6/18/2018

Chochote Mungu Asemacho Ndiyo Hukumu Hasa ya Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Xunqiu    Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan
Nilikuwa nikidhani kwamba Mungu alimhukumu na kumuadibu mwanadamu wakati tu Alipoufichua upotovu wa asili wa mwanadamu au alipoeleza maneno mkali ambayo yaliuhukumu mwisho wa mwanadamu. Ilikuwa ni baadaye kabisa tu ambapo tukio moja liliponiongoza kutambua kwamba hata maneno mapole ya Mungu pia yalikuwa ni hukumu na kuadibu Kwake. Niligundua kuwa kila neno Alilolisema Mungu ni hukumu Yake kwa mwanadamu.
Hivi karibuni, dada mzee wa familia ya mwenyeji alipata kuhusika na hisia za kimwili, na kwa sababu hiyo aliteseka sana. Niliwasiliana naye kwa karibu mara kadhaa, lakini ilionekana kuwa bure. Alibaki vile vile. Pole pole nikakosa subira, nikifikiria mwenyewe, "Nimezungumza nawe mara kadhaa, lakini hujabadilika. Labda huna shauku katika ukweli. Sitawasiliana nawe kwa karibu tena." Baada ya hapo, sikuhisi tena kuwa radhi kujihusisha naye na ni mara chache sana nilishughulika naye. Siku moja, dada mwingine ambaye nilishirikiana naye alipendekeza kwamba tulipaswa kuomba na dada huyo mzee. Baada ya kusikia hivyo, nilihisi maudhi, "Kwa nini? Ingekuwa ni kupoteza wakati kukaa pamoja naye, na sala zetu hazingezaa matunda." Kwa kweli nilijua hili lilifichua kiburi changu, kilichokuwa ni tabia ya Shetani. Nilikuwa nawadharau wengine na kutoonyesha upendo kwa wengine. Hata hivyo, sikuweza tu kuzuia hili. Tulipoomba pamoja, bado niliona ugumu kuachia huru mawazo na hisia zangu za ndani sana kiasi kwamba nilizama katika giza la kiroho na sikuweza kuhisi kuwa Mungu alikuwa pamoja nami. Aidha, nilihisi kusongwa ndani kana kwamba moyo wangu ulizuiwa na haungeweza kuachiliwa. Baadaye, niliomba mbele ya Mungu juu ya mashaka yangu, "Mungu, nilikuwa nafahamu kiburi na ukatili wangu. Sikuonyesha nadhari wala wema kwa dada yule mzee. Lakini nilishindwa tu kujibadilisha. Mungu, nakusihi Wewe unipe nuru kuhusu ukweli na kujijua vyema." Nilipokuwa nikitoa hiyo sala, nilikumbuka visivyo dhahiri maneno ya Mungu. Mara moja nikafungua kitabu cha neno la Mungu na kupata kauli zifuatazo: “Mbona inasemwa kwamba kiwango cha uamuzi wako kumpenda Mungu, na iwapo kweli umeukataa mwili, kinategemea iwapo una chuki bila sababu kwa ndugu zako, na iwapo, kama una chuki bila sababu, unaweza kuweka kando chuki bila sababu kama hiyo. Ambayo ni kusema, wakati uhusiano wako na ndugu zako ni wa kawaida, basi hali zako mbele ya Mungu pia ni za kawaida. Wakati mmoja wa ndugu zako ni dhaifu, hutamchukia, kumdharau, kumtania, ama kutomthamini. Ikiwa unaweza kumsaidia, utawasiliana naye…. Ukihisi huwezi kumkimu, basi unaweza kumtembelea. Si lazima hili lifanywe na kiongozi wa kanisa—ni jukumu la kila ndugu kufanya kazi hii. Ukiona kwamba kaka au dada yuko katika hali mbaya, unapaswa kumtembelea. Hili ni jukumu la kila mmoja wenu” (“Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, onyo dogo kwamba “wakati uhusiano wako na ndugu zako ni wa kawaida, basi hali zako mbele ya Mungu pia ni za kawaida” lilichapiwa akilini mwangu kwa njia fulani ya wazi. Nilikuwa nikitafuta huku nikifikiria sana kanuni hii. Kupitia kupewa nuru na Roho Mtakatifu, nilihisi kuwa kanuni hii iliyoonekana kuwa ya wazi kwa kweli ilijumuisha uadhama na hukumu, na iliuchoma moyo wangu kama upanga. Mungu daima kwa dhahiri alikuwa amemwambia mwanadamu kwamba ni kwa msingi wa maneno ya Mungu tu wanadamu wanapoweza kuanzisha uhusiano wa kawaida miongoni mwa ndugu wa kiume na kiume, na uhusiano wa mtu huyo na Mungu utakuwa wa kawaida mradi uhusiano wake na ndugu wa kiume na wa kike ulikuwa wa kawaida. Nilipoelewana na wengine, yote niliyothibitisha ilikuwa ni tabia potovu ya Shetani, hasa katika kudharau na kuwakataa wengine. Sikukuwa na uhusiano wa kawaida na watu, kwa hiyo ningewezaje kufurahia uhusiano wa kawaida na Mungu? Lilikuwa jukumu lisilobadilika la mtu kuwatembelea na kuwatumikia ndugu wa kiume na wa kike ambao walikuwa baridi na dhaifu. Yalikuwa ni maisha ya kuishiwa na watu wanaotaka kumpenda Mungu; mwenendo wa ndugu wa kiume na wa kike waliopendana. Kwa kulinganisha, sikujali kabisa nilipopata habari kuhusu hali mbaya ya dada mzee. Ingawa nilionekana kuwasiliana nawe kwa karibu, ndani kabisa sikufanya hivyo kwa moyo uliompenda Mungu. Sikujaribu kadri ilivyowezekana kumsaidia na kumtegemeza. Sikuwasiliana naye kwa karibu kwa uvumilivu kwa moyo mwema au ufahamu wa mtu ambaye alikuwa ameteseka—mtu ambaye alikuwa ameishi katika giza—kumsaidia kutoka kwa hali hasi. Hata niliamua kuwa huyu dada mzee hakuwa na nia ya kuutafuta ukweli, na kwa hiyo nilimdharau na kumuepuka. Kwa hiyo nilipoteza uhusiano mzuri na Mungu na nikawa wa kustahili kuadibu Kwake. Niliteseka kutokana na giza la kiroho. Si ni kweli kwamba tabia ya Mungu ilikuwa imenijia? Nilivyozidi kuifikiria, ndivyo nililivyozidi kuhisi kabisa kuwa kanuni hii hii ni hukumu ya uso kwa uso ya Mungu kwangu. Nilitahayari na kuona majuto kwa kina. Niligundua kwamba nilikuwa mnyama katili asiye na hata chembe ya ubinadamu. Kisha, hata hivyo, uchaji wangu kwa Mungu ukainuka wenyewe na sawia. Nikagundua kwamba tabia ya Mungu ni moja ya uadhama na ghadhabu. Niligundua kwamba Mungu kweli ni mwenye haki mno na mtakatifu. Mungu aliweza kupekua ndani ya kila wazo, hivyo hapakuwa na utorokaji kutoka kwa hukumu Yake.
Hukumu ya maneno ya Mungu ilinisaidia kuacha chuki yangu dhidi ya yule dada mzee. Hivyo, nilipata radhi ya kuwasiliana naye kwa roho ya upendo na wema. Bila kutarajia, hata hivyo, kabla ya wasiliana naye kwa karibu tena, huyu dada mkubwa alikuwa amepokea nuru kutoka kwa Mungu na akayaondokea mashaka yake hasi kwa kuomba na kusikiliza nyimbo za neno la Mungu. Wakati huo, nilijihisi kufurahishwa kwamba hali yake ilikwishakuwa nzuri kabisa. Nilifurahi kwamba Mungu alikuwa ametuongoza, kama Atakavyo daima. Pia nilihisi kutaharishwa tabia mbovu ambayo nilikuwa nimeonyesha.
Nilimshukuru Mungu! Licha ya ukweli kwamba nilikuwa nimeonyesha uasi na upotovu tu wakati wa uzoefu huu, nilijifunza kuwa maneno ya Mungu makali kidogo yalikuwa pia ni hukumu Yake kwa mwanadamu na kuadibu kwa mwanadamu, na kwamba kila neno kutoka Kwake linakusudiwa kuwa la hukumu ya wanadamu. Sitaangalia tena kamwe maneno ya Mungu kwa dhana yangu mwenyewe. Nitakubali hukumu ya Mungu na kuadibu katika maneno na utii kamili. Nitatambua na kupokea ukweli zaidi ili kubadilisha tabia yangu haraka iwezekanavyo.
Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo Juzuu ya 1
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni