5/25/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mungu Akitoa Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mungu Akitoa Sheria

Amri na sheria ambazo Yehova Mungu aliwapa Waisraeli hazijakuwa na athari kubwa sana kwa sheria ya binadamu tu, lakini pia zimetekeleza jukumu muhimu katika kuanzishwa na utengenezwaji wa ustaarabu wa kimaadili na taasisi za kidemokrasia katika jamii za binadamu.
Neno la Mwenyezi Mungu  | Halafu hebu tusome fahamu zifuatazo.
6. Ibada Mlimani
1) Sifa na Heri (Mat 5:3-12)
2) Chumvi na Nuru (Mt 5:13-16)
3) Sheria (Mat 5:17-20)
4) Kuhusu Hasira (Mat 5:21-26)
5) Kuhusu Uzinzi (Mat 5:27-30)
6) Kuhusu Talaka (Mat 5:31-32)
7) Kuhusu Viapo (Mat 5:33-37)
8) Kuhusu Kujilipiza Kisasi (Mat 5:38-42)
9) Upendo kwa Adui (Mat 5:43-48)
10) Kuhusu Utoaji Sadaka (Mat 6:1-4)
11) Kuhusu Maombi (Mat 6:5-8)
7. Mifano ya Bwana Yesu
1) Mfano wa Mpanzi (Mat 13:1-9)
2) Mfano wa Magugu katikati ya Ngano (Mat 13:24-30)
3) Mfano wa Punje ya Haradali (Mat 13:31-32)
4) Mfano wa Chachu (Mat 13:33)
5) Mfano wa Magugu Umeelezwa (Mat 13:36-43)
6) Mfano wa Hazina (Mat 13:44)
7) Mfano wa Lulu (Mat 13:45-46)
8) Mfano wa Wavu (Mat 13:47-50)
8. Amri
(Mat 22:37-39) Yesu akamwambia, Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri ya kwanza na iliyo kuu. Na ya pili inafanana nayo, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.

Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka, n.k? Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya matendo haya bado yanafaa leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katika Mungu. Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au akitumia lugha gani, asili yake, na sehemu yake ya kuanzia, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo Ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na upana uliotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndani ya mawanda haya.
kutoka kwa Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu


Kuhusu Sisi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni