Waumini wengine wa Bwana hufikiria kwamba yote tunayohitaji kufanya ni kuteseka na kulipa gharama ya kueneza injili ya Bwana, kubeba msalaba ili kumfuata Bwana, na kutenda unyenyekevu, subira na uvumilivu, na kwamba kwa kufanya mambo haya yote tunafuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, na pia wao huamini kwamba kila mara tukifuatilia imani yetu kwa njia hii, basi hatimaye tutaokolewa na Mungu na kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Lakini je, ni sahihi kuwa na ufahamu wa aina hii na kutenda kwa njia hii?
Bwana Yesu alisema, "Wengi wataniita siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujafanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Halafu nitasema wazi kwao, Sikuwajua nyinyi kamwe: ondokeni mbele yangu, nyinyi watenda maovu" (Mathayo 7:22-23). Kwa nini watu hawa ambao huhubiri na kufanya kazi kwa bidii kwa jina la Bwana hawataingia katika ufalme wa mbinguni pekee, lakini pia wataadhibiwa na Bwana?
Mungu anasema "Kazi Yangu ya mwisho si kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, kazi Yangu ni kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote niliyofanya ni sahihi na ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, wala nguvu za asili, ambao ulimleta mwanadamu. Kinyume na hili, Mimi Ndiye ambaye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, mwanadamu anaweza tu kuangamia na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna yeyote atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; mwanadamu atakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde lisiloepukika la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa pekee wa mwanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la pekee la mwanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa mwanadamu. Bila Mimi, mwanadamu atasimama kabisa. Bila Mimi, mwanadamu atakumbana na msiba mkuu huku akikanyagwa na mapepo, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila Mimi Nikiwa na matumaini kwamba mwanadamu atanilipa kwa kutenda mema. Ingawa wachache wanaweza kunilipa, bado Nahitimisha safari Yangu duniani na Nianze kazi ambayo itatokea baada ya hapa, kwa sababu safari Yangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali sana kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu. Huu ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa. Maafa haya hutoka Kwangu na ni wazi kwamba Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamtaweza kuonekana kuwa Wema mbele Yangu, hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuwa vinafaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na ulionyesha tu woga au hali yenu ya uthabiti. Kwa mintarafu hii, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya. Shaka Yangu inaendelea kuhusu vitendo na tabia zenu ambazo Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba sitawahurumia wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Nisingependa kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hataweza kupokea huruma Yangu tena, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele."
kutoka katikaUnapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako
Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni