6/01/2018

Umeme wa Mashariki | 33. Mazungumzo Mafupi Kuhusu Chanzo cha Giza na Uovu wa Dunia na Uovu

Umeme wa Mashariki | 33. Mazungumzo Mafupi Kuhusu Chanzo cha Giza na Uovu wa Dunia na Uovu

Yang Le    Mji wa Wuhai, Eneo Huru la Mongolia la Ndani
Nilipokuwa bado shuleni, baba yangu alikuwa mgonjwa na akafa. Baada ya kufa, wajomba wa pande zote mbili za familia ambao mara nyingi walisaidiwa na baba yangu hawakukosa kututunza tu—mama yangu ambaye hakuwa na chanzo cha mapato, dada zangu wawili na mimi—lakini, kwa kinyume, walifanya kila kitu walichoweza kutengeneza faida kutoka kwetu, hata kupigana nasi kwa ajili ya urithi mdogo ambao baba yangu alikuwa ameacha. Kama nimekabiliwa na kutojali kwa jamaa zangu na vitu vyote walivyovifanya ambavyo sikuweza kutarajia, nilihisi uchungu mwingi mno na sikuweza kujizuia kuchukia ukosefu wa dhamiri na ukatili ambao jamaa hawa walionyesha, wakati huo huo nikipata pia hisia ya hali ya asili ya binadamu ya kuwa kigeugeu. Baada ya hapo, wakati wowote nilipoona matukio katika jamii ya wanakaya wakipigana juu ya fedha, au watu wakiiba na kuua juu ya pesa, mara nyingi ningesikitika kuwa ulimwengu leo ulijaa giza mno, kwamba mioyo ya watu kwa kweli ilikuwa miovu na ulimwengu kwa kweli ulikuwa mgeugeu pia. Wakati huo, nilifikiria sababu ya ulimwengu kuwa ulikuwa umejaa giza sana ilikuwa kwa kuwa watu leo walikuwa wamepotoka, kwamba hawakuwa na dhamiri yoyote tena na kwamba kulikuwa na watu wengi waovu mno duniani. Baadaye, ni kwa kupitia tu kula na kunywa maneno ya Mungu nilipotambua kwamba kile nilichokuwa nimefikiria kilikuwa kimebabia tu, na hakikuwa chanzo cha giza na uovu wa dunia. Kutoka kwa maneno ya Mungu niliona wazi chanzo halisi cha giza na uovu ulimwenguni.
Maneno ya Mungu yasema: “Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno yake. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi” (“Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Maarifa ya maelfu kadhaa ya miaka ya utamaduni wa kale na historia vimefunga fikra na dhana na akili ya mwanadamu kwa nguvu sana kiasi cha kutoweza kupenyeka na kutoweza kubadilishwa. … Maadili ya kishirikina yamempeleka mwanadamu 'Kuzimu,' kiasi kwamba mwanadamu anakuwa na uwezo mdogo wa kupinga. Ukandamizaji wa aina mbalimbali umemlazimisha mwanadamu taratibu kuzama chini kabisa Kuzimu…. Maarifa ya utamaduni wa kale kwa taratibu yamemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu na kumweka mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko ya Kale ya Kiyunani Matano vimepeleka fikra na mawazo ya mwanadamu katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje kutoka katika moyo wa mwanadamu bila wao kujua, huku akifurahia kuuchukua moyo wa mwanadamu. Baada ya hapo na kuendelea mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na sura ya mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani…. Genge hili la washiriki jinai! Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani[a] na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemharibu mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anafanana na wanyama wabaya wasioweza kuvumilika, wala hana tena hata chembe ya mwanadamu asilia mtakatifu” (“Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka kwa maneno haya ya Mungu nilielewa kuwa wanadamu ambao Mungu aliumba mwanzoni walikuwa watiifu kwa Mungu, walimwabudu Yeye, walikuwa na dhamiri na mantiki ya wanadamu wa kawaida, na hawakuwa wametiwa najisi, wala hawakuwa wamefanya uovu wowote. Baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, dhambi ilianza kuwa mwenzi wa mwanadamu ya daima. Kwa miaka elfu kadhaa, Shetani ameendelea kumbughudhi na kumpotosha mwanadamu. Huingiza fikra za kupinga maendeleo na nadharia katika mwanadamu, ili kwamba mwanadamu huishi katika kutegemea sumu yake, ikisababisha wanadamu kuwa wapotovu na kukengeushwa milele, na ulimwengu kuwa wa giza na muovu milele. Maneno kama vile "Kila mtu ajitetee mwenyewe bila kujali jaala ya wengine," "Kwa nini niamke mapema kama hakuna faida yangu hapo?" "Mshahara wa ulafi ni mauti," "Akili kidogo si ya muungwana, mtu halisi hakosi sumu," "Maisha ni mafupi, hivyo jifurahishe," "Hakujawahi kuwa na mwokozi" na "Hakuna Mungu hapa duniani kabisa" yote ni sumu ambazo zimeingizwa ndani ya mwanadamu na Shetani. Mambo haya huwa maisha ya watu na kuwa sheria zao za maisha, ili kwamba hakuna mtu anayeamini kuwepo kwa Mungu tena, hakuna yeyote anayemwabudu Mungu tena, na hakuna yeyote anayesikiliza mantiki au dhamiri zao tena. Hakuna tena mahali popote pa Mungu ndani ya moyo wa mwanadamu, hakuna tena vikwazo kutoka kwa sheria na kanuni ambazo zilitoka kwa Mungu. Mwanadamu amelishwa sumu kabisa na kudhibitiwa na Shetani, kiasi kwamba mwanadamu amekuwa mdanganyifu milele, mwenye ubinafsi, wa kudharauliwa, mlafi, mwenye kiburi, mwenye uovu zaidi na aliyepotoshwa, asiyezuiliwa, asiye na sheria hata zaidi, asiyemwamini Mungu na kaidi. Amekuwa pepo mfano halisi wa mwanadamu asiye na dhamiri, maadili, asiye na asili ya mwanadamu, na ya mmoja ambaye uovu ni desturi. Hasa, "Kila mtu ajitetee mwenyewe bila kujali jaala ya wengine " ni sumu ya mauti ambayo Shetani hupanda ndani ya mwanadamu, na hili lilikuwa dhahiri sana na wajomba zangu. Mwanadamu huishi tu kwa ajili ya umimi wake mwenyewe, akiweka faida mbele ya kila kitu kingine, akifikiria " Kwa nini niamke mapema kama hakuna faida yangu hapo?" Ili kupata manufaa zaidi na mengi mno, mtu anaweza kufanya chochote kibaya au kiovu, kufanya mpango wowote usio na haya, wa kudharauliwa au mpango wa kishenzi na wa hila. Hakuna upendo wa kweli au urafiki kati ya watu—yote ni kudanganya, kutumiana na kudhuriana. Wanakaya wa familia moja wanaweza kukosana wenyewe kwa wenyewe na kuwa maadui, kupigana wenyewe kwa wenyewe juu ya fedha na maslahi. Kisha hata zaidi, jamaa na marafiki husahau kanuni zote za maadili kwa ajili ya faida; wanaweza kufanana na wanadamu, lakini wana mioyo ya wanyama. ... Kwamba wanadamu wanaweza kufanya mambo haya maovu yote ni kwa sababu wameathiriwa na usemi wa Shetani "Kila mtu ajitetee mwenyewe bila kujali jaala ya wengine," na wako chini ya utawala wake. Inaweza kuonekana kwamba chanzo cha matendo maovu ya wanadamu ni sumu ya Shetani, na kwamba hiki ndicho chanzo cha giza duniani.
Katika vioja vingi tunavyoishi navyo, tunaweza kuona giza la ulimwengu kwa urahisi sana. Tunaweza kusema kuwa watu ambao huongoza mitindo ya ulimwengu leo wote ni mfano halisi wa Shetani. Hasa, wale ambao wana nguvu na mamlaka ni wakuu wa pepo, na miongoni mwao joka kubwa jekundu ndilo jeusi na ovu mno. Tangu joka kubwa jekundu lichukue mamlaka, limetumia mamlaka katika mikono yake kufanya kila linalowezekana ili kumpotosha mwanadamu, kumpotosha ili awe pepo kwa mfano wa binadamu, kiasi kwamba mwanadamu hafanani tena na mwanadamu. Joka kubwa jekundu hutukuza vurugu na kutetea mapinduzi. Huwa linatumia vurugu kutwaa mamlaka na hutumia vurugu kutawala taifa. Wale ambao huishi chini ya utawala wake pia hufurahia vurugu na hutumia nguvu kwa udhabiti kutatua suala lolote, mara nyingi wakirushiana makonde juu ya jambo ndogo zaidi. Kuna visa vingi zaidi vya wizi na mauaji ambayo hukasirisha watu, na njia ambazo watu huuawa pia huwa ni za ukatili zaidi na za kuchukiza milele. Huu wote ni ukweli ambao upo kwa wote kuuona. Joka kubwa jekundu huwaongoza watu wake "kuendeleza uchumi," na hutukuza misemo kama vile "Haijalishi kama paka ni mweusi au mweupe, mradi anakamata panya," "Ukahaba ni bora kuliko umaskini," "Ukiwa na pesa, unaweza kumfanya shetani asukume mango," "Kitu kingine chochote unaweza kuishi bila, lakini sio pesa" na "Pesa zinaweza kufanya lolote." Kwa utetezi wake wenye nguvu wa mambo kama hayo, watu huheshimu pesa na uwezo, yeyote aliye na pesa na uwezo anaweza kufanikiwa, na yeyote asiye na pesa na uwezo anaweza kudhulumiwa tu na kumezea malalamiko yote, na matokeo yakiwa mioyo ya watu imejazwa na pesa tu. Kwa pesa, mishikamano ya uhusiano wa damu inasahauliwa; kwa pesa na uwezo wanaweza kuchukua na kutoa rushwa, kununua na kuuza viongozi, kuiba, kughilibu, kuwaua watu na kuchukua mali yao, kupigana na kuuana—inaweza kusemwa kuwa watatumia njia yoyote ya lazima. Aidha, ukahaba umeenea kila mahali katika jamii ya leo na maeneo ya umalaya na madawa ya kulevya yanaweza kuonekana kila mahali. Rushwa za ngono na shughuli za ngono ndio mtindo wa kisasa na watu hushikilia maovu, kuheshimu maovu, bila kufikiria kuwa ni aibu, lakini badala yake wakifikiri ni jambo tukufu. Haya pia ni matokeo ya kukuza uchumi, na kufanya uhusiano kati ya watu kuwa uhusiano wa pesa. Joka kubwa jekundu hutumia hili ili kuharibu maadili ya watu na kuwafanya wasiwe na dhamiri. Kipengele cha giza zaidi, cha kupinga maendeleo zaidi cha hili ni kwamba joka kubwa jekundu halikubali kwamba kuna Mungu, lakini badala yake hueneza upingaji Mungu ili watu wamkane Mungu, wakane ukuu Wake, wamtelekeze Mungu halisi na kumwabudu Shetani. Wale wanaoishi chini ya udanganyifu na taarifa ya uongo ya joka kubwa jekundu hawaamini kwamba kuna Mungu na hawamwabudu Mungu halisi, lakini badala yake humfuata Shetani, kutukuza uovu, na wameondolewa kutoka kwa haki ili kwamba milele wamepotoka sana na kukengeuka. ... Sasa ninaweza kuona wazi milele kwamba kwa sababu ya "mfano" huu wa joka kubwa jekundu, mwanadamu alikuwa mpotovu sana na mwovu, bila dhamiri, bila ubinadamu. Mzizi wa uharibifu huu wote upo kwa joka kubwa jekundu kikamilifu. Mhalifu mkuu aliyeumba uovu katika mioyo ya wanadamu, maadili mapotovu na kubadilikabadilika kwa ulimwengu katika jamii leo ni joka kubwa jekundu; kwamba joka kubwa jekundu lilichukua mamlaka ndiyo sababu ya msingi ya giza yote ya dunia na uovu. Kama joka kubwa jekundu lingechukua mamlaka kwa siku moja tu, kama Shetani siku moja haangamizwi, basi wanadamu hawangeweza kuishi katika mwanga na ulimwengu haungejua amani tena.
Baada ya kuona giza na uovu wa joka kubwa jekundu na jinsi linavyowapotosha na kuwakanyagia watu chini, ninahisi hata zaidi utakatifu na uzuri wa Kristo. Kristo ndiye nuru pekee katika ulimwengu huu wa giza, Kristo peke yake ndiye anayeweza kuwaokoa wanadamu na kuwasaidia kutoroka kutoka kwa mahali hapa pa giza na maovu, na ni wakati Kristo atakapotwaa mamlaka tu ndipo nuru itakapoletwa kwa wanadamu. Kwa sababu ni Mungu peke yake aliye na kiini ambacho ni kizuri na chema, Mungu peke yake ndiye asili ya haki na mwanga, Mungu ni ishara pekee ambayo haiwezi kushindwa au kuingiliwa bila heshima na giza na uovu wote, ni Mungu pekee anayeweza kubadilisha uso wa zamani wa dunia nzima na kuleta mwanga ulimwenguni, na ni Mungu peke yake anayeweza kuwaleta wanadamu kwa hatima ya ajabu. Mbali na Mungu, hakuna yeyote anayeweza kutenda kazi hii na hakuna yeyote anayeweza kumshinda au kumwangamiza Shetani. Kama vile inavyosema katika maneno ya Mungu: “Katika dunia hii kubwa, mabadiliko yasiyo hesabika yamefanyika, tena na tena. Hapana aliye na uwezo wa kuongoza binadamu isipokuwa Yeye ambaye Anatawala juu ya kila kitu katika ulimwengu. Hakuna yeyote hodari kwa kazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya binadamu, wala aliye na uwezo wa kuwaongoza wanadamu kurejelea mwanga na ukombozi kutokana na ukosefu wa haki duniani” (“Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Ninataka kurekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu Mimi binafsi ulimwenguni kote, Nitamkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nitawakomesha maadui wasifanye kile wapendacho. Nitakuwa Mfalme wa dunia na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui waanguke mchangani na kukiri makosa yao mbele Yangu” (“Tamko la Ishirini na Saba” katika Neno Laonekana katika Mwili). Niliona katika maneno ya Mungu ukuu Wake na mamlaka Yake, nikaona kwamba Mungu pekee ndiye anayeweza kutuokoa sisi tunaoishi chini ya miliki ya joka kubwa jekundu na ambao tumekanyagiwa chini nalo. Kwa sababu ya hili moyo wangu unatamani hata zaidi kwa Kristo kutwaa mamlaka, na kwa joka kubwa jekundu kufikia mwisho wake karibuni.
Ninashukuru kupatiwa nuru ya maneno ya Mungu ambako kuliniwezesha kuona chanzo cha giza na uovu ulimwenguni, ambako kulisababisha kutokea moyoni mwangu kuchukia kwa kweli kwa joka kubwa jekundu, na ambako kuliniwezesha kuelewa kwamba ni Kristo pekee anayeweza kumwongoza mtu kutoroka kutoka mahali hapa pa giza, kuingia kwenye mwanga. Ni kwa kumfuata Kristo tu na kumwabudu Kristo, mwanadamu anapoweza kutoroka kutoka kwa mateso ya Shetani. Kuanzia leo kwendelea, napenda kutafuta ukweli na kuufuata mwongozo wa Kristo, kuyakubali maneno ya Mungu na kuyafanya kuwa maisha yangu, kujiondolea sumu zote za joka kubwa jekundu, kufumua udhibiti wa ushawishi wa joka kubwa jekundu, kuasi kabisa dhidi ya joka kubwa jekundu, na kufikia wokovu wa Mungu na kukamilishwa na Mungu.
Tanbihi:
a. "Kigeugeu duniani” inaonyesha kwamba ikiwa mtu ni tajiri na mwenye nguvu, watu hujipendekeza naye, na kama mtu hana hela na hana nguvu, watu humpuuza. Kifungu hiki kinahusu udhalimu wa ulimwengu.

kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi MunguNeno la Mwenyezi Mungu 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni