9/26/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Nilifurahia karamu kubwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Nilifurahia karamu kubwa

Xinwei    Mkoa wa Zhejiang
Juni 25 na 26 zilikuwa siku zisizohaulika. Eneo letu la Zhejiang lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na wafanyakazi wa eneo wakiwa wamekamatwa na joka kubwa jekundu. Ni wachache wetu tu tuliokimbia bila kuumia na, mioyo yetu ikiwa imejaa shukrani, tulikula kiapo cha siri kwa Mungu: kushirikiana vizuri na kazi iliyokuwa ifuate. Kufuatia hilo tulianza kazi yenye msisimko na shughuli nyingi ya kushughulika na matokeo. Na baada ya karibu mwezi mmoja, mipango ilikuwa inakaribia kukamilika. Mwezi huo ulikuwa wa joto, na wakati tulikuwa tumeteseka kimwili mioyo yetu ilikuwa imeridhika yenye furaha, kazi yetu ikiwa imeendelea vizuri mbele ya joka kubwa jekundu. Wakati kazi ilipokuwa imekamilika mimi bila kujua nilijikuta katika hali ya kujiridhisha, nifikiria jinsi nilivyokuwa mwerevu kupanga hiyo kazi vizuri sana. Jinsi nilivyokuwa mfanyakazi mwenye uwezo! Na ilikuwa ni wakati huu ambapo Mungu alipatiliza hukumu Yake kwangu na kuniadibu …
Jioni moja mimi na dada kadhaa tulikuwa tukiongea. Dada mmoja alipendekeza niwaandikie barua fulani na fulani, alinipa kazi fulani, na akaongeza sentensi moja ya mwisho: "Usikurupuke huku na kule tu, sasa ndio wakati wa kujificha na kufanya ibada za kiroho. Zingatia ibada za kiroho na kuingia katika maisha." Mara tu niliposikia maneno haya moyo wangu uliyakataa: Ni lazima niandike barua, ni lazima nifanye kazi. Wakati uko wapi wa ibada za kiroho? Wewe ni mgeni, mimi ni mwenyeji, mimi ninakukinga kwa kutokuruhusu kwenda nje na kufanya kazi, na unanihakiki? Nikiketi nyumbani nikifanya ibada za kiroho siku nzima kama ufanyavyo, ni nani angeenda na kufanya kazi? Kazi inayostahili kufanywa inahitaji kuzingatiwa wakati wa kugawa kazi; na hali inahitaji kuzingatiwa kabla ya kunipogoa. … Asubuhi iliyofuata kila mtu alikuwa akila na kunywa na kuwasiliana maneno ya Mungu, lakini nilikuwa nimevurugika, nikikosa kufurahia kula na kunywa huko. Dada wote walikuwa wakiongea juu ya ufahamu wao wa maneno ya Mungu, huku nikiwa nimekaa kimya. Kisha huyo dada akaniuliza: "Kwa nini huzungumzi?" Nikajibu kwa hasira: "Sina ufahamu wowote." Huyo dada akandelea: "Naona huko katika hali nzuri." Nilijibu bila kufikiri: "Sijahakiki shida yoyote." Lakini kwa kweli mawazo yangu yalikuwa yamepangwa kupasuka na kutoka nje yangu. Hatimaye sikuweza kuyadhibiti tena na nikamwambia kilichokuwa kikinisumbua. Dada huyo alisikiliza na kukiri mara moja kwamba alikuwa mwenye kujiamini mno na hakupaswa kunipa kazi jinsi alivyotaka. Lakini hili halikunitosha kuupuuza upinzani wangu—kwa kinyume, nilihisi kazi yangu wakati huu yote ilikuwa kuweka ukweli katika vitendo, na hakupaswa kusema kuwa sikuwa katika hali njema. Viongozi wa wilaya kando yetu wangefikirije? Kisha dada huyo aliendelea: "Nina wasiwasi kuwa ukifanya kazi tu bila wakati wowote wa kuingia kwako mwenyewe utakuwa mpotovu….” Alivyozidi kuzungumza ndivyo nilivyozidi kumpinga, nifikiri: Unaniita mpotovu? Nafikiri niko katika hali nzuri sana, sitakuwa mpotovu! Sikukubaliana kabisa na mawasiliano yake. Baada ya kifungua kinywa nilikwenda kazini, nikihisi nimekasirika na kufikiri: Nitaacha kazi kama kiongozi, nifanye kazi za kawaida na kumalizana nalo. Kama anasema mimi ni mpotovu na sina ingizo katika maisha, ninawezaje kuwaongoza wengine hata hivyo? Jinsi nilivyozidi kufikiri ndivyo roho yangu ilivyozidi kuhuzunika, nikifikiria: Wakati kazi hizi zitakapokamilika nitajiuzulu. Kisha nikajihisi tu mdhaifu mwili wangu mzima, kana kwamba nilikuwa mgonjwa. Nilitambua kuwa hali yangu ilikuwa mbaya. Niliporudi nyumbani nilikuja mbele ya Mungu na kuomba: "Mwenyezi Mungu, nimekuwa mwenye kiburi sana na mwenye kushikilia maoni yangu, sijauupenda ukweli, sijaweza kukubali kuadibu Kwako na hukumu Yako, kunishughulikia Kwako na kunipogoa. Natumaini kwamba Unaweza kunisaidia na kuulinda moyo wangu, roho yangu, kunifanya niweze kuitii kazi Yako, kujichunguza kwa unyofu, na kujifahamu kwa kweli." Baadaye niliona maneno yafuatayo: "Wewe kujijua ni: Jinsi unavyozidi kuhisi kuwa umefanya vyema katika eneo fulani, ndivyo unavyozidi kufikiria kuwa umefanya jambo sahihi katika eneo fulani, ndivyo unavyozidi kufikiri unaweza kuyaridhisha malengo ya Mungu katika eneo fulani, na ndivyo unavyozidi kufikiri wewe ni wa kustahili kujisifu katika eneo fulani—ndivyo ilivyo vyema zaidi kwako kujijua katika maeneo haya na ndivyo ilivyo vyema zaidi kwako kutafiti kwa kina maeneo hayo ili kuona ni uchafu gani uliomo na nini mambo gani ambayo hayawezi kuyaridhisha malengo ya Mungu. … Jambo hili juu ya Paulo hutupa kila mmoja wetu sisi waumini onyo leo, ambalo ni kwamba wakati tunapohisi kuwa tumefanya vyema hasa, au tunaamini kuwa sisi hasa tumetunukiwa kipaji katika kipengele fulani, au tunahisi hatuhitaji kubadilisha au kukubali kushughulikiwa katika kipengele fulani, tunapaswa kujaribu kujijua zaidi katika suala hilo hasa. Hili ni kwa sababu hungeweza kwa waziwazi kutafiti katika maeneo ambayo tayari unafikiri wewe ni mzuri, na hungeyatafakaria au kuyachangua ili kuona kama yana vitu vinavyompinga Mungu" ("Wewe Kujijua Kunahitaji Kujua Mawazo Yako Yenye Mizizi Imara na Maoni" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yaliuakisi moyo wangu kama kwamba katika kioo chenye kung'aa. Mungu hututaka tujifahamu wenyewe kwa kuelewa mahali ambapo tunadhani tunanawiri, ambapo tunadhani tunafanya mema, na kujielewa wenyewe zaidi katika vipengele ambapo tunadhani hatuhitaji kushughulikiwa. Nikifikiria wakati huo, naona kwamba nilikuwa nikiubeba mzigo. Kazi yangu ilikuwa inaonyesha matokeo mema na nilikuwa nikishughulikia kazi nyingi kubwa vyema, nikidhani kuwa nilikuwa nikiweka ukweli katika vitendo, kwamba haya yote yalikuwa ni maingio halisi na hali yangu ilikuwa nzuri sana—hivyo sikuja mbele ya Mungu na kujichunguza. Leo, kwa sababu ya kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu natambua kwamba wakati huo nilikuwa nikifanya kazi yangu vyema, lakini asili yangu ya kiburi ilikuwa ya kuenea pote. Nilidhani kuwa matokeo ya kazi yangu yalikuwa kwa sababu ya jitihada zangu, kwamba nilikuwa mfanyakazi mwenye uwezo. Nilikuwa mwenye kujikinai kabisa. Kwa kweli, nikifikiria nyuma kwa wakati huo sasa ninatambua kuwa nilikuwa tu nikifanya kazi, kufanya kile nilichoweza kufanya chini ya uongozi na ulinzi wa Roho Mtakatifu, lakini wakati nikifanya kazi sikuutafuta ukweli. Sikuwa na ingizo katika maisha, na kwa muda sikujifahamu mwenyewe, sikuwa na ufahamu wa Mungu, wala uzoefu wangu wa kazi ya Mungu haukuniletea ufahamu wa wazi zaidi wa kipengele chochote cha ukweli. Kwa kinyume nilikuwa mwenye kiburi kiasi cha kutomsikiliza yeyote, na kuiba utukufu wa Mungu kwa ajili ya sehemu yangu ndogo katika kazi Yake kuu. Hivyo tabia ya Shetani niliyoifichua ilikuwa imemkosea Mungu na ilitosha kwa Yeye kunitaja kuwa mwenye dhambi! Lakini kupitia kwa huyo dada, Mungu leo alinikumbusha kuzingatia ibada za kiroho, kuepuka upotovu. Hata hivyo bado sikulikubali. Kwa hakika sikujua vizuri tofauti ya wema na ubaya na nilikuwa mjinga mno kujihusu. Wakati huo huo nilihisi kuwa nilikuwa katika hali ya kutisha. Kama Mungu hakuwa amemsisimua huyo dada kuonyesha hali yangu na kunitaka nirudi kwa Mungu kwa haraka, ningeendelea kuishi katika upotovu, bila kujua kwamba nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, na hatimaye ningekuwa nimefanya kosa kubwa dhidi ya Mungu. Ninaogopa ningekuwa nimekwisha, nimepotea. Wakati huu niliona jinsi nilivyokuwa na haja ya hukumu ya Mungu na kushughulikiwa ili kunilinda kwa njia iliyo mbele. Ingawa katika njia ya hukumu na kuadibiwa, ya kupogolewa na kushughulikiwa, nilihisi nilikuwa nimeaibika na kwamba hii ilikuwa dhiki, huu ulikuwa wokovu wa Mungu. Nilikuwa tayari kuikubali aina hii ya kazi zaidi kutoka kwa Mungu.
Baada ya kupitia kuadibiwa huko na hukumu hali yangu ilibadilika. Tabia na mwenendo wangu zikawa bila makeke zaidi, na mimi nilielewa kazi ya Mungu kidogo, kazi ambayo hailingani na dhana za mwanadamu. Lakini punde, kwa sababu ya ufunuo mwingine wa Mungu, niliona tena kwamba ufahamu wangu ulikuwa wa juujuu mno. Mapema mwezi wa Agosti nilipandishwa cheo kufanya kazi katika eneo. Wakati huo nilikuwa na uchangamfu na nikala kiapo kwa siri: Mungu, asante kwa kuniinua na kwa kunipa agizo kubwa jinsi hiyo. Sitaki kukosea imani Yako kwangu, na ninataka kufanya kila liwezekanalo, na kutumaini kuwa Utaniongoza na kunielekeza. Na hivyo nikajitupa kwenye ratiba ya kazi yenye shughuli nyingi. Kila siku nilikabiliwa na rundo la ujumbe niliouhitaji kujibu, nikitoa mwongozo kwa kila mmoja. Ningeandika mara nyingi hadi asubuhi, lakini nilifurahia kufanya hivyo. Wakati mwingine ningekabiliwa na hali ambayo sikuifahamu au ambayo haikuwa wazi, na ningemwomba Mungu na kuona uongozi Wake na mwongozo, na kazi iliendelea vizuri. Na bila kujua nikawa mwenye kiburi tena, nikifikiri: Mimi ni wa kufaa sana, mimi ni mfanyakazi mwenye uwezo. Siku moja nilikumbana na matatizo kadhaa. Sikujua jinsi ya kugawa vitabu vya eneo hilo, kazi ilikuwa imevurugika, barua zilikuwa zikipelekwa na kurudishwa polepole, na mambo yalikuwa yakicheleweshwa. Kwa hiyo niliomba na kutafakari jinsi ya kuondoa mawazo yangu, na kisha nikahisi yalikuwa wazi: Tafuta mbinu iliyotumika kabla ya tukio hilo kufanyika, jaza nafasi zote za kazi zilizo wazi, na uwateue wafanyakazi kadhaa wapya wa wilaya, halafu kazi inaweza kuendelea mbele kwa wepesi. Kwa hiyo nikaandika barua kwa kiongozi wangu kutoa maoni haya na kuuliza kama ingewezekana au la. Wakati nilipokuwa nikiandika barua hii nilidhani kiongozi huyo hakika angefikiri nimechukua mzigo na kuwa mimi ni mfanyakazi mwenye uwezo. Nilisubiri jibu, nikitumainia sifa zao. Siku chache baadaye nilifurahi kupokea jibu, lakini baada ya kulifungua na kulisoma nilihisi kujawa na huzuni. Huyu kiongozi hakukosa tu kunisifu, jibu lake lilijaa kunishughulikia na kunipogoa, likisema "Wewe una tabia mbaya kufanya hili, unataka umaarufu, na kama utaendelea kwa njia hii utakatiza kazi ya Mungu! Ikiwa wilaya zinaweza kushughulikia kazi zao zenyewe, ziruhusu, kama haziwezi iweke kando tu. Unapaswa kufanya ibada za kiroho kwa haraka na kuandika makala ….” Wakati huo nilikuwa nimeshikilia wema na ubaya na nilihisi kuwa nilikuwa nimetendewa vibaya: "Huyu ni kiongozi wa aina gani, ambaye hatatui matatizo ya wasaidizi? Kumekuwa na tukio katika eneo letu, kazi yetu yote imevurugika: Si tunaka mipangilio? Wilaya zikishughulikia kazi zao zenyewe, ni nini kitakachofanyikia barua hizi zote? Je, vifaa kuhusu kuondoshwa na kufukuzwa na video havitapelelezwa? Ndugu wa kiume na wa kike hawajui jinsi ya kusambaza vitabu vya eneo, na tunakabiliwa na mgogoro, na wanaandika jumbe ili kuharakisha mambo—hili litapuuzwa pia? Sitaki umaarufu, nilitaka tu kuufungua mchakato wetu wa kazi. …"Nilishindwa kabisa kujichunguza na nilikuwa na hasira sana kiasi kwamba nililalamika kwa dada mwenyeji wangu, na hata nikafikiri: Nitaacha kazi, nisipoiacha mimi ni madakizo, nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii sana na bado mimi ni madakizo. Kuna haja gani?
Siku iliyofuata nilisimama mbele ya Mungu na kuchunguza kile nilichokuwa nimekifichua, nikifikiria jinsi ambavyo huyo aliye juu alivyokuwa amesema kuwa kukataa kupogolewa na kushughulikiwa kunaonyesha kushindwa kuupenda ukweli, na watu ambao hawapendi ukweli wana asili mbaya. Kwa hiyo niliangalia kwa utambuzi "Kanuni ya Kukubali Kupogolewa na Kushughulikiwa." Niliona kwamba maneno ya Mungu yanasema: “Watu wengine wanakuwa wa kutoonyesha hisia baada ya kupogolewa na kushughulikiwa; wanahisi wanyonge kiasi cha kutotekeleza wajibu wao na wanapoteza uaminifu wao na kujitolea kwao. Kwanini hivi? Hili kwa kiasi ni kwa ajili ya watu kukosa ufahamu kuhusu kiini cha matendo yao ambayo hupelekea kutokubali kupogolewa na kushughulikiwa. Pia kwa kiasi ni kwa ajili ya watu kutoelewa umuhimu wa kushughulikiwa na kupogolewa, wakiamini hilo kuwa ishara ya kuamuliwa kwa matokeo yao. Kwa sababu hiyo, kimakosa watu huamini kuwa wakiwa na uaminifu fulani na kujitolea kwa Mungu, basi hawawezi kushughulikiwa na kupogolewa; wakishughulikiwa, haiwezi kuwa haki ya Mungu. Kutoelewa kama huku kunawafanya wengi kutoaminika na kutojitolea kwa Mungu. Hakika, yote ni kwa sababu watu ni waongo sana; hawataki kupitia ugumu—wanataka kupata baraka kwa njia rahisi. Hawana ufahamu wa haki ya Mungu. Si kwamba Mungu hajafanya lolote la haki ama kwamba hatafanya lolote la haki, ni tu kwamba watu daima hawafikiri kwamba Anayofanya Mungu ni haki. Machoni pa wanadamu, kama kazi ya Mungu haipatani na mapenzi ya mwanadamu ama kama si matarajio yao, ina maana kuwa Yeye si mwenye haki. Watu kamwe hawatambui wakati kile wanachofanya si sahihi ama haiambatani na ukweli; katu hawatambui kwamba wanampinga Mungu” (“Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalifichua ukweli wangu wa ndani. Sikukubali kupogolewa na kushughulikiwa kwa sababu sikuwa na ufahamu wa asili ya kile nilichokifanya. Nilidhani hakukuwa na kitu kibaya katika kile nilichokifanya, lakini kazi yangu na kutimiza wajibu wangu vilikuwa vimeondoka kwa mipango ya kazi kitambo, lakini nilidhani nilikuwa nikionyesha moyo wa ibada kamili. Nikikumbuka kuwa yule aliye juu alikuwa amesema kuwa "hukuna haja ya kuhangaika juu ya matatizo ya jumla…, hakuna haja ya mtu kulitatua. … Hakuna haja ya uangalifu maalumu, kiongozi wa umma anaweza kulishughulikia." Yule aliye juu hakututaka tushughulikie matatizo ya jumla, wakati mtazamo wangu ulikuwa kwamba maswali yote yaliyotumwa juu kutoka chini yalipaswa kupokea mwongozo na majibu, bila kujali suala lilikuwa kubwa kiasi gani. Ni kama tu matatizo yalishughulikiwa ambapo ningeweza kutulia na kufanya ibada za kiroho. Nilipokabiliwa na ukweli niliona kuwa sikuwa nimeitii kabisa na bila masharti mipango ya aliye juu, na hivyo nilijitahidi kuendelea na mwelekeo mpya wa kazi ya Roho Mtakatifu. Nilikuwa na wasiwasi mwingi mno ambao sikuweza kuuwacha na nilikuwa na kiburi kiasi cha kutokuwa na mantiki. Mungu alikuwa akitumia mratibu kuyashughulikia mambo ndani yangu ambayo hayakulingana na mapenzi ya Mungu, hivyo ningeelewa asili yangu ya kumpinga na kumsaliti Mungu na mwelekeo mpya wa kazi ya Roho Mtakatifu na mapenzi ya Mungu: Ibada za kiroho na kujichunguza zinapaswa kuwa za msingi, na sipaswi kuzingatia kazi tu. Lakini sikutambua kwamba asili ya matendo yangu ilikuwa kinyume na mahitaji ya aliye juu na ilienda dhidi ya, na kumpinga Mungu. Nilishikilia mema na mabaya. Nilishindwa kuielewa roho, nilishindwa kuielewa kazi ya Mungu. Halafu nikakumbuka tena mawasiliano ya mwanadamu: "Haijalishi ni mtu yupi, kiongozi yupi, mfanyakazi, ambaye hunipogoa na kunishughulikia, haijalishi kama linalingana kabisa na ukweli. Almradi linalingana kiasi nalikubali na kulitii, ninalikubali kabisa; sitoi maelezo au kusema kuwa ninakubali asilimia fulani yalo lakini siyo masalio, na kwa kufanya hivyo ninaonyesha kuwa ninaitii kazi ya Mungu. Kama hutayatii maneno ya Mungu na kazi ya Mungu kwa njia hii, itakuwa vigumu kwako kupata ukweli, itakuwa vigumu kwako kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu" ("Jinsi ya Kupata Matokeo Kutoka kwa Kula na Kunywa Maneno ya Mungu" katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha (I)). Ndiyo, hata kama maneno ya mratibu hayakukubaliani kabisa na hali yangu ni lazima niyatii na kuyakubali. Na kwa vyovyote kutimiza kwangu kwa wajibu wangu kulikuwa kumekwisha kwenda kinyume zamani na mipango ya aliye juu na kazi ya Roho Mtakatifu. Si hata ningefanya haraka zaidi kutii, kukubali na kubadilika? Baadaye kwa utambuzi nilifanya kila lililowezekana kutimiza matakwa ya aliye juu wakati nilikuwa nimejiendeleza kidogo na kutulia, kushiriki katika ibada za kiroho, kufanya mazoezi ya kuandika makala, niliona kwamba Mungu Mwenyewe alikuwa akiilinda kazi ya Mungu, na ilikuwa inaendelea kama kawaida, bila kuchelewa.
Matukio haya mawili ya kuadibu na hukumu, ya kupogolewa na kushughulikiwa yalikuwa matatizo, lakini yaliniacha na ufahamu zaidi juu yangu mwenyewe na kwa haraka yalibadilisha hali yangu. Baadaye niliona kwamba maneno ya Mungu yanasema: “Dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote” (“Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Yeye hukulaani ili uweze kumpenda, na ili uweze kujua kiini cha mwili; Yeye hukuadibu ili uweze kuamshwa, kukuruhusu wewe ujue kasoro zilizo ndani yako, na kujua kutostahili kabisa kwa mwanadamu. Hivyo, laana za Mungu, hukumu Yake, na uadhama na ghadhabu Yake—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Yote ambayo Mungu anafanya leo, na tabia yenye haki ambayo Yeye huifanya kuwa wazi ndani yenu—yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na huo ndio upendo wa Mungu” (“Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Sikuweza kujizuia kushusha pumzi: Ndiyo, Mungu ni maonyesho ya uzuri na wema wote, kiini Chake ni uzuri na wema, kiini Chake ni upendo, hivyo kila kitu kitokacho kwa Mungu ni chema na kizuri, iwe ni hukumu, kuwe ni kuadibu, au kama watu, matukio na vitu vilivyo karibu na sisi hutumiwa kutupogoa na kutushugulikia—hii inaweza kuhisi kama tatizo au mashambulizi ya mwili wa mwanadamu, lakini kile Mungu afanyacho ni cha manufaa kwa maisha yetu, yote ni wokovu na upendo. Lakini sikumwelewa Mungu au kazi Yake, wala sikuziona nia Zake njema. Nikiwa nimekabiliwa na hukumu na kuadibiwa, nikiwa napogolewa na kushughulikiwa, nilipinga kwa kutishia kuiacha kazi yangu, nikishindwa kukubali hili kutoka kwa Mungu, kana kwamba watu walikuwa wananisababishia shida. Kupitia ufunuo wa Mungu wa mara mbili, niliona kuwa licha ya kula na kunywa neno la Mungu kwa miaka mingi, kusikia mahubiri mengi sana, msukumo wangu wa kuasi wakati nimekabiliwa na hukumu na kuadibiwa, na kupogolewa na kushughulikiwa, ulikuwa wenye nguvu na niliukataa kabisa. Niliweza kuona kwamba licha ya kumwamini Mungu wakati huu wote tabia yangu ilikuwa haijabadilika, asili ya Shetani ilikuwa yenye mizizi imara, asili ya kumpinga na kumsaliti Mungu, na nilikuwa nimekwisha kuwa nguvu ya kumpinga Mungu. Ghafla nilitambua kwamba nilihitaji hukumu na kuadibiwa, kupogolewa na kushughulikiwa. Bila ya aina hii ya kazi na Mungu singeuona uso wangu wa kweli, singekuwa na ufahamu wa kweli juu yangu mwenyewe, sembuse kutambua jinsi asili ya Shetani ilikuwa na mizizi imara ndani yangu. Ni sasa tu ninapoelewa kwa nini Mungu anasema wanadamu waliopotoka ni adui Yake, na kwamba sisi ni dhuria wa Shetani …. Hili lilifichuliwa kupitia hukumu ya Mungu na kuadibu, kunipogoa na kunishughulikia, na hili ndilo nililojifunza kutoka kwa mchakato huo. Nikitafakari maneno ya Mungu, moyo wangu ukapata nuru. Ninaona jinsi Mungu anavyonipangia kwa uangalifu kupata uzoefu wa kazi Yake, kuingia katika uhalisi wa ukweli, na kuniongoza kwenye njia ya kweli ya uzima. Mungu huniinua na kunitendea kwa huruma. Nilikuja kutambua pia kwamba kila kitu ambacho Mungu hufanya kwa ajili ya mwanadamu ni upendo. Hukumu ya Mungu na kuadibu, kupogoa na kushughulikia ndizo haja kubwa mno za mwanadamu na wokovu bora zaidi.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo Juzuu ya 1
Sikiliza zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni