1/15/2019

"Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (8) - Jinsi ya Kupata Njia ya Uzima wa Milele


Kwa maelfu ya miaka waumini wa Bwana wametaka kupata uzima wa milele, lakini hakuna mtu ambaye ameweza kutimiza matamanio haya. Sasa, umechanganyikiwa kuhusu kama kweli kuna njia ya uzima wa milele au la au umechanganyikiwa juu ya jinsi unavyoweza kufuatilia hili kwa njia ambayo utapata njia ya uzima wa milele? Hii video fupi itakuambia jinsi ya kupata njia ya uzima wa milele.

        Mwenyezi Mungu anasema, " Kuingia katika Enzi ya Neno, yaani, Enzi ya Ufalme wa Milenia, ndiyo kazi ambayo inakamilishwa sasa. Kuanzia sasa, fanya mazoezi ya kushiriki kuhusu neno la Mungu. Ni kupitia tu kula na kunywa neno Lake na kulipitia ndipo unapoweza kuonyesha neno la Mungu. Ni kupitia tu maneno yako ya uzoefu ndipo wengine wanapoweza kushawishika na wewe. Kama huna neno la Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuongea neno la Mungu. Kama huwezi, hii yaonyesha kwamba Roho Mtakatifu bado hajakufanyia kazi na ungali bado hujafanywa kuwa mtimilifu. Huu ndio umuhimu wa neno la Mungu. Je, unao moyo ulio na kiu ya neno la Mungu? Wale walio na kiu ya neno la Mungu huwa na kiu ya ukweli, na binadamu kama hao tu ndio wanaobarikiwa na Mungu. Katika siku za usoni, kunayo maneno mengi zaidi ambayo Mungu atatamka kwenye madhehebu na dini zote. Kwanza anaongea na kutoa sauti Yake miongoni mwenu na kuwafanya kuwa kamili kabla ya kusonga mbele na kuongea na kutoa sauti Yake kwa Mataifa na kuwashinda. Kupitia kwa neno, wote wataweza kushawishika kwa uaminifu na kwa kikamilifu. Kupitia neno la Mungu na ufunuo Wake, tabia iliyopotoka ya binadamu imepungua. Wote wanao wajihi wa binadamu, na tabia asi ya binadamu imelegea vilevile. Neno linafanya kazi kwa binadamu kupitia kwa mamlaka na linamshinda binadamu ndani ya nuru ya Mungu. Kazi ambayo Mungu atafanya katika enzi ya sasa, pamoja na jambo kuu katika kazi Yake vyote vinaweza kupatikana ndani ya neno Lake. Kama hulisomi neno Lake, hutaelewa chochote. Kupitia kula na kunywa kwako mwenyewe kwa neno Lake, kuwa na ushirika na ndugu, na kile utakachopitia kwa uhalisi, maarifa yako ya neno la Mungu yatakuwa pana. Na hapo tu ndipo unapoweza kuishi kwa kulidhihirisha kwa kweli katika uhalisia."
kutoka katika Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni