1/14/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 38


Mwenyezi Mungu alisema, Si kwamba imani yako ni nzuri au safi, lakini badala yake, kazi Yangu ni ya ajabu! Kila kitu ni kwa sababu ya rehema Zangu! Hupaswi kuwa na tabia potovu ya ubinafsi au kiburi hata kidogo, vinginevyo kazi Yangu kwako haitaendelea. Lazima uelewe wazi kwamba iwapo watu wanaanguka au kusimama imara si kwa sababu yao, ni kwa sababu Yangu. Leo, kama huelewi vizuri hatua hii, hutaweza kuingia katika ufalme! Lazima uelewe kwamba kile kinachofanywa[a] leo ni kazi ya ajabu ya Mungu; hakina uhusiano na mwanadamu. Je, matendo ya mwanadamu yana umuhimu gani? Wakati si mwenye ubinafsi, wenye kiburi, na mwenye majivuno, anakatiza usimamizi wa Mungu na kuharibu mipango Yake. Eh, ninyi wapotovu! Lazima unitegemee Mimi leo; usipofanya hivyo, leo Nitakuambia kwamba hutafanikisha chochote kamwe! Yote yatakuwa bure na shughuli zako hazaitakuwa na maana!

     Usipoteze wakati au kusita; leo kila mmoja anayenipenda atakuwa na kazi Yangu ya ajabu ikifanywa juu yake. Siwahitaji wale ambao hawajinyenyekezi, na leo Ninawatumia tu wale ambao wananyenyekezwa kabisa. Ni wale tu wanaonipenda kwa moyo wa kweli, wanaodharauliwa na wengine, wanaoweza kujifunua kabisa Kwangu, Nitakuwa wazi kwako kabisa. Nitakuwezesha kuelewa nia Zangu na wakati wote upo mbele Yangu ukipokea baraka Zangu. Leo wale wanaojitumia kwa ajili Yangu, kujitolea kwa ajili Yangu, na kubeba mizigo kwa ajili Yangu, kamwe Sitawatendea isivyo haki, na hivyo haki Yangu inafichuliwa. Usilalamike kunihusu Mimi; neema Yangu inakutosha. Ni afadhali uje kuichukua ili uweze kuonja utamu usio na kifani. Hii haitasababisha tu upendo kwa ajili Yangu ndani yako, bali itaimarisha upendo huo vile vile.
Kazi Yangu hutekelezwa hatua kwa hatua, na bila shaka siyo isiyojali, au isiyo dhahiri. Ili kunifuata, lazima pia mfanye hivi: Angalieni mwenendo Wangu na mjifunze kutoka Kwangu; kwa njia hii, mkifuata nyayo Zangu basi mtaletwa katika udhihirisho wa ufalme. Shangilia kwa sauti moja! Wanangu! Kazi ya Mungu itafanikishwa juu yenu kundi la watu. Je, hamhisi kuwa mmebarikiwa?
Kwa kweli ni vigumu kuelewa! Nimewaleta hapa leo ili mweze kuiona kazi Yangu ya ajabu!
Tanbihi:
a. Nakala ya asili inaacha "kile kinachofanywa."

 kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili  
Yaliyopendekezwa : Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni