6/01/2018

Umeme wa Mashariki | "Siri ya Utauwa: Mfuatano" (1) - Ni Jinsi Gani Bwana Ataonekana kwa Mwanadamu Atakaporudi Tena


Katika karne zote tangu Bwana Yesu alipofufuka na Akapaa mbinguni, sisi waumini tumetamani sana kwa hamu kurudi kwa Yesu Mwokozi. Watu wengi wanaamini kwamba utakuwa mwili wa kiroho wa Yesu aliyefufuka ambao utaonekana kwetu wakati Bwana atarudi. Lakini kwa nini Mungu ameonekana kwa mwanadamu akiwa mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho? Mwenyezi Mungu asema, "Mungu Asipokuwa mwili, Atabaki kama Roho bila kuonekana au kuguswa na mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe wa mwili, na mwanadamu na Mungu ni wa dunia mbili tofauti na ni tofauti kwa asili. Roho wa Mungu hana uuwiano na mwili wa mwanadamu, na hakuna uhusiano unaoweza kuwepo kati yao...." "Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake..." (Neno Laonekana Katika Mwili).

Umeme wa MasharikiKanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni