mungu hafanyi chochote kisicho na umuhimu. Kupata mwili kumekuja kufanya kazi Yake na kupitia uchungu wa dunia. Ni muhimu kwamba Mungu afanye kazi hii, na ni muhimu sana, kwa mwanadamu na kwa hatima ya baadaye ya mwanadamu. Yote ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa ajili ya kupatikana kwa mwanadamu—matendo haya yanafanywa na juhudi hii inagharimika kwa sababu ya hatima wa ajabu wa mwanadamu.
    Kipengele cha ukweli ambacho ni kupata mwili kinapaswa kujadiliwa kutoka katika mitazamo kadhaa:
    1. Umuhimu wa mwili wa kawaida.
    2. Hali ya utendaji ya kazi ya mwili wa kawaida.
    3. Maana ya kuja kwa Mungu miongoni mwa mwanadamu kuupitia uchungu wa dunia, hiyo ni, umuhimu wake.
    Ni kwa nini Mungu anataka kufanya mambo haya kwa njia hii? Ingewezekana kutofanya mambo haya kwa njia hii? Kuna hali nyingine ya maana hapa. Kazi ya mwili huu wa kawaida inaweza kumshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu. Kulingana na kiini cha mwanadamu na sheria zinazoongoza maisha, hata hivyo, mwandamu anaendelea kuishi katika utupu, uchungu, huzuni na kutanafusi. Magonjwa ya mwanadamu bado hayawezi kutupiliwa mbali. Kwa mfano, bado unaishi kama kawaida, umeshafanywa mkamilifu na Mungu, upendo wako kwa Mungu umeshafika hatua fulani, pia una uzoefu fulani wa kumwelewa Mungu na tabia yako potovu imetatuliwa. Basi Ninasema kwamba umekamilishwa, kwamba wewe ni mtu anayempenda Mungu, na kwamba uendelee kuishi kwa namna hii. Unahisi kwamba tabia yako potovu imeshasuluhishwa, unafikiri kwamba kwa kuwa umepitia upendo huu kwa Mungu ni jambo la maana sana, unahisi kwamba kuishi na kumpenda Mungu ni jambo kubwa, na unaweza kuchukuliwa kuwa umepiga hatua kadhaa. Tuseme shida za mwanadamu zingetatuliwa kwa kiasi hiki, kisha Mungu aondoke, na kazi ya kupata mwili ilimalizika. Magonjwa ya mwanadamu, utupu wa dunia na huzuni na matatizo ya mwili wa mwanadamu bado yangekuwepo, hivyo lingeashiria kwamba kazi ya wokovu wa Mungu wa mwanadamu haukuwa kwa kweli umekamilishwa. Mtu amekamilishwa na anamwelewa Mungu, anaweza kumpenda Mungu na kumwabudu Yeye. Ilhali, je, anaweza kutatua shida zake mwenyewe na magonjwa yake mwenyewe? Hata palipo na ukweli, shida hizi haziwezi kutatuliwa. Hakuna anayeweza kusema: “Ninao ukweli hivyo, ingawa mwili wangu ni mgonjwa, bado sina wasiwasi.” Hakuna anayeweza kutatua uchungu huu. Unaweza tu kusema: “Ninahisi sasa kwamba kuna umuhimu mkubwa kwa maisha yangu, lakini mimi ni mgonjwa na bado nahisi uchungu mwingi.” Je, hii sio sahihi? Je, hisia hii sio halisi? Hivyo iwapo kupata mwili kungefanya tu kazi ya kuwashinda na kuwakamilisha wanadamu, kama kupata mwili hakungetatua maumivu yote ya mwili wa mwanadamu, badala yake kumkamilisha tu mwanadamu, basi uchungu na magonjwa ya mwanadamu, huzuni wote na furaha ya dunia na matatizo ambayo mwanadamu anakumbana nayo akiishi duniani yangebaki bila kusuluhishwa. Hata kama ungeishi duniani kwa miaka elfu moja, au miaka elfu kumi, na usife kamwe, matatizo haya bado yangesalia bila kusuluhiswa, na suala la kuzaliwa, kifo, magonjwa na kuzeeka bado vingebaki bila kusuluhishwa. Watu wengine ni wapumbavu na wanauliza, “Mungu, je, Huwezi kutatua matatizo haya?” Ninachozungumzia sasa ni tatizo hili, kwamba Mungu amekuja kupitia mambo haya na, baada ya Yeye kuyapitia, Atayatatua kabisa, kutoka kwa mizizi mpaka juu, ili kwamba mwanadamu baada ya hapo hatawahi tena kupitia katika kuzaliwa, kifo, magonjwa na kuzeeka. Yesu alionja kifo; kupata mwili kwa sasa kwa Mungu kunapitia uchungu wa kuzaa na magonjwa (Hahitaji kupitia kuzeeka, na mwanadamu baada ya hapo hatawahi kuwa mzee). Ameupitia uchungu huu wote ili kwamba, mwishowe, unaweza kuondolewa wote kutoka kwa mwanadamu. Baada ya kupata mateso yote kwa niaba ya mwanadamu, Atakuwa basi na ushuhuda wa nguvu ambao hatimaye utaleta hatima ya ajabu ambayo itafuata kwa ajili ya binadamu, ambao ni kuondolewa kwa kuzaliwa, kifo, magonjwa na uzee. Je, si hili ni jambo la maana? Hivyo kupata mwili kunapitia mateso ya dunia, iwe ni kuzaliwa, magonjwa, hali ngumu au uchungu, na haijalishi ni ipi kati ya hali hizi za mateso imestahimiliwa, inapitiwa kwa niaba ya mwanadamu. Anatumika kama ishara na dalili; ameyapitia yote na kuyafanya yote kuwa mzigo Wake ili mwandamu asiweze kuteseka tena kamwe. Maana iko papa hapa. Baada ya mwanadamu kukamilishwa, anaweza kumwabudu Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya mambo kulingana na mapenzi ya Mungu, kulingana na neno Lake na kulingana na matakwa Yake. Kisha Anasuluhisha matatizo na uchungu wa mwanadamu. Hii ndiyo maana ya kuteseka Kwake kwa niaba ya mwanadamu, ambayo ni kwamba mwanadamu duniani hawezi tu kumwabudu Mungu, lakini kwamba pia hawezi kuwa bila mateso hayo na kuzongwa na magonjwa, na vilevile kuwa bila kuzaliwa, kifo, magonjwa na uzee wa dunia; anaweza kuwa bila mafuatano ya maisha na mauti. Kupata mwili kwa Mungu kwa sasa kunastahimili na kupitia uchungu huu na tayari umeshayakabili mambo haya kwa niaba ya mwanadamu. Baadaye, wale watakaosalia hatawahi tena kuteseka na mambo haya kamwe—hii ni ishara. Watu wengine wenye uwongo huuliza, “Unaweza kufanya yote haya kwa niaba ya mwanadamu peke Yako?” Inatosha kwa Mungu mwenye mwili kufanya hili kwa niaba ya mwanadamu; je, vibadala vingine vinahitajika kweli? Mungu Mwenyewe anaweza kufanya chochote na anaweza kuchukua nafasi ya chochote, na Anaweza kuyawakilisha yote na kuwa ishara ya yote, kuwa ishara ya mambo yote yaliyo mazuri na mema, na mambo yote yaliyo mazuri. Zaidi ya hayo, sasa Anayapitia kwa utendaji uchungu wa dunia, hivyo Anahitimu hata zaidi kuwa na ushahidi wa nguvu na kutoa ushuhuda wa nguvu zaidi kumwondolea mwanadamu mateso yote ya siku za usoni.
    Kupata mwili kukifanya kazi katika hatua hizi mbili kwa njia hii inamaanisha kuwa zimefanywa vizuri kabisa na kuwa zimetengeneza mlolongo. Kwa nini Ninasema zimetengeneza mlolongo? Ni kwa sababu kazi ambayo imefanywa katika hatua hizi mbili na kupata mwili kwa kwanza na kupata mwili kwa sasa inatatua mateso yote katika maisha ya mwanadamu na uchungu wa mwanadamu mwenyewe. Mbona ni muhimu kwa kupata mwili kufanya hili Mwenyewe? Uchungu wa kuzaliwa, kufa, magonjwa na uzee uliopo katika maisha yote ya mwanadamu ulitoka wapi? Ni kwa sababu ya nini ndio watu walikuwa na vitu hivi mwanzo? Je, mwanadamu alikuwa na vitu hivi alipoumbwa mara ya kwanza? Hakuwa navyo, sivyo? Hivyo vitu hivi vilitoka wapi? Vitu hivi vilikuja baada ya majaribu ya Shetani, baada ya mwili wa mwanadamu kuwa mpotovu. Uchungu wa mwili, matatizo na utupu wa mwili na ufukara wa dunia ulitoka kwa mateso ya Shetani kwa mwanadamu baada ya kuwapotosha. Mwanadamu kisha alipotoka zaidi na zaidi, magonjwa ya mwanadamu yalikuwa ya kina, mateso yake yakawa makali zaidi, na mwanadamu akahisi utupu zaidi, msiba na kukosa uwezo wa kuendelea kuishi duniani. Mwanadamu alihisi akikosa tumaini zaidi kwa dunia, na hivi vyote ni vitu ambavyo vilitokea tu baada ya Shetani kumpotosha mwanadamu. Hivyo mateso haya yaliletwa kwa mwanadamu na Shetani, na yalikuja tu baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani na kuwampotovu. Hivyo ili kuleta hatima ya ajabu unaomngoja mwanadamu mbali na mfumbato wa Shetani, Mungu lazima apitie mateso haya Mwenyewe. Hata kama mwanadamu sasa hana dhambi, bado anapitia mambo fulani ya uchungu. Shetani bado anaweza kumshika na kumtawala kwa hila mwanadamu na kumfanya apitie mateso na uchungu. Hivyo kwa kupata mwili Mwenyewe kuja kupitia uchungu huu, mwanadamu anarejeshwa kutoka kwa mfumbato wa Shetani na baada ya hapo hahitaji kupata mateso ya chochote tena. Je, maana hii si ya kina sana? Wakati huo, kupata mwili uliokuwa Yesu uliiondoa sheria, ukaitimiza sheria na kuileta Enzi ya Neema. Alileta huruma na upendo kwa mwanadamu na kisha akasulubiwa, hivyo kusamehe dhambi zote za mwanadamu. Alitumia damu Yake ya thamani kumkomboa mwanadamu kutoka kwa Shetani, kuwarudisha mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ingawa mwanadamu alikuwa amepotoshwa na Shetani na alikuwa mwenye dhambi, bado damu Yangu ya thamani ilitolewa badala yake na, kwa kulipa gharama, mwanadamu angerejeshwa. Ingeweza kusemwa kwamba ushuhuda wa damu ya thamani na kusulubishwa kulitumiwa kumkomboa mwanadamu. Baada ya mwanadamu kukombolewa, alisamehewa dhambi zake. Lakini je, kuna dhambi ndani ya mwanadamu? Bado yeye ni mwenye dhambi. Mwanadamu amepotoshwa na Shetani na hivyo bado ni mwenye dhambi, na huu ni ukweli. Kwa hivyo, Mungu amekuwa mwili kwa mara ya pili. Kusamehewa kwa dhambi ya mwanadamu kulipatikana kupitia kwa damu ya thamani ya Yesu na kupitia katika kusulubiwa Kwake. Kisha baada ya dhambi za binadamu kusamehewa, kupata mwili kwa mara ya pili kulikuja. Mwanadamu amerejea mbele za Mungu awali na kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kumekuja kumshinda mwanadamu. Binadamu amerejea mbele za Mungu lakini bado amechanganyikiwa, bado hajui kile Alicho Mungu na anauliza Aliko Mungu. Mungu amesimama mbele yake, ilhali bado hawezi kumtambua, hivyo anaanza kuwa na uhasama kwa Mungu. Kisha Mungu anazungumza na kufanya kazi na, mwishowe, anajilaza kifudifudi kwenye ardhi na kumwona Mungu. Binadamu anaweza kumwona Mungu lakini anamjua kweli? Bado hamjui Yeye, hivyo Mungu bado anahitaji kuzungumza maneno fulani, kumfanya binadamu aelewe zaidi kuhusu ukweli na kumfanya afahamu zaidi kuhusu tabia ya Mungu ili kwamba, mwishowe, binadamu atamjua Mungu. Mwanadamu anaweza kuwa na ufahamu fulani na awe radhi kuishi au kufa kwa ajili ya Mungu, ilhali Shetani bado yuko katika udhibiti wa, na ana maarifa mengi juu ya udhaifu ndani ya mwanadamu. Bado unaweza kumfanya ateseke na pepo wabaya bado wanaweza kufanya kazi kumpinza yeye. Pepo hawa wabaya wanaweza kumsababisha awe katika hali ya kuchanganyikiwa kimawazo, kupoteza ufahamu wake, kutokuwa mtulivu katika mawazo yake na kupata upinzani katika kila jambo. Bado kuna mambo fulani ya kimawazo ndani ya binadamu au roho ambayo yanaweza kudhitiwa na Shetani na kutawaliwa nayo kwa hila. Hivyo inawezekana kwako kuwa na magonjwa, matatizo na kuhisi mwenye kutaka kujitia kitanzi, wakati mwingine pia ukihisi huzuni ya dunia, au kwamba maisha hayana maana. Hiyo ni kusema, kuteseka huku bado kuko chini ya uongozi wa Shetani—huu ni udhaifu wa kusababisha mauti kwa mwanadamu. Shetani bado ana uwezo wa kutumia vile vitu ambavyo amevipotosha na kuvikanyagia chini—huu ni mshiko wa Shetani kwa mwanadamu. Kufuatia hilo, Mungu mwenye mwili alianza hatua ya pili ya kazi, Akiumia kwa niaba ya mwanadamu kwa wakati uo huo Akifanya kazi ya ushindi. Kwa kupata mwili kulipa gharama ya mateso, udhaifu wa kusababisha mauti katika mwanadamu utafikishwa kikomo na kusuluhishwa. Baada ya kupitia kwa uchungu duniani kumrejesha mwanadamu, Shetani hatakuwa na mshiko tena kwa mwanadamu na mwanadamu atamgeukia Mungu kikamilifu. Hili tu ndilo linaloweza kuitwa binadamu kumilikiwa na Mungu kikamilifu. Unaweza kuishi kwa ajili ya Mungu na umwabudu Yeye kwa kweli, lakini si dhahiri kuwa wewe ni mali ya Mungu kikamilifu. Mbona iko hivi? Pepo wabaya wanaweza kutwaa nafasi ili wakufikie, wakufanyie mchezo na bado wanaweza kukutawala kwa hila. Hii ni kwa sababu binadamu ni mpumbavu sana kiasi kwamba, wakati mwingine, hawezi kuelewa tofauti kati ya kuguswa na Roho Mtakatifu na kuingiliwa na pepo wabaya. Je, huu si udhaifu wenye kusababisha mauti? Roho wabaya ni wenye kujitakia mema wenyewe. Wanaweza kuzungumza kutoka ndani mwako au ndani ya sikio lako, au la sivyo wanaweza kuyachanganya mawazo na akili yako, wanazuia kuguswa kwa Roho Mtakatifu ili usiweze kuuhisi, na baada ya hapo wanaanza kukuingilia, kuzifanya fikira zako ziwe zilizochanganyikiwa na akilia yako iwe iliyovurugika, na kukufanya usiyekuwa na utulivu na usiye thabiti. Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya roho wabaya. Kwa kuwa Mungu anafanya kazi Yake, wakati mwanadamu baadaye yuko na hatima yake ya ajabu hataweza tu kumuishia Mungu, lakini hatakuwa tena mali ya Shetani na hapatakuwa na chochote kingine tena ambacho Shetani anaweza kushikilia. Mwanadamu atakuwa mali ya Mungu, mawazo, roho, mwili na pia nafsi. Moyo wako sasa unaweza kumgeukia Mungu, lakini bado wakati mwingine unaweza kutumiwa na Shetani bila hiari yako. Hivyo ingawa binadamu anaweza kuwa na ukweli na aweze kumtii na kumwabudu Mungu kikamilifu, hawezi kuwa huru kabisa kutoka kwa kazi ya pepo wabaya, na hata zaidi aweze kuwa bila magonjwa, kwa sababu mwili wa binadamu na roho yake vimekanyagiwa chini ya miguu na Shetani. Roho ya binadamu ni mahali duni na ndani yake mmeishi Shetani na kutumiwa na Shetani. Shetani bado anaweza kuichukua kutoka kwako na aitawale kwa hila ili kwamba mawazo yako yavurugike na usiweze kuutambua ukweli kwa uwazi. Kupitia uchungu wa dunia kwa kupata mwili na kustahimili Kwakeuchungu huu kwa niaba ya binadamu si jambo lisilo la maana. Ni jambo la muhimu sana. Unaelewa hili, sivyo?
    Sharti muelewe kwamba kupata mwili mara mbili pamoja kumefanya kazi yote ili kuwaokoa binadamu. Kwa kupata mwili mara ya kwanza pekee, basi binadamu hangeokolewa kikamilifu, kwa sababu kupata mwili huko kulitatua tu tatizo la kuziondoa dhambi za binadamu, na hakungeweza kulitatua tatizo la tabia potovu ya binadamu. Kama kupata mwili mara ya pili kungefanikisha tu ushindi juu ya binadamu na kutatua tatizo la tabia potovu ya binadamu, lakini hakungeweza kutatua tatizo la iwapo binadamu ni mali ya Mungu kikamilifu, basi ni kwa kupitia kupata mwili kwa mara ya pili kupitia uchungu wa dunia pia ndipo sehemu hizo za binadamu ambazo zimepotoshwa na Shetani zinaweza kutatuliwa. Hili linatatua tatizo la kuteseka kwa binadamu na uchungu kutoka kwa mzizi kwenda juu—kupata mwili huku kunatatua tatizo hili kabisa. Hizi ndizo hatua za kazi ya kupata mwili huku mara mbili, na hakuna hata moja yao isiyo muhimu. Hivyo hufai kudunisha mateso ambayo kupata mwili kumestahimili. Wakati mwingine Yeye hulia, wakati mwingine anahisi huzuni. Wakati mwingine, wengine humwona Yeye kama mnyonge na mwenye huzuni nyingi. Hufai kuyadunisha mateso haya, na hata zaidi hufai kuwa na dhana kuyahusu. Ukiwa na dhana zozote kuyahusu basi unakuwa mpumbavu na muasi sana. Bila shaka hupaswi kufikiri kuwa uchungu huu ni kitu ambacho kinapaswa kustahimiliwa na mwili huu wa kawaida, na hilo ni baya hata zaidi. Ukisema hivi basi wewe unakufuru dhidi ya Mungu. Watu sharti waelewe kwamba uchungu uliostahimiliwa na kupata mwili kwa kwanza au kupata mwili kwa pili yote ni muhimu, ambayo sio kusema kwamba ni muhimu kwa Mungu Mwenyewe, bali kwamba ni muhimu kwa binadamu. Hili sharti lifanywe kwani binadamu amepotoshwa kwa kiasi kikubwa; kutolifanya hakukubaliki. Ni kwa kufanya hivi tu ndio binadamu anaweza kuokolewa kikamilifu na Mungu. Yeye hufanya mambo kwa njia fulani ili binadamu aweze kuona kwa macho yake wenyewe na ajionee wenyewe. Kila Afanyacho kinawekwa wazi na hakifichwi kwa yeyote. Yeye hapitii uchungu kwa siri, akihofu kwamba iwapo watu wataona basi watakuwa na dhana kuhusu jambo hilo. Yeye halifichi jambo hili kwa mtu yeyote, iwe wao ni wageni kanisani au wakongwe wa kanisa, iwe wao ni wazee au ni vijana, au iwe wanaweza kuupokea ukweli au la. Kwa sababu huu ni ushuhuda, na yeyote anaweza kuthibitisha kwamba kupata mwili kunapitia uchungu mwingi sana wakati Wake na kwa kweli ameyachukua mateso ya binadamu. Yeye hateseki kwa siri kwa siku chache mahali fulani ambako hakuna yeyote anayeweza kujua, akiishi kwa raha na starehe wakati mwingi. Haiko hivi. Kazi na mateso ya Kristo hayajafichwa kwa yeyote, bila kuhofiwa kwamba unaweza kufifia, wala kwamba unaweza kuwa na dhana zozote, wala kuwa na hofu kwamba unaweza kuiacha imani yako. Hii inaonyesha nini, kwamba Mungu hayafichi mambo haya kwa yeyote? Yeye Hana wakati wa kupumzika. Kupata mwili kuna shughuli nyingi sana. Unaweza kumwona sasa akiwa hasemi chochote, lakini bado Anafanya kazi, sio kupumzika. Ingawa Anaweza kuwa hasemi chochote, bado Anaweza kuhisi huzuni moyoni Mwake. Je, binadamu amelielewa hili? Hata kama binadamu akiliona hili, hataweza kujua kunachoendelea. Baadhi ya watu husema kwamba wanajua kwamba Mungu ni mwili wa kawaida, lakini je, unajua kazi ambayo mwili huu wa kawaida unafanya sasa? Hujui. Macho yako ya kimwili yanaweza tu kuona juu na huwezi kuona asili yoyote ya ndani. Hivyo haijalishi ni miaka mingapi ambayo kupata mwili kunafanya kazi, haijalishi ni miaka mingapi ambayo watu wanafikiri Amefanya kazi kirasmi, kwa ukweli wa hakika Mungu hajapumzika hata kidogo. Ingawa Anaweza kuwa hazungumzi sasa hivi, Yeye bado anateseka. Ingawa Hatamki neno lolote na huenda Hafanyi kazi yoyote kwa kiwango kikubwa, bado kazi Yake haijasimama. Watu wengi wanatoa hukumu kuhusu iwapo Yeye ni Mungu mwenye mwili au la, iwapo Yeye kweli ni Kristo kupitia kwa iwapo Anasema chochote. Iwapo Hasemi chochote kwa miaka miwili au mitatu basi Yeye si Mungu, na wanageuka na kuondoka. Imani ya mtu kama huyu kwa Mungu ni kama yeye kukaa kwenye ukingo; mtu wa aina hii hana ufahamu wa Mungu hata kidogo. Kunaweza kuwa na baadhi ya watu ambao bado kwa sasa wanakaa ukingoni na, wakiona kwamba Mungu hajazungumza kwa muda mrefu sana, wanashangaa iwapo Roho ameondoka na iwapo Roho wa Mungu amepanda juu mbinguni. Je, hili sio kosa? Watu hawafai kutoa hukumu jinsi wapendavyo, na hawapaswi kufikiri “Labda hili, labda lile, pengine hiki, pengine kile.” “Pengine” hii ni kosa, ni neno la upumbavu na ni dhana ya ibilisi Shetani! Kazi ya Mungu haijakoma hata kwa sekunde. Hajapumzika ila Amefanya kazi muda huu wote, na yote yanafanyika katika huduma ya binadamu.
Asili ya Kristo sharti ieleweke kutoka katika kila hali. Unawezaje kuijua asili ya Kristo? Cha msingi ni kuelewa kazi ambayo inafanywa na mwili huu. Ukifikiri tu kwamba Roho inafanya mambo kwa njia fulani, lakini mwili haufanyi vile, kwamba mwili unadhibitiwa tu, basi hili si sahihi. Ni kwa nini inasemekana kwamba kupitia mateso, kusulubiwa, kuwashinda binadamu wote na kupitia mateso ya dunia yote ni kazi inayofanywa na Kristo? Ni kwa sababu Mungu aligeuka mwanadamu na kwa sababu haya ni mambo ambayo Mungu hufanya miongoni mwa binadamu. Roho na mwili hufanya kazi kwa pamoja. Sio vile watu huwaza, kwamba ikiwa mwili hautazungumza basi Roho lazima imlazimishe Yeye kuzungumza. Hali sio hivyo. Badala yake inafanywa kwa uhuru kabisa; Roho na mwili vinafanya kitu kimoja. Mwili ukiona jambo kwa njia fulani, basi Roho pia analiona kwa njia hiyo. Hata hivyo inasemwa , vyote vinafanywa kwa pamoja. Ukisema kwamba mwili unachukua uongozi, basi hili pia si sahihi. Mwili kuchukua uongozi, ina maana gani? Kuna maelezo ya nyuma kuhusu hili, ambayo ni kwamba Mungu alikuwa binadamu na vyote ambavyo binadamu anaweza kuona ndivyo ambavyo mwili unaona, kwamba mwili umechukua uongozi wakati wa kupata mwili. Haijalishi jinsi inavyosemwa, kila ambacho mwili unafanya kinafanywa kwa pamoja na Roho. Haiwezekani, kwamba Roho anaona kitu na kuusababisha mwili kuzungumza, na mwili hauzungumzi na kusalia kimya. Hili haliwezekani. Au ikiwa mwili ungependa kuzungumza lakini Roho hatoi maneno. Hili haliwezekani. Ikiwa watu wanafikiri hivyo, basi wamekosea na wanakuwa wapumbavu. Inaweza kuwa kwamba Roho aliye ndani anauchochea mwili kuzungumza, ilhali mwili hauzungumzi? Hili halifanyiki hata. Roho na mwili viko kama kitu kimoja. Ni Roho ambaye amejitokeza ndani ya mwili. Inawezaje kuwa kwamba Roho angependa kuzungumza lakini mwili haungeweza kuzungumza? Au iwapo mwili ulipenda kuzungumza lakini Roho hakutoa maneno? Hakuwezi kuwa na hoja ya aina hii. Mungu mwenye mwili ni ukamilisho wa Roho ndani ya mwili. Mwili Wake unaweza kuzungumza wakati wowote na pahali popote wakati wa kazi Yake. Na kuhusu Roho Mtakatifu kufanya kazi kwa binadamu, punde Roho Mtakatifu anamwacha mtu, anaweza kulitambua. Mungu mwenye mwili hawezi kuwa na hisia ya aina hii. Ufahamu wa binadamu umejaa upotovu na makosa, ukifikiri kwamba Mungu amefanya kazi mpaka hatua hii, na sasa hana kitu cha kusema, na kwamba hata Akitaka kusema jambo, Hana kitu cha kusema. Je, hii ndiyo hali? Anaweza kuzungumza wakati wowote. Roho na mwili daima vimefanya kazi kama kitu kimoja, iwe kwa kazi yoyote au katika kuzungumza kuhusu kipengele chochote cha ukweli.... Haijalishi jinsi unavyolitazama, Roho anakamilishwa ndani ya mwili na Mungu amekuwa mwanadamu; huwezi katu kuzungumza kuhusu kitu kinachoutenga mwili na Roho.
    Kazi ambayo imefanywa na kupata mwili inawezaje kufanyiwa ushirika ili watu waweze kuelewa? Kwanza, usihubiri jinsi mwili wa kawaida unateseka, lakini badala yake hubiri kuhusu jinsi kazi ya kupata mwili mara mbili kumetengeneza mlolongo. Hubiri kuhusu jinsi kupata mwili mara ya kwanza kulisulubiwa kuwakomboa wanadamu wote na jinsi Alivyojichukulia dhambi za binadamu juu Yake Mwenyewe. Hubiri kuhusu vipande hivi viwili vya kazi ya kupata mwili kwa pili, cha kwanza kikiwa Yeye kutatua tabia potovu ya binadamu, na cha pili kikiwa Yeye kuamua hatima ambayo itafuata kwa ajili ya mwanadamu. Mara unapohubiri kuhusu hili, mlolongo utakuwa wazi. Kisha unaweza kuzungumza kutoka kwa hali tofauti. Iwapo watu watauliza maswali fulani, basi shiriki nao tena. Kupitia katika ushirika wa kila mara itakuwa wazi kabisa.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Masomo yanayohusiana: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni