6/18/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Si Rahisi Kuwa Mtu Mwaminifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Si Rahisi Kuwa Mtu Mwaminifu
Zixin    Jiji la Wuhan, Mkoa wa Hubei
Kupitia kula na kunywa neno la Mungu na kusikiliza mahubiri, nilikuja kuelewa umuhimu wa kuwa mtu mwaminifu na hivyo nikaanza kufanya mazoezi kuwa mtu mwaminifu. Baada ya muda, niliona kuwa nilipata kuingia kiasi katika kuwa mtu mwaminifu. Kwa mfano: Wakati wa kuomba au kuzungumza na mtu, ningeweza kuongea ukweli na kutoka kwa moyo; niliweza pia kuchukulia kutekeleza wajibu wangu kwa uzito, na wakati nilipofichua upotovu niliweza kujiweka wazi kwa watu wengine. Kwa sababu ya hili, nilifikiri kuwa mtu mwaminifu lilikuwa jambo rahisi sana kutenda, na sio vigumu hata kidogo kama ilivyodaiwa kuwa na maneno ya Mungu: “Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu.” Ni baadaye tu nilipoweza kufahamu kupitia uzoefu kwamba kwa kweli si rahisi kwa mtu mpotovu kuwa mtu mwaminifu. Maneno ya Mungu kwa kweli ni ya kweli kikamilifu na hayajatiwa chumvi kabisa.
Nilipokuwa nikihariri makala siku moja, niliona kuwa dada mmoja kutoka kwa timu ya uhariri ya wilaya fulani alikuwa bora zaidi kuniliko, bila kujali kama ilikuwa kwa kuandika au kuhariri makala. Halafu nikawaza: ni lazima niwe mwenye kutiisha zaidi kwa makala alizohariri, iwapo huenda viongozi wataona kwamba anahariri makala vyema kuniliko na kumpandisha madaraka, jambo ambalo lingeweka cheo changu mwenyewe kwa hatari. Baada ya kusudi hili kutibuka, nilihisi kushutumiwa ndani. Baada ya kuchunguza na kuchangua, nilitambua kuwa haya yalikuwa ni maonyesho ya kujitahidi kwa ajili ya umaarufu na faida, kuwa na wivu wa talanta halisi, na kuwatenga walio tofauti na mimi. Katika mkutano mmoja, mwanzo nilitaka kutangaza upotovu wangu waziwazi, lakini niliwaza: nikiwasiliana nia zangu mbovu, mshirika wangu na dada wa familia mwenyeji wangenionaje? Wangesema moyo wangu ni mbaya mno na asili yangu ni mbovu mno? Sahau, ni bora nisiliseme. Lilikuwa wazo tu, na si kama kwa kweli kuwa nilikuwa nimelifanya kwa vyovyote vile. Na hivyo tu, nilitaja tu kwa juujuu jinsi nilivyokuwa na wasiwasi sana kwamba ningebadilishwa nilipomuona mtu mwingine akihariri makala vizuri, huku nikificha upande wangu wa kweli wa giza. Baadaye, lawama katika moyo wangu iliongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa hiyo niliapa mbele ya Mungu kwamba hili lingetokea mara moja tu, na kwamba wakati ujao haswa ningefanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu.
Siku chache baadaye, nilipokuwa nikipiga soga, nilimsikia dada wa familia mwenyeji akisema jinsi dada wawili waliokuwa wakiishi nyumbani mwake (niliwajua) walivyokuwa wazuri, lakini hakusema lolote juu ya kama mimi nilikuwa mzuri au la, jambo hilo likinikosesha furaha sana ndani. Kumfanya anistahi zaidi, kisha niliorodhesha makosa ya dada hao wawili moja moja, nikionyesha bila kutaja kuwa hawakuwa wazuri kama mimi. Baada ya kusema jambo hili, nilitambua pia kuwa kile nilichokisema hakikuwa cha kufaa, na kwamba nia yangu na kusudi langu vilikuwa ni kuwashusha wengine na kujiinua. Lakini nilikuwa na aibu sana kujiweka wazi kwao, hivyo nikamwambia dada wa familia mwenyeji: "Niliposikia ukiwasifu hao dada wawili, nilihisi kuwa una vijimungu vichache ndani ya moyo wako, na hivyo ni lazima niharibu picha yao kidogo ili kwamba usiwaheshimu sana watu tena." Mara tu sauti yangu ilipotulia, yule dada niliyeshirikishwa naye akasema: "Hili linategemea kama ulikuwa na nia zozote zilizofichika. Ikiwa ni hivyo, basi huo ni udanganyifu mno. Ikiwa sivyo, basi inaweza tu kusemwa ulikuwa ufunuo wa upotovu." Niliposikia akisema hili, niliogopa sana kwamba wangepata picha mbaya yangu, kwa hiyo nikajaribu kujieleza mwenyewe: "Sikuwa na nia zozote zilizofichika. Ni kwamba tu kuwa sikuliwasilisha kwa njia sahihi ….” Baada ya utoaji hoja huu wa kuhadaa, nilikuwa na hasira sana ndani, na wakati nilipoomba nikahisi hasa kulaumiwa: Wewe ni mwenye hila sana. Wewe hunena kwa njia za kuzungukazunguka, kutunga uongo, na kufunika ukweli, kila mara ukificha na kuchomekea makusudi yako maovu na matamanio ya kiburi. Si huku ni kumdanganya Mungu? Hata hivyo, bado sikutubu na nilimuomba tu Mungu anisamehe. Lakini tabia ya Mungu haikosewi, na nidhamu ya Mungu ingenishukia baadaye kidogo.
Siku iliyofuata, kwa ghafla nilipata homa kubwa, na kila kiungo katika mwili wangu kiliniuma. Mwanzoni nilifikiri kuwa nilishikwa na baridi nilipokuwa nimelala usiku na kwamba ningepata nafuu kama ningemeza dawa. Lakini ni nani aliyejua kwamba kunywa dawa hakungeweza kunisaidia, na siku mbili baadaye sikuweza hata kutoka nje ya kitanda. Aidha, ulimi wangu ulifura na kuwa mgumu, na koo langu pia likafura kwa maumivu, likiumia vibaya sana kiasi kwamba sikuweza kuzungumza. Kumeza mate kulikuwa kugumu sana, sembuse kula. Nikiwa nimekabiliwa na ugonjwa huu wa ghafla, nilikuwa na hofu, na nikamwomba Mungu mara kwa mara moyoni mwangu. Wakati huo, ufahamu wa wazi ulizuka ndani yangu ghafla: Ni nani aliyekuacha useme uongo? Ukisema uongo lazima ufundishwe nidhamu. Kwa njia hii, ulimi wako hautatenda dhambi zozote. Ni hapo tu nilipojua kwamba nidhamu ya Mungu ilikuwa imenifika. Kwa haraka niliomba msamaha kwa Mungu moyoni mwangu: "Ee Mungu, najua nilikuwa na kosa. Tafadhali nisamehe. Wakati huu nitajiweka wazi hasa." Baada ya kuomba, niliona kuwa maumivu katika koo langu yalikuwa kwa kuonekana yamepungua. Hata hivyo, wakati mshirika wangu na dada ya familia mwenyeji walipokuja kuniuliza ni kwa nini niliugua kwa ghafla, mwanzoni nilitaka kuwaambia ukweli wote, lakini nikawaza: "Mara nitakapojiweka wazi, mambo mengi niliyoyasema hapo awali yangehitilafiana. Wangesema nina hila mno? Tutawezaje kupatana wakati ujao?" Baada ya kufikiria mambo haya, bado sikuwa na ujasiri wa kuufunua ukweli, na nilisema tu kwa juujuu kuwa niliugua kwa sababu ya kutamani nyumbani. Walipoondoka, aibu moyoni mwangu ilikuwa kama ubapa unaokata. Sikuwahi kufikiri kuwa udanganyifu wangu sasa ungekuja kwa urahisi na bila kukusudiwa. Nililala kitandani, nikihisi kubanwa ndani ya kifua changu na shida ya kupumua, kana kwamba nilikuwa karibu kufa. Niliogopa kwamba ningesongwa, hivyo bila kujali kila kitu nilijikokota kuufungua mlango wa chumba na kuiacha hewa ienee. Ni nani aliyejua kwamba mara tu nilipofika kwa mlango, nilihisi ulimwengu ukizunguka. Giza liliingia mbele ya macho yangu wakati miguu yangu ilipohisi kuwa dhaifu na mwili wangu wote ukaanza kuwa na kijasho chembamba. Kama nimechukuliwa na msukumo, nilijiegemeza kwa fremu ya mlango. Wakati huu, mstari wa neno la Mungu ulikuja ghafla ndani ya moyo wangu: “Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?” (“Tabia Yako Ni Duni Sana!” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kama nimekabiliwa na maneno maadhimu na ya ghadhabu ya Mungu, nilihisi hasira kali ya Mungu kwangu, na moyo wangu haungejizuia kutetemeka kwa hofu. Tabia ya Mungu haiwezi kukosewa, lakini kwa ajili ya sifa yangu mwenyewe, hadhi, na majisifu, nilisaliti kiapo changu mara kwa mara, nikimdanganya Mungu bila haya. Mungu angewezaje kuniruhusu kumtendea Yeye jinsi hii? Nilitweta kwa nguvu na bila kukoma nikamwambia Mungu moyoni mwangu: "Wakati huu bila shaka nitajiweka wazi, bila shaka nitajiweka wazi …” Chini ya nidhamu na adhabu ya Mungu, hatimaye sikuwa na chaguo ila kufunua hadithi yote kwa dada wale.
Ilikuwa ni kupitia tu uzoefu huu nilipoelewa hatimaye maneno ya Mungu kwamba “Wengi wanaona afadhali washutumiwe hadi kuzimu kuliko kuongea na kutenda kwa uaminifu” ni ya kweli hasa na yanakusudiwa watu wenye hila kama mimi. Kwa kuwa asili yangu ya hila ilikuwa imekita mizizi ndani sana yangu na ikawa maisha yangu, kuwa mtu mwaminifu kwangu kulikuwa kugumu zaidi kuliko kukwea juu angani. Nilikuwa nikidhani kwamba kuwa mtu mwaminifu kulikuwa rahisi, lakini hiyo ilikuwa ni kwa sababu matendo yangu hayakuhusisha mambo ya ndani ya nafsi yangu hata kidogo na ulikuwa tu ni mwenendo fulani wa juujuu uliofanywa kwa sharti la mwanzo kwamba hakuna maslahi ya binafsi yangeathirika. Kama leo jambo hili lingeathiri maslahi yangu muhimu au kupambanisha matarajio yangu na hatima, hadhi yangu na heshima, asili yangu ya zamani ingejifichua yenyewe na ningeweza kuwa mtu mwaminifu. Nikiwa na ukweli mbele yangu, nilianza kufahamu kwa kina kwamba kwa kweli si rahisi kuwa mtu mwaminifu. Hasa kwa mtu wa hila kama mimi, siwezi kamwe kuwa mtu mwaminifu pasipo kuondoa visingizio vyote na bila nidhamu ya Mungu na adhabu. Kuanzia sasa kwendelea, nitafuatilia ukweli kwa uangalifu sana, kuyakubali maneno yote ya Mungu, kuielewa asili yangu ya hila hata kwa undani zaidi, na kuondoa visingizio vyote na kuwa mtu mwaminifu, ili niweze kuishi kwa kudhihirisha desturi halisi ya mwanadamu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo Juzuu ya 1

Sikiliza zaidi:Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni