6/05/2018

Ee Mwenyezi Mungu, Mpendwa Wangu Mzuri

Mwenyezi Mungu, mpendwa wangu mzuri, Una moyo wangu.
Unapitia magumu, Unavumilia aibu, yote kwa ajili ya kutuokoa.
Unatoa maisha Yako kwangu, naona jinsi Ulivyo mzuri.
Unakuja duniani kutoka mbinguni, ukiwa mwenye mwili.
Uko hapa Ukiishi na sisi, lakini hakuna anayejua Wewe ni nani.
Sikuota kamwe kuwa Muumba Mwenyewe angekuja ulimwenguni.
Aa … mpendwa wangu! Aa … mpendwa wangu!
Hapa duniani, Wewe ndiye unapendeza sana, Wewe ndiye unayependeza sana.
Mwenyezi Mungu, kipenzi cha moyo wangu! Mpendwa wangu mzuri.
Hakuna moyo, hakuna upendo katika ulimwengu wa mwanadamu unaoweza kufananishwa na Wako.
Unakuwa mwanadamu, mnyenyekevu na aliyejificha, ukituletea wokovu mkuu.
Haki Yako, hekima Yako vinafichuliwa katika mwili.
Unatuletea uzima, Unaleta ukweli;
Unatupa njia sahihi ya kutembea.
Kupata kwako mwili ni kitu ambacho mwanadamu anahitaji zaidi, anahitaji zaidi.
Aa … mpendwa wangu! Aa … mpendwa wangu!
Hapa duniani, Wewe ndiye unapendeza sana, Wewe ndiwe unayependeza sana.
Uasi wa mwanadamu, na uovu, unaonekana wazi katika macho Yako.
Kazi Unayofanya, neno Unalonena, vinaifichua tabia Yako.
Tumebarikiwa sana, tunaweza kukujua Wewe, tabia yetu ikibadilishwa.
Neno na upendo Unayonipa tayari umeushinda moyo wangu.
Umenyakua, Umenyakua moyo wangu. Umeamsha moyo wangu, umeutia msukumo upendo wangu.
Siwezi kusahau jinsi Ulivyo mzuri, siwezi kusahau jinsi Ulivyo mzuri.
Aa … mpendwa wangu! Aa … mpendwa wangu!
Hapa duniani, Wewe ndiye unapendeza sana, Wewe ndiwe unayependeza sana.
Aa … mpendwa wangu! Aa … mpendwa wangu!
Hapa duniani, Wewe ndiye unapendeza sana, Wewe ndiwe unayependeza sana.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

  Jifunze zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni